Mitindo ya Lugha Inayowabainisha Wahusika Wazimu katika Riwaya za Habwe

  • Joseph Ondiek Odhong’ Chuo Kikuu cha Maseno
  • Debora Nanyama Amukowa Chuo Kikuu cha Maseno
  • Beverlyne Asiko Ambuyo Chuo Kikuu cha Maseno
Keywords: Motifu, Wahusika wazimu, Mitindo, Uumbaji
Sambaza Makala:

Ikisiri

Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni zinaonyesha ongezeko la idadi ya wazimu katika jamii duniani kote (Kovacevic, 2021). Waandishi wa fasihi wamewaumba wahusika wazimu wakiakisi mazingira wanamoishi. Tangu jadi wahakiki wamejitahidi kueleza vipi wahusika wazimu wametumika katika fasihi. Tahakiki za tamthilia za Shakespeare na za Kiingereza za karne ya ishirini zimeeleza namna na sababu za uumbaji wao. Katika riwaya za Kiswahili hakuna tahakiki zinazoshughulikia wahusika wazimu wala mitindo ya lugha inayowabainisha. Makala hii ilidhamiria kuchanganua mitindo ya lugha inayowabainisha wahusika wazimu katika kazi teule za Habwe. Uteuzi huu ulitokana na Habwe kusifiwa kuwa mwandishi wa fasihi ya kiongofu aliyetumia motifu ya wazimu katika riwaya zake (Gromov, 2018). Riwaya tano za Habwe:  Paradiso (2005), Cheche za Moto (2008), Fumbo La Maisha (2009), Safari ya Lamu (2011) na Kovu Moyoni (2014) ziliteuliwa kupitia usampulishaji dhamirifu kwa kuwa zilikuwa na wahusika wazimu. Nadharia ya umitindo iliyoasisiwa na Bally (1909) ) na kuendelezwa na Thornborrow na Wareing (1998) iliteuliwa kwa ajili ya kazi hii. Muundo wa kiuchanganuzi umetumiwa. Data zilikusanywa kutumia kifaa cha kudondoa data kilichokuwa na vidokezo vya mitindo ya lugha inayotambulisha wahusika wazimu. Matini ya riwaya teule imesomwa kwa makini na vipengele mbalimbali, kurekodiwa. Kisha data imechanganuliwa, kufasiriwa na kuratibiwa kulingana na madhumuni ya utafiti. Matokeo yamewasillishwa kwa njia ya maelezo. Makala hii imedhihirisha jinsi mitindo ya lugha ilivyotumiwa kuwatambulisha wahusika wazimu.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Bally (1909) The origins of translational Equivalents: Translated and edited by Anthony Pym (2022) Routlege UK.

Bollo (2020) Utafiti nyanjani: Ukusanyaji wa data ya fasihi simulizi https://www.youtube.com/channel/UC3EEBQNhW-y6VNg3JgpN76Q

Chiduo, F na wengine (2016) Kamusi Elezi ya Kiswahili: The Jomo Kenyatta Foundation; Nairobi

Feder, L. (1980). Madness in Literature. Princeton University Press U.

Filson, C. (2014). Portrayals of Mental Illness in Literature, From Tennyson to Today. http://talonbooks.com/meta-talon/portrayals-of-mental-illness-in-literature-from-tennyson-to-today

Flores, D. (2014). Social Realism: The Turns of a Term in the Philippines: http://filozofskivestnikonline.com/index.php/journal/article/viewFile/164/150; http://www.journals.uchicago.edu/doi/pdfplus/10.1086/674189

Gelder, M. G., Mayou, R., & Cowen, P. (2001). Shorter Oxford textbook of psychiatry (Vol. 4). Oxford: Oxford University Press.

Gromov, M. D. (2018). Three novels of John Habwe: Social criticism through “new enlightenment”. Journal of Language, Technology & Entrepreneurship in Africa, 9(1), 90- 101. https://www.ajol.info/index.php/jolte/article/view/170520

Habwe, J. (2005) Paradiso: Jomo Kenyatta Foundation Nairobi Kenya.

Habwe, J. (2008) Chche za Moto, Jomo Kenyatta Foundation Nairobi Kenya.

Habwe, J. (2011) Fumbo la Maisha, Jomo Kenyatta Foundation Nairobi Kenya.

Habwe, J. (2011) Safari ya Lamu: Sasa Sema (Longhorn), Narobi.

Habwe, J. (2014) Kovu Moyoni: Book Mark Africa Publishers Nairobi.

Habwe, J. (2016) Curr. Vitae: https://profiles.uonbi.ac.ke/h_john/files/prof._john_habwes_c.v._-_2016.pdf

Kahigi (1994). Lugha katika vitabu vya watoto. Katika Kahigi K.K (Mh), Kioo cha Lugha: Jarida la Kiswahili, Isimu na Fasihi. Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Juzuu, Na. 1. (Uk. 21-36)

Kemunto (2016) Mtindo Katika Utenzi wa Katirifu: Tasnifu ya Uzamili Chuo Kikuu cha Nairobi (Haijachapishwa).

Kombo, D.&Tromp (2006) Proposal and Thesis Writing - An introduction: Pauline Pub. Nairobi.

Kramer, L. (2014). Hamlet: The Motif of Madness: https://prezi.com/hfyob9gzhrpm/hamlet-the-motif-of-madness/

Kovacevic, R (2021) Mental Health : Lessons Learnt in 2020 for 2021 and forward: https://blogs.worldbank.org/health/mental-health-lessons-learned-2020-2021-and-forward Retrived on 4th March 2023

Leech, G. N. (1969) Towards a semantic description of Engish: Longman Green and co. London

Lemon, L. T., & Reis, M. J. (Eds.). (1965). Russian formalist criticism: Four essays (Vol. 405) University of Nebraska Press.

Lugwiri (2011). “Sitiari, Taashira na Tashbihi katika Utenzi wa Tambuka.” Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu Cha Nairobi ( Haijachapishwa)

Madumulla, J. (2009). Riwaya ya Kiswahili: Nadharia, na Misingi ya Uchambuzi. Phoenix Nairobi.

Milner, M. (1987). Suppressed Madness of Sane Men. Tavistock Publication London.

Morris, S. (2012). Shakespeare’s Minds Diseased: Mental Illness and Its Treatment. The Shakespeare Blog. http://theshakespeareblog.com/

Msokile, M. (1992). Misingi ya Hadithi Fupi. Dar es Salaam University Press: Dar es Salaam.

Murumba, J. (2013). Mtindo katika Watu wa Gehenna. Tasnifu ya MA Chuo Kikuu cha Nairobi.

Murungi, G. (2013). Mtindo Unavyoendeleza Maudhui Katika Natala. Tasnifu ya MA Chuo Kikuu cha Nairobi (Haijachapishwa).

Mwamanda, J. (2008) Nadharia ya Fasihi Uchambuzi na Uhakiki, JPD Company & General Supplies Ltd, Da es Salaam.

Nazemi, Z.et al (2022) New insights into literary topoi: A study of ‘madness for guilt and remorse; Razi University (Iran) and University of Córdoba (Spain)

Ntarangwi, M. (2004). Uhakiki wa Kazi za Fasihi. Augustana College: Rock Island

Nyamari, R .K. (2016) Mtindo Katika Utenzi wa Katirifu: Tasnifu ya Shahada ya Uzamili, Chuo Kikuu Cha Nairobi (Haijachapishwa)

Olson A. (2014) Illuminating Schizophrenia: Insights into the uncommon mind. https://www.thriftbooks.com/w/illuminating-schizophrenia-insights-into-the-uncommon-mind_ann-olson/14147337/#edition=60602281

Rono, P. (2013). Uhakiki wa kimaudhui na kifani Wa kidagaa kimemwozea (Doctoral dissertation, University of Nairobi).

ROSS, D. W. (1989): «Revising a Map Misread: Hamlet, Romantic Self consciousness, and the Roots of Modern Tragedy». In Dotter, R.L. (ed.): Shakespeare: Text, Subtext, and Context. Selinsgrove: Susquehanna University Press, 107-123.

Senkoro, F. (1982): Fasihi. Press and Publicity Centre: Dar es Salaam

Wareing, S., & Thornborrow, J. (1998). Patterns in language: Stylistics for students of language and literature. Taylor and Francis.

Veit-Wild, F. (2006). Writing madness: borderlines of the body in African literature. James Currey (GB).

Wamitila, K. (2002). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele vyake. Phoenix Publishers Nairobi

Wamitila, K. (2003) Kamusi ya Fasihi Istilahi na Nadharia: Focus Books, Nairobi

Wamitila, K. (2008). Kanzi ya Fasihi: Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi. Nairobi: Vide Muwa Publishers Ltd, Kenya.

Watuha (2022) Mwongozo wa Bembea ya Maisha - Timothy Arege.. Climax Pubishers Nairobi.

Tarehe ya Uchapishaji
31 July, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Odhong’, J., Amukowa, D., & Ambuyo, B. (2023). Mitindo ya Lugha Inayowabainisha Wahusika Wazimu katika Riwaya za Habwe. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 243-258. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1345