Athari ya Mitindo Mbalimbali ya Breili katika Unukuzi wa Maandishi ya Breili ya Kiswahili

  • Daniel Mburu Mwangi, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Unukuzi, Breili, Usahihi Wa Unukuzi, Uchanganuzi Wa Unukuzi
Sambaza Makala:

Ikisiri

Utafiti huu ulinuia kuchanganua usahihi wa unukuzi wa maandishi ya breili hadi maandishi ya kawaida na kinyume chake, ili kuleta maana iliyokusudiwa. Katika kutimiza lengo hilo, utafiti huu umechunguza changamoto au ugumu wanaokumbana nao wanukuzi wa maandishi haya na athari yake kwa wanafunzi wasioona katika elimu. Utafiti wa nyanjani ndio uliofaa kazi hii, nazo mbinu za kukusanya data zilizozofaa ni hojaji na mahojiano. Wanafunzi walipewa kazi ya kuandika insha zilizopewa wanukuzi walizozinukuu ili kuchanganuliwa. Uchunguzi huu ulikusudiwa kufanywa katika vyuo vya elimu kama vile Chuo Kikuu cha Kenyatta, Chuo Kikuu cha Maseno, Taasisi ya Elimu ya Machakos, Taasisi ya Wasioona ya Kenya na Taasisi ya Elimu ya Kagumo kwa sababu vyuo  hivi ndivyo vilivyo na wahadhiri wengi wasiojua kusoma breili na mara nyingi husaidiwa na wanukuzi kunukuu kazi za breili katika maandishi ya kawaida ili wakapate kusoma na kuelewa. Kutokana na utafiti huu ni wazi kuwa tafsiri ya breili ya Kiswahili hadi maandishi ya kawaida imepungukiwa katika kuwasilisha maana iliyokusudiwa kwa sababu ya ukosefu wa breili sanifu ya Kiswahili, kuwepo kwa changamoto zilizofafanuliwa katika tasnifu hii na ukosefu wa umilisi katika breili ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi na wanukuzi huathiri pakubwa tafsiri ya maandishi haya. Utafiti huu utawanufaisha wanaotumia breili, walimu wao na wanukuzi wa maandishi haya ya breili

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Adjer, D. (2003). Core Syntax: A Minimalist Approach. London: Oxford University Press. https://doi.org/10.1515/tlir.2003.014

Chomsky, N. (1995). Categories and transformations. The minimalist program, 219, 394.

Chomsky, N. (2014). The minimalist program.(20th Anniversary ed.) MIT press.

Haegeman, L. (1995). The syntax of negation (Vol. 75). Cambridge University Press.

Lasnik, H. (1993). Case and expletives revisited: On Greed and other human failings. . Linguistic inquiry, 615-633.

Marantz, A. (1995). The minimalist program. Kwenye The principles and parameters approach to linguistic theory (kur. (pp. 351-382)). Blackwell.

Martos, P. L. (2023). Anthropolojia ya Isimu: Mambo Yanayoathiri Mchakato wa Kujifunza Lugha Mpya. Retrieved from YOAIR: https://www.yoair.com/sw/blog/linguistic-anthropology-factors-affecting-the-process-of-learning-a-new-language/

Mwihaki, A. (2007). Minimalist Approach to Kiswahili Syntax . Kiswahili a referred journal, 70, p. 27.

Newmeyer, F. J. (2021). Chomsky and Usage‐Based Linguistics. A Companion to Chomsky, 287-304.

Obuchi, S. M. (2010). Muundo wa Kiswahili: Ngazi na Vipengele. Nairobi: A~Frame Publishers.

Radford, A. (1997). Syntax: A Minimalist Introduction.( 1st edition) Cambridge: Cambridge University Press.

Simile, O. D. (2022). A Minimalist Approach to the Analysis of the Structure of the KɨbhwanɈi Determiner Phrase. Journal of Linguistics & Language in Education, 16(2).

Tarehe ya Uchapishaji
13 May, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Mwangi, D. (2024). Athari ya Mitindo Mbalimbali ya Breili katika Unukuzi wa Maandishi ya Breili ya Kiswahili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 233-243. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1843