Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu

  • Daniel Mburu Mwangi, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Ishara za Isimu Katika Breili, Mikato Ya Kiingereza, Mikato Ya Kiswahili
Sambaza Makala:

Ikisiri

Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee ya uandishi ambayo watu wasioona hutumia katika mawasiliano na usomi wao. Vilevile, kutokuwepo kwa kipengele muhimu cha matamshi katika kamusi za breili na vitabu vya sarufi hasa vya sekondari. Jambo jingine ni kwamba, wanafunzi wanaotumia breili hupewa maswali mbadala wakati wanapotahiniwa katika maeneo ya fonolojia, mofolojia, na hata katika uchanganuzi wa sentensi. Aidha, kutokuwepo kwa ishara bainifu za isimu katika maandishi ya breili ya Kiswahili. Kichocheo cha mwisho, praima mbili za breili ya Kiswahili: ya 1978 na 1995 zinazotumiwa Afrika Mashariki hazina ishara za kiisimu. Utafiti huu ulikusudia kujibu maswali yafuatayo: changamoto zipi zinazozuia usimilishaji wa ishara za kiisimu katika breili ya Kiswahili? Rasimu za Kiingereza na Kiswahili huathiriana kwa njia zipi? Ukosefu wa ishara za isimu katika breili huathiri ufundishaji wa isimu kwa njia gani? Na mwisho, mikato ya Kiswahili na ya Kiingereza inayotumia nukta zinazofanana huathiri uchapishaji wa vitabu vya isimu kwa njia zipi? Utafiti huu ulilenga kutimiza malengo yafuatayo – kwanza, kubainisha na kutatua changamoto zinazozuia usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Pili, Kuchanganua rasimu ya Kiingereza na ya Kiswahili. Aidha, kuchunguza athari ya ukosefu wa ishara hizi katika ufundishaji wa isimu. Mwisho, kutathmini athari ya matumizi ya mikato inayotumia nukta zinazofanana katika uchapishaji wa vitabu vya isimu. Makala haya yameshughulikia lengo la tatu na la nne. Mbinu za utafiti zifuatazo ndizo zilizotumiwa kukusanya data; uchunzaji, hojaji na mahojiano. Utafiti huu ulichanganua usimilishaji wa ishara hizi kwa kuzingatia nadharia ya usomaji na uandishi wa breili iliyoasisiwa na Kizuka na Fuji (2005). Mtafiti aligundua kuwa uchache wa nukta nundu umesababisha uradidi mwingi wa matumizi ya nukta nundu hizi. Uradidi huu umechangia kuwepo kwa utata  wa kimaana katika fonolojia na sintaksia ya Kiswahili, vikwazo vya ufundishaji wa isimu miongoni mwa wanafunzi wasioona, makosa katika vitabu vya sarufi hasa kidato cha kwanza na kidato cha pili na changamoto zinazotinga usimilishaji wa ishara za kiisimu katika Breili. Utafiti huu utawafaidi wanafunzi wanaotumia breili na walimu na wahadhiri wanaofunza isimu

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Creswell, J. W. (2012). Research Design: quantitative, Qualitative and Mixed Methods approach, 2nd Ed. Sage Publications Inc.

Dooley, D. (1984). Social Research Methods. Prentice Hall inc.

Fanike, J. (1984). Exceptional Child. Oxford University Press.

Johnson, D. G. (2004). Fact Sheet on Braille Writers, Printers and Software. US Department of Education.

Kizuka, Y., Oda, K., & Fujii, K. (1985). 6-7 A Hierarchical Model of Braille Reading. In Proceedings of the 23rd Convention of the Japanese Association of Special Education.

Koenig, A. J. (1996). Selection of Learning and Literacy Media for Children and Youth with Low Vision. In A. L., Corn, & A. J. Koenig, (Eds), Foundations of Low Vision Clinical and Functional Perspectives. American Foundation for the Blind/AFB Press.

Kothari, C. (1985). Research Methodology: Methods and Techniques. New Age International Publishers.

Laroche, L., Labbé, C. A., Benoît, C., St-Pierre-Lussier, F., & Wittich, W. (2017). Current use of contracted and uncontracted French braille in Quebec. British Journal of Visual Impairment, 35(3), 232-246.

Mweu, J. et al. (2007) Braille 1. Basic English Braille; Mudule IEO21 – KISE.

Prima (2004). ‘Braille’ ya Kiswahili. TSB.

Ndurumo, M. (1993). Exceptional Children. Longman Publishers.

Prima (1978). Kiswahili Braille: KIB.

Prima (1993). Kiswahili Braille: KIB.

Travers, R. M. W. (1978). An introduction to educational research. Collier-Macmillan.

Tarehe ya Uchapishaji
22 January, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Mwangi, D. (2024). Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 69-78. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1712