Matumizi ya Riwaya Katika Kutoa Muktadha wa Ufafanuzi wa Muundo wa Sentensi Katika Shule za Upili, Kaunti Ndogo ya Webuye Magharibi

  • Elizabeth Nakhumicha Soita Kibabii University
  • Edwin Masinde, PhD Kibabii University
  • Ben Nyongesa, PhD Kibabii University
Sambaza Makala:

Ikisiri

Kwa muda mrefu mafunzo ya lugha na fasihi yamekuwa yakitengwa ingawa silabasi ya K.I.E. (2002) ilipendekeza mwalimu anapofundisha atumie mwelekeo mse kwa sababu silabasi hii iliorodheresha tu mada za fasihi na lugha bila kutoa mwelekeo wa utekelezaji. Hali hii ilimpa mtafiti msukumo wa kufanya utafiti kuhusu matumizi ya riwaya katika kutoa muktadha wa ufafanuzi wa muundo wa sentensi katika shule za upili, kaunti ndogo ya Webuye Magharibi. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuonyesha matumizi ya riwaya katika kutoa muktadha wa ufafanuzi wa muundo wa sentensi na utekelezaji wake shuleni. Nadharia jumuishi ya ufundishaji wa lugha iliyoasisiwa na Hammerly (1985) ilitumika katika utafiti. Muundo wa usoroveya-elezi ulitumika katika utafiti huu. Shule 17 zilifanyiwa utafiti. Idadi ya walimu 35 na wanafunzi 43 walitafititwa. Deta ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya hojaji, mahojiano na utathmini wa maazimio ya kazi, mipangilio ya masomo na mitihani. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa riwaya inaweza kutoa muktadha wa ufafanuzi wa muundo wa sentensi ingawa changamoto ni kuwa asilimia 68.57 ya walimu hawakutambua pendekezo la silabasi ya K.I.E (2002) la ufundishaji wa mwelekeo mseto. Walimu 11 (31.43%) walikuwa na ufahamu wa kuseta. Walimu 7 kwa 11(63.63%) walipata ugumu wa kutekeleza ufundishaji mseto. Walimu 4 kwa 11 (11.43%) walifundisha riwaya pamoja na muundo wa sentensi wala si kufundisha muundo wa sentensi kwa kutumia riwaya. Walimu 31 kwa 35 ambao hawakuzingatia mwelekeo mseto katika ufundishaji wa muundo wa sentensi kwa kutumia riwaya walionyesha uwezekano wa riwaya kuweza kutumika kufundisha muundo wa sentensi. Mtafiti alipendekeza walimu wahamasishwe kuhusu utekelezaji wa mwelekeo mseto wa fasihi na lugha darasani ili kuboresha lugha kwa ujumla. Kwa mujibu wa utafiti huu, vitabu vya riwaya vinapaswa kuteuliwa kwa uangalifu ili viwe na manufaa kwa ufundishaji wa muundo wa sentensi.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.
Tarehe ya Uchapishaji
26 July, 2019
Jinsi ya Kunukuu
Soita, E., Masinde, E., & Nyongesa, B. (2019). Matumizi ya Riwaya Katika Kutoa Muktadha wa Ufafanuzi wa Muundo wa Sentensi Katika Shule za Upili, Kaunti Ndogo ya Webuye Magharibi. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 1(1), 13-22. Retrieved from https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/15