Matumizi ya Vifaa vya Kisasa vya Ufundishaji na Ujifunzaji Vinavyotumika Kufundisha na Kujifunza Sarufi Katika Shule za Upili Zilizoko Kaunti Ndogo ya Moiben, Uasin Gishu

  • Melly Joachim Kibabii University
  • Misiko Wasike, PhD Kibabii University
  • Edwin Masinde, PhD Kibabii University
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yanawasilisha matokeo ya awali ya utafiti kuhusu matumizi ya vifaa vya kisasa katika ufundishaji na ujifunzaji wa sarufi. Yanalenga matumizi ya tarakilishi na vipakatalishi vinapotumika na vinuruweo. Serikali ya Uasin Gishu imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa kuna matumizi ya Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika ufundishaji katika shule za upili. Shule za upili zimepokea tarakilishi, vipakatalishi na vinuruweo kutoka serikali hii. Uhakiki wa mtihani wa Eastern Zone Joint Exam (EZOJE) unaofanywa na shule zote katika kaunti ndogo ya Moiben ulionyesha matokeo duni katika karatasi ya pili ya Kiswahili. Sarufi huchukua asilimia 50% ya karatasi ya pili; hivyo, ufundishaji wake unapaswa kutiliwa maanani. Hojaji, mahojiano na uchunzaji zilitumika kukusanya data. Walimu walichaguliwa kwa kuzingatia vipindi vya sarufi ya Kiswahili wanavyovifundisha. Wanafunzi wa kidato cha tatu walihusishwa kwa kuwa mada zilizolengwa na utafiti zilifundishwa katika kidato cha tatu. Utafiti huu ulitumia usampulishaji wa kimakusudi. Shule moja ya kitaifa, shule tatu za viwango vya zaidi ya kaunti, shule saba za viwango vya kaunti na nne za viwango vya kaunti ndogo zilihusishwa katika utafiti. Shule ya wasichana ya Moi iliteuliwa kimaksudi kwa kuwa ni shule ya kitaifa pekee katika kaunti ndogo ya Moiben. Walimu kumi na watano na wanafunzi mia moja na watano walijaza hojaji kuhusu umuhimu wa matumizi ya vifaa hivi. Ilibainika kuwa vifaa vya kisasa ni muhimu sana vikitumika kufundisha na kujifunza sarufi. Matokeo yalithibitisha kuwa, vifaa hivi hurahisisha uelewekaji wa mada zinazofundishwa, huleta uchangamfu darasani, huokoa muda na kuwashirikisha wanafunzi katika somo. Hivyo, makala haya yanatoa pendekezo kwa walimu kuachana na matumizi ya vifaa vya kimapokeo na kuingiza usasa katika ufundishaji wao.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.
Tarehe ya Uchapishaji
22 August, 2019
Jinsi ya Kunukuu
Joachim, M., Wasike, M., & Masinde, E. (2019). Matumizi ya Vifaa vya Kisasa vya Ufundishaji na Ujifunzaji Vinavyotumika Kufundisha na Kujifunza Sarufi Katika Shule za Upili Zilizoko Kaunti Ndogo ya Moiben, Uasin Gishu. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 1(2), 55-61. Retrieved from https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/26