Changamoto Zinazowakumba Vijana katika Tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga

  • Jackson Ndung’u Mwangi, PhD Chuo Kikuu cha KCA
Keywords: Dhana ya Vijana, Kitumbua Kimeingia Mchanga, Uhalisia
Sambaza Makala:

Ikisiri

Katika ulimwengu wa sasa, kuna mabadiliko chungu nzima yanayoshuhudiwa duniani yanasababishwa na masuala anuwai kama vile maendeleo ya kiteknolojia pamoja na utandarithi yanayoathiri pakubwa maisha ya vijana. Nchini Kenya, vijana wana umuhimu wa kipekee kwani wanatekeleza majukumu muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi. Isitoshe, idadi ya vijana kote ulimwenguni imeendelea kuongezeka kila uchao na imepiku ile ya wazee.  Kwa hivyo, ni nyema kujadili changamoto zinazowakabili na kupendekeza hatua za kukabiliana nazo. Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuchanganua changamoto zinazowakumba vijana pamoja na athari zake katika ya tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga ya S.A Mohamed (2000). Mada hii ilichaguliwa kwa misingi kwamba vijana wanakumbwa na changamoto nyingi katika maisha yao zinazowaathiri kwa kiasi cha haja na kutinga juhudi za kuafikia jaala zao. Utafiti huu ulilenga kubainisha changamoto zinazowakumba vijana katika tamthilia hii na kutambua mbinu ambazo vijana hawa wanazua ili kukabiliana nazo. Nadharia ya Uhalisia ilitumika kwa sababu ilionekana kufaa  zaidi  kuchanganua  changamoto  zinazowakumba  vijana. Hii ni kwa sababu  changamoto  hizi  zina uhalisia mkubwa katika maisha yao. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuchunguza na kueleza namna changamoto za vijana zinavyojitokeza katika tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga na kisha kubainisha hatua zinazochukuliwa kuzitatua changamoto hizo. Utafiti huu ni wa kimaelezo na kiudhamano kwani ulihusisha kuchanganua matini zinazohusiana na mada husika. Sampuli katika utafiti huu iliteuliwa kimakusudi kwani ndiyo ingempa mtafiti data aliyonuia kuipata. Ni bayana kuwa utafiti huu utaifaa jamii ya wasomi wanaoshughulikia maswala ibuka katika jamii.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Chepkwony, A. (2005). The Youth: A challenge to the Church in Africa Today.

Flaubert, G. (1850). Realism Theory in the Making: A Ideological Perspective. London. Merlin Press.

Hegel, G. (1979). Introduction to Aesthetics. Oxford: Clarendon.

Kezilahabi, E. (1971). Rosa Mistika. Nairobi: Kenya Literature Bureau.

Kezilahabi, E. (2007). Dunia Uwanja wa Fujo. Vide Muwa Publishers Limited.

Lukacs, G. (1963). The meaning of Contemporary Realism. London: Merlin Press. Mbatiah, M. (2005) Upotevu . Nairobi: Phoenix Publisher Limited.

Mohamed, S. (2000) Kitumbua Kimeingia Mchanga. Nairobi: Oxford University Press, East Africa Limited.

Momanyi, C. (2006) Tumaini: Vide Muwa.

Mutua, J. (2007). Mitazamo ya Vijana na Wazee kuhusu ukombozi wa mwanamke katika tamthilia tatu za Kiswahili. Chuo Kikuu Cha Nairobi (tasnifu ambayo haijachapishwa).

Naliaka, R. (2012). Uhakiki wa hali ya vijana katika Riwaya ya Vipanya vya Maabara. Chuo Kikuu Cha Nairobi (tasnifu ambayo haijachapishwa).

Njogu, K. na Chimera R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Natharia na Mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Obure, E. (2012). Dhuluma dhidi ya vijana wa kike katika riwaya za Rosa Mistika na Tumaini. Chuo Kikuu Cha Nairobi (tasnifu ya M.A).

Wafula, R. na Njogu, K. (2007). Nadharia za uhakiki wa fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Tarehe ya Uchapishaji
14 November, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Mwangi, J. (2022). Changamoto Zinazowakumba Vijana katika Tamthilia ya Kitumbua Kimeingia Mchanga. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(2), 69-77. https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.959