Mitazamo ya Lugha na Utambulisho wa Kijamii Miongoni mwa Wazungumzaji wa Kĩndia na Kĩgĩchũgũ

  • Peris Mwihaki Ndung’u Chuo Kikuu cha Egerton
  • Raphael Mwaura Gacheiya, PhD Chuo Kikuu cha Egerton
  • Catherine Wawasi Kitetu, PhD Chuo Kikuu cha Egerton
Keywords: Utambulisho wa Kijamii, Lugha, Jamiilugha, Mitazamo, Kĩndia, Kĩgĩchũgũ
Sambaza Makala:

Ikisiri

Lugha ni kipengele muhimu cha utambulisho ambacho huweza kuwaunganisha, kuwatenganisha au kuwabagua wazungumzaji katika jamii. Utambulisho ni mtazamo wa kibinafsi wa mtu, yeye ni nani na vibainishi vinavyoashiria ushirika wake katika kikundi fulani cha kijamii. Mitazamo au maoni ya wazungumzaji kuhusu wao ni akina nani au utambulisho wao katika jamii, yanaweza kutofautiana na ushahidi wa kiisimu ambao huweka makundi ya wazungumzaji wanaozungumza lahaja mbalimbali kama wanajamii wa lugha moja. Dhana hii hudhihirika kwa wazungumzaji wa Kĩndia na Kĩgĩchũgũ ambao huchukuliwa kuwa wao si Wakikuyu hata ingawa kiisimu wameainishwa na kuwekwa katika kundi moja kama Wakikuyu. Makala haya yanaazimia kuchunguza mitazamo wanayoendeleza wazungumzaji wa Kĩndia na Kĩgĩchũgũ kuhusu utambulisho wao wa kijamii katika jamii. Mtazamo ni tathmini, chanya au hasi, kuelekea kitu au mtu, ambayo hujidhihirisha kwa imani, hisia au nia ya mtu mwenyewe. Kuna wakati wazungumzaji huweza kujinasibisha na kikundi fulani cha kijamii na wakati mwingine kukana utambulisho huo kutokana na sababu mbalimbali. Hii hutokana na wao kuendeleza mitazamo mbalimbali kuhusu utambulisho huo. Utafiti wa makala haya uliongozwa na nadharia ya Tajfel na Turner (1979). Data ilikusanywa kupitia mahojiano na kuchanganuliwa kimaelezo. Matokeo ya utafiti yalidhihirisha kuwa wazungumzaji wa Kĩndia na Kĩgĩchũgũ wana mitazamo hasi na chanya kuhusu utambulisho wao wa kijamii. Mitazamo hasi ya kubaguliwa na kudhalilishwa ilichangia watafitiwa kukana utambulisho wao na jamiilugha ya Wakikuyu na kujitambulisha kama Wakĩrĩnyaga.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Crystal, D. (2000). Language death. Cambridge: Cambridge University Press.

Edwards, J. (2013). Sociolinguistics. Avery short introduction. Oxford: Oxford University Press.

Giles, H. (1979). Ethnicity markers in speech. In Scherer, K. R., & Giles, H. (1979). Social markers in speech. Cambridge England: Cambridge University Press.

Gituru, M. (2019). Unyambulishaji wa vitenzi katika Kĩgĩchũgũ. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Chuka.

Greenberg, J. H. (1948). The Classification of African languages. American Anthropologist, NS, 50 (1): 24-30. https://doi.org/10.1525/aa.1948.50.1.02a00050

Guse, L., & Samuelsson, M. (2009). Construction of identities in Kenya: A Discursive analysis regarding the communicative meaning of identity building in interpersonal communication and mass media among young adults in Nairobi. B.A Thesis. University of Kalmar, Institutionen för Kommunikation och Design.

Guthrie, M. (1967). The classification of the Bantu languages. London: Dawson’s of Pall Mall

Macharia, D. (2011). Phonological variation and change in Gikuyu: A case study of Mathira dialect in Kenya. Unpublished MA Thesis, Kenyatta University

Msanjila, P. (2011). “Utata wa kutumia lugha kama kibainishi cha utambulisho wa mzungumzaji,” Swahili forum 18 (2011): 87-9. https://nbn-resolving.org/urn:nbn:de:bsz:15-qucosa-90552

Msanjila, P., Kihore, Y. M., & Massamba, D. (2009). Isimu jamii sekondari na vyuo. Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.

Mukhwana, A. (2014): Attitudes towards Kiswahili in urban Kenya. International Journal of Scientific Research and Innovative Technology. Vol. 1 No.4; October 2014.

Mutahi, K. (1983). Sound changes and classification of the southern dialects of southern Mt. Kenya. D. Reimer, Berlin.

Mutahi, K. (1977). Sound changes and classification of the southern dialects of southern Mt. Kenya. Tasnifu ya uzamifu, Chuo Kikuu cha Nairobi.

Mwangi, Irungu. (2019, August 21). Kirinyaga community ushes for identification. https://www.kenyanews.go.ke/kirinyaga-community-ushes-for-identification/

Mwaniki, D. (2014). A synchronic survey of Kiembu dialects. Tasnifu ya uzamili, Chuo Kikuu cha Nairobi.

Ngure, K., & Karuru, D. (2015). Language and identity within the decision theoryframework: The case of the Rendille people of Kenya. International Journal of Liberal Arts and Social Science 3(8). https://ijlass.org/data/frontImages/gallery/Vol._3_No._8/4._17-24.pdf

Tajfel, H., & Turner, J.C. (1986) The Social Identity Theory of Intergroup Behavior. In: Worchel, S. and Austin, W.G. (Eds.), Psychology of Intergroup Relation (pp. 7-24), Chicago: Nelson Hall Publishers. http://web.mit.edu/curhan/www/docs/Articles/15341_Readings/Intergroup_Conflict/Tajfel_&_Turner_Psych_of_Intergroup_Relations_CH1_Social_Identity_Theory.pdf

Tajfel, H. (1982a). Social identity and intergroup relations. Cambridge: Cambridge University Press.

Tajfel, H. (1982b). The Psychological structure of intergroup relations. Katika Tajfel, H. (Ed.), Differentiation between social groups: Studies in the social psychology of intergroup relations. London: Academic Press.

Tajfel, H. (1981). Human groups and social categories: Studies in social psychology. Cambridge: Cambridge University Press.

Tajfel, H., & Turner, J. C. (1979). An integrative theory of intergroup conflict. In Austin, W. G. & Worchel, S. (Eds.), The social psychology of intergroup relations (pp. 33-37). Monterey, CA: Brooks/Cole.

Tajfel, H. (1978). Differentiation between social groups: Studies in the social psychology of intergroup relations. London: Academic Press.

UNHCR. (2017). “Hapa ni nyumbani kwetu”. Walio wachache wasio na utaifa na juhudi zao za kutafuta uraia. https://www.refworld.org/cgibin/texis/vtx/rwmain/opendocpdf.pdf?reldoc=y&docid=5a017db84

Waita, N. (2020). Ngugi wa Thiong’o’ cosmogenic meta-myth in the perfect nine: The epic of Gikuyu and Mumbi (kenda muiyuri: rugano rwa Gikuyu Na Mumbi). International Journal on Studies in English Language and Literature (IJSELL) 8(7): 28-34 http://dx.doi.org/10.20431/2347-3134.0807004

Wakiuru, K. (2013). Uchanganuzi wa lugha na itikadi za mamlaka ya kijinsia katika nyimbo za harusi kutoka jamii ya wakikuyu wilaya ya Kirinyaga.Tasnifu ya uzamili, Chuo Kikuu cha Egerton.

Tarehe ya Uchapishaji
29 Septemba, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Ndung’u, P., Gacheiya, R., & Kitetu, C. (2022). Mitazamo ya Lugha na Utambulisho wa Kijamii Miongoni mwa Wazungumzaji wa Kĩndia na Kĩgĩchũgũ. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 215-223. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.769