‘Huyu Mtu Hasimami’: Uhuishi katika Mazungumzo ya Daktari na Wanaume katika Kliniki ya Afya ya Uzazi, Kenya

  • Melvin Atieno Ouma Chuo Kikuu cha Egerton
  • Jonathan Furaha Chai, PhD Chuo Kikuu cha Pwani
  • Catherine Wawasi Kitetu, PhD Chuo Kikuu cha Egerton
Keywords: Afya Ya Uzazi, Sehemu Za Siri, Uhuishaji, Ujinaishaji, Wanaume
Sambaza Makala:

Ikisiri

Lugha ni kiungo muhimu katika mawasiliano kati ya daktari na mgonjwa. Katika kliniki ya afya ya uzazi, kutaja sehemu za mwili kwa majina yao ni kigezo muhimu katika utoaji na upokeaji wa huduma za afya. Ujinaishaji ni jambo la zamani kama ilivyo ubinadamu. Ujinaishaji wa sehemu za siri ina historia ndefu kutoka karne ya zamani sana. Ujinaishaji wa sehemu hizi ni jambo linalofanyika katika mataifa yote ulimwenguni. Makala haya yanaangazia uhuishi unavyotumiwa na wanaume kama mkakati wa mazungumzo katika kliniki ya afya ya uzazi. Kuafikia hili, makala haya yatashughulikia majina ambayo wanaume wanayapa sehemu zao za siri katika kliniki ya afya ya uzazi. Pia yatafafanua sifa na tabia za kibinadamu zinazopewa sehemu za siri katika mazungumzo ya wanaume na daktari kuhusu matatizo ya afya ya uzazi. Majina kama vile dick, mwanaume, uume, mkuki, chuma na huyu mtu ni baadhi ya majina wanaume walitumia kutaja sehemu zao za siri. Sehemu za siri ya wanaume ilipewa sifa na tabia za kibinadamu kupitia urejeleo kwa ngeli ya A-WA. Matumizi ya ngeli ya A-WA ni idhibati kuwa dhakari ni kama binadamu na wala si sehemu ya mwili ya kawaida kama inavyodhaniwa. Uhuishi ulijitokeza katika mazungumzo kupitia maneno kama vile anakataa, hakubali, hasimami, anajikunja. Semi za wanaume zinaonyesha kuwa dhakari ina uwezo wa kuamuka na kufanya kazi. Dhakari ina uwezo wa kutoa adhabu. Ina uwezo wa kusimama. Ina uwezo wa kuwa imara na ina uwezo wa kuenda. Sehemu za siri za mwanamume zina maisha yake na fahamu zake kando na yule mwanamume anayemiliki sehemu hizo. Kupitia mazungumzo ya daktari na mgonjwa, sehemu za siri (dhakari) ndio sehemu ya mwili inayothaminiwa zaidi miongoni mwa wanaume.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Aceto, M. (2002). Ethnic personal names and multiple identities in Anglophone Caribbean speech communities in Latin America. Language in Society, 31(4), 577-608.

Al-Dilaimy, H., & Thabiti, E. (2017). The Concept of Naming and Definite Descriptions in English and Arabic: A Semantic and Sociolinguistic Analysis. Journal of Al-Maaref University-College, 357-377.

Allan, K. (2001). Natural Language Semantics. Oxford: Blackwell.

Cameron, D. (1992). Naming of parts: Gender, culture, and terms for the penis among American college students. American Speech, 67(4), 367-382.

Cornog, M. (1986). Naming Sexual Body Parts: Preliminary Patterns and Implications. Journal of Sex Research, 22(3), 393-398.

Creswell, J. (1998). Qualitative Inquiry and Research Design: Choosing among five traditions. Thousand Oaks,CA: Sage.

Frege, G. (1892). "On Sense and Reference". Translated.

Gacheiya, R. (2018). Peo na Mikakati ya Kimazungumzo katika Uwasilishaji wa Ujinsia miongoni mwa Wazulufu. Egerton University: Unpublished PhD Thesis.

Guest, G., Namey, E., & Mitchel, M. (2013). Collecting Qualitative Data: A Field Manual for Applied Research. London: Sage Publications Ltd.

Howlett, B., Rogo, J. E., & Shelton, T. G. (2014). Health-care Research Methods. In B. R. Howlett, Foundations of Evidence-Based Practice for Health Professionals: An Interprofessional Approach. Jones and Barlettt Publishers.

Izugbara, C. O. (2005). Hypothesis on the origin of hegemonic masculinity. Sexuality in Africa Magazine, 2(1), 13-14.

Jayaraman, R. (2005). Personal identity in a globalized world: Cultural roots of Hindu personal names and surnames. The Journal of Popular Culture, 38(3), 476-490. doi:10.1111/j0022-3840.2005.00124.x

Massamba, D. (2004). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI.

Msanjila, Y., Kihore, Y., & Massamba, D. (2009). Isimu Jamii, Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam, Tanzania: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.

Musyimi, D. (2011). Maana za Majina ya Watu katika Jamii ya Wakamba. Chuo Kikuu cha Kenyatta: Tasnifu ya Uzamili, Haijachapishwa.

Olatunji, A., Issah, M., Noah, Y., Muhammed, A. Y., & Sulaiman, A. R. (2015). Personal name as a reality of everyday life: Naming dynamics in select African societies. The journal of Pan African studies, 8(3), 72-90.

Ouma, M. (2018). Mitazamo ya Vijana wa Kiume wa Kenya kuhusu Ubabedume: Mkabala wa Uchanganuzi Hakiki Usemi. Egerton University: Unpublished Masters' Thesis.

Potts, A. (2000). The essence of the hard on” hegemonic masculinity and the cultural construction of “Erectile dysfunction. Men and masculinities, 3(1), 85-103. doi:10.1177/1097184x00003001004

Potts, A. (2001). The man with two brains: Hegemonic masculine subjectivity and the discursive construction of the unreasonable penis-self. Journal of Gender Studies, 10(2), 145-156. doi:10.1080/09589230120053274.

Resani, M. (2016). Maana katika Majina ya Wabena nchini Tanzania. Mulika, 35.

Russell, B. (1905). "On Denoting". Retrieved from http://cscs.umich.edu/

Sanders, J. S., & Robinson, W. L. (1979). Talking and not talking about sex: Male and female vocabularies. Journal of Communication, 29(2), 22-30.

Sanders, J. S. (1978). Male and female vocabularies for communicating with a sexual partner. Journal of Sex Education and Therapy, 4(2), 15-19. doi:10.1080/01614576.1978.11074587.

Udechukwu, G. I., & Nnyigide, N. M. (2016). The religious and socio-cultural implication of African names: igbo naming system as a paradigm. AFRREV IJAH: An International Journal of Arts and Humanities, 5(3), 89-103.

Yusuf, N., Olatunji, A. & Issah, M. (2014). Yoruba Names as Reflection of People's Cultural Heritage. In A. A. al (Ed.), Bringing Our Cultures Home Festchrift for Bode Ayayi at 70 (pp. 186-196). University of Ilorin: Department of Linguistics and Nigerian Languages.

Tarehe ya Uchapishaji
29 September, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Ouma, M., Chai, J., & Kitetu, C. (2022). ‘Huyu Mtu Hasimami’: Uhuishi katika Mazungumzo ya Daktari na Wanaume katika Kliniki ya Afya ya Uzazi, Kenya. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 131-141. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.685