Nafasi ya Riwaya za Kingano za Kiswahili katika Harakati za Kupigania Hadhi-Msingi ya Mwanamke. Mfano Riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba

  • Furaha J Masatu Mwenge Catholic University
  • Venancia F Hyera Mwenge Catholic University
  • Osmunda R Ndunguru Mwenge Catholic University
Keywords: Ukombozi Wa Mwanamke, Ufeministi, Hadhi-Msingi, Riwaya Za Kingano, Riwaya Ya Marimba Ya Majaliwa
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yanalenga kuonesha namna riwaya za kingano za Kiswahili zinavyoweza kutumika kumpigania na kumkomboa mtu mnyonge hususani mwanamke na mtoto. Baadhi ya watu wanadhani ngano ni kwa ajili ya watoto kuburudika na kuwatia hofu kama njia ya kuwajengea adili. Ukweli ni kuwa, ngano ni zaidi ya burudani na hofu. Ndani ya ngano mna mambo mazito yanayoweza kumlea mtoto kwa kumuumba upya ili awe kiumbe kipya cha haki na usawa duniani bila hofu. Baadhi ya ngano zinaonekana kuvuka mipaka ya kitamaduni ya mafunzo anayostahili kupata mtoto. Mfano wa ngano hizo ni riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba inayomsawiri mwanamke kama kiumbe mwenye mapaji na uwezo mkubwa hata kumshinda mwanaume dhalimu. Mtazamo huu ni kinyume na mafunzo yanayopatikana katika ngano nyingi tulizonazo sokoni - kutokana na utiisho uliokita katika mfumodume. Makala yanabeba muhtasari wa uchunguzi uliongozwa na nadharia ya Ufeministi kuitalii riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008). Uchunguzi umebaini kuwa, mwandishi amemchora mwanamke kwa mtazamo chanya kwa kuonesha hadhi-msingi alizoumbiwa mwanamke mbali ya changamoto anazozipitia katika kujitetea. Ingawa mwanamke anaonekana kuendelea kukandamizwa na mfumodume, bado ukombozi wa kifikra unamfanya asikubali kuutii na kuuabudu. Katika mapambano haya, mwanamke amefanikiwa kuonesha hadhi-msingi zake tofauti tofauti zikiwemo: huruma na upendo kwa wanyonge, mpinga dhuluma, mjasiri, mwenye bidii, ubunifu, ujuzi, maarifa na nyenzo bora za kumwezesha kuhimili mikikimikiki ya mfumodume. Kwa picha hii, makala haya yatasaidia kuongeza matini za Kiswahili zilizoshughulikia mchango wa riwaya za kingano katika ukombozi wa mwanamke na mtoto. Vilevile, makala haya yatasaidia kuwaongoza wahakiki na watafiti wanaotarajia kuitalii riwaya ya Marimba ya Majaliwa au kazi nyingine ya kingano ili kumsawiri mwanamke.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Badru, Z. A. (2019). Mfumo Dume – Chanzo cha Ufungwa wa Mwanaume: Uhakiki wa Semi Kutoka Jamii za Kiafrika. Katika JULACE: Journal of University of Namibia Language Centre, Vol. 4 (1).

Bible Society of Tanzania. (1997). Maandiko Matakatifu ya Mungu yaitwayo BIBLIA. Nairobi: Africa Area Typesetting Unit.

Graviningen, K. na wenzake, (2017). Reported Reasons for Breakdown of Marriage and Cohabitation in Britain: Findings from the Third National Survey of Sexual Altitudes and lifestyle (Natsal-3). PLOS ONE 12 (3); eo174129. https;//doi.org/10.1371/journal.pone.0174129.

Hanson, B. J. (2008). Takadini (toleo la pili). Dar es Salaam: Methews Bookstore and Stationers.

Hardiman, R., Jackson, B. W., & Griffin, P. (2010). Conceptual Foundations. Katika B. Adams, Castaneda, Hackman, Peters & Zúnigana wenzake. (Wahariri), Readings for Diversity and Social Justice. New York, NY: Routledge.

Hewitt, N. A. (2010). Introduction. Katika N. A. Hewitt. (Mhariri). No Permanent Waves: Recasting Histories of U.S. Feminism. New Brunswick, NJ: Rutgers University Press.

Hooks, B. (2000). Feminism is for Everybody: Passionate Politics. Cambridge, MA: South End Press.

Hunter, A. G. & Sellers, S. L. (1998). Feminist Attitudes among African American Women and Men. Katika Sage Journals. https://doi.org/10.1177/089124398012001005.

International Organization for Migration. (2019). World Migration Report 2020. https://publications.iom.int/system/files/pdf/wmr_2020.pdf.

Karisa, B. S. & Mwinyifaki, A. (2017). ‘Iktibasi’ katika Tenzi za Mwanakupona na Al-Inkishafi. Katika Kioo cha Lugha, Vol. 11. https://journals.udsm.ac.tz/index.php/kcl/article/view/786

Koda, B. (2000). The Gender Dimension of Land Rights in Tanzania: Case Study of Msindo Village, Same District. PhD Thesis (unpublished). University of Dar es salaam.

Levine, L. (1977). Black Culture and Black Consciousness: Afro - American Folk Thought From Slavery to Freedom. London: Oxford University Press.

Maggie, H. (1996). Feminist Literary Criticism in America and England. Katika Women’s Writing: A Challenge to Theory. Sussex: Harvesters Press.

Masatu, F. na wenzake. (2020). Mwingilianomatini katika Tamthilia ya Utangamano Wetu Ushindi Wetu (2017) ya Anitha E. Mgimba. Katika East African Journal of Swahili Studies 2 (2), 128-143. https://doi.org/10.37284/eajss.2.2.217.

Mbogo, E. (2002). Watoto wa Mama N’tilie. Dar es Salaam: HEKO Publishers.

Mbyana, H. H. (h.m). Ndoa ya Kiislam. https://www.alislam.org/swahili/Ndoa-ya-Kiislamu.pdf.

Mgimba, A. E. (2017). Utangamano Wetu Ushindi Wetu. Dar es Salaam: E & CE Publishers.

Msuya, M. B. (2012). Usawiri wa Mhusika ‘Bibi’ katika Riwaya za Kiswahili: Mfano kutoka Riwaya za Marimba ya Majaliwa na Ngome ya Mianzi. Tasnifu ya Shahada ya Uzamili (haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Muhando, P. (2007). Nguzo Mama. Dar es Salaam: Macmillan Aidan Ltd.

Mulokozi, M. M. (2017). Taaluma ya Lugha na Fasihi - 2: Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili Kozi za Fasihi Vyuoni na Vyuo Vikuu. Dar es salaam: KAUTTU.

Nimavat, S. (2014). Gloria Steinem – A Feminist Activist with a Difference (A Study of Her Major Views). Katika International Journal of Research and Analytical Reviews. http://ijrar.com/upload_issue/ijrar_issue_65.pdf.

p’Bitek, O. (1975). Wimbo wa Lawino: Ombolezo. Dar es Salaam: EAPH.

Pasque, P. A. (2011). Women of Color in Higher Education: Theoritical Perspectives. Katika G. Jean-Marie & B. Llyod-Jones. (Wahariri), Women of Color in Higher Education: Turbulent Past, Promising Future, Vol. 9. Bingley, UK Emerald.

Pearson, R. (2000). Rethinking Gender Matters in Development. Katika Allen, T & Thomas, A. (Wahariri). Poverty and Development into the 21st Century. Oxford: Oxford University Press.

Rutherford, A., Marecek, J. & Sheese, K. (2012). Psychology of Women and Gender. Katika Weiner Vol. 1. https://www. Researchgate.net/publication/312056770.

Semzaba, E. (2008). Marimba ya Majaliwa. Dar es salaam: E&D Vision Publishing.

TUKI. (2005). Kamusi ya Kiswahili Sanifu (toleo la pili). Nairobi: Oxford University Press.

Ward, P. (2001). ‘Women of Britain Say Go’: Women’s Patriotism in the First World War. Katika Twentieth Century British History, Vol. 12 (1). Doi: 10.1093/tcbh/12.1.23

Wazambi, F. & Komanya, J. (2019). Ukatili wa Kingono: Tishio kwa Haki na Ustawi wa Mtoto Nchini Tanzania, Muhtasari wa Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania 2018: Tanzania Bara. Dares salaam: Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu.

Weathers, M. A. (1969/2010). An Argument for Black Women’s Liberation as a Revolutionary Force. http://scriptorium.lib.duke.edu/wlm/fun-games2/argument.html.

Yakubu, A. M. (2014). Women as Their Own Worst Enemies: Rewrting the Stepmother and Mother-in-Law Archetypes in Adimora-Ezeibo’s Roses and Bullets. Katika IOSR Journal of Humanities and Social Sciences, Vol. 19 (1). http://www.iosrjournals.org/iosr-jhss/papers/Vol19-issue1/Version-11/C0191110915.pdf?id=8829.

Tarehe ya Uchapishaji
18 December, 2021
Jinsi ya Kunukuu
Masatu, F., Hyera, V., & Ndunguru, O. (2021). Nafasi ya Riwaya za Kingano za Kiswahili katika Harakati za Kupigania Hadhi-Msingi ya Mwanamke. Mfano Riwaya ya Marimba ya Majaliwa (2008) ya Edwin Semzaba. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 4(1), 68-81. https://doi.org/10.37284/jammk.4.1.512