Mwingilianomatini katika Tamthilia ya Utangamano Wetu Ushindi Wetu (2017) ya Anitha E. Mgimba

  • Furaha J Masatu Mwenge Catholic University
  • Venancia F Hyera Mwenge Catholic University
  • Osmunda R Ndunguru Mwenge Catholic University
  • Aneth K Ponera Mwenge Catholic University
Keywords: Mwingilianomatini, Utangamano Wetu Ushindi Wetu, Anitha E. Mgimba, Majazi, Mwangwi wa Kifalsafa, Anwani za Sura, Mithiolojia ya Ishara
Sambaza Makala:

Ikisiri

Mwingilianomatini ni mbinu, stadi ama taaluma na mwongozo wa uchunguzi wa matini kisayansi, hususani kazi za kisanaa na zisizo za kisanaa ili kubaini kuwepo kwa athari ya uchopekaji ama usemezano; yaani kufanana kifani, kimaudhui na kimbinu kati ya matini moja na nyingine. Ufanano huo huweza kuwa wa moja kwa moja au kuwapo kwa ukaribiano. Mwingiliano huo hutambulika pia kama mwangwi. Inaaminika kwamba, mwingilianomatini ni miongoni mwa mbinu kongwe za kiutunzi, ilhali kiuhakiki inaonekana bado ngeni, haijashughulikiwa sana katika uga wa fasihi na sanaa ya Kiswahili. Kwa mantiki hiyo, makala haya yatasaidia kuongeza maandiko ya Kiswahili yaliyoshughulikia eneo la uhakiki kupitia nadharia ya mwingilianomatini ili kubaini mwingilianomatini uliopo katika matini, kwa mfano tamthilia ya Utangamano Wetu Ushindi Wetu. Matokeo ya uchambuzi yamebaini kuwapo kwa mwingilianomatini mwingi unaofungamana na historia ya makuzi na malezi ya mwandishi kidini (kiroho), kimwili (kiutamaduni na kimaadili), kijamii na kitaaluma – kwa namna moja ama nyingine. Sehemu ya matokeo hayo ndiyo inayobeba makala haya. Hivyo basi, makala yanawasilisha mwingilianomatini kati ya tamthilia teule ya Utangamano Wetu Ushindi Wetu na maandiko kutoka vitabu vitakatifu, majazi katika uteuzi na uumbaji wa wahusika, mwangwi wa kifalsafa, anwani za sura au ploti, na mithiolojia ya kiishara.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Ambrose, B. M. (2014). Kuchunguza Masuala ya Kisiasa katika Riwaya za Shaaban Robert: Mfano wa Kusadikika na Kufikirika. Tasnifu ya Shahada ya Uzamili katika Kiswahili (Haijachapishwa). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Bertoncini, E. Z. (1989). Outline of Swahili literature. Leiden: E. J. Brill.

Bible Society of Tanzania. (1997). Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo BIBLIA. Nairobi: Africa Area Typesetting Unit.

Boaz, B. Z. (1974). Mwanamalundi: Mtu Maarufu katika Historia ya Usukuma. Dar es salaam: Wizara ya Elimu ya Taifa.

Hambly, W. D. (1929). The Serpent in African Belief and Custom. In American Anthropologist, [N. S., 31].

Hellier, A. B. (1964). Nunda Mla Watu na Hadithi Nyingine. London: Sheldon Press.

Hussein, E. N. (1976). Jogoo Kijijini na Ngao ya Jadi. Dar es salaam: Oxford University Press.

Kezilahabi, E. (2006). Gamba la Nyoka. Nairobi: Vide~Muwa Publishers.

Kipacha, A. (2005). Osw 101: Utangulizi wa Lugha na Isimu. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Kristeva, J. (1980). Desire in Langauge: A Semiotic Approach to Literature and Art. New York: Columbia University Press.

Lemaster, T. (2012). What is “Intertextuality”? United States: University of Wisconsin-Madison.

Lynch, P. A. & Roberts, J. (2010). African Mythology A to Z, (second edition). New York: Chelsea House Publishers. https://img.fireden.net/tg/image/1454/78/1454787608049.pdf.

Madumulla, J. S. (2009). Riwaya ya Kiswahili: nadharia, historia na misingi ya uchambuzi. Dar es salaam: Mture Educational Publishers Ltd; Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.

Masatu, F. J. (hakuna mwaka). Shujaa Gishegu na Hadithi Zingine.

Massamba, D. P. B. (2004). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI.

Massamba, D. P. B., Kihore, Y. M., na Hokororo, J. I. (2012). Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA): Sekondari na Vyuo. Dar es Saalam: TUKI.

Mbogo, E. (1988). Ngoma ya Ng’wanamalundi. Dar es salaam: Education Services Centre Ltd.

Mgimba, A. E. (2017). Utangamano Wetu Ushindi Wetu. Dar – es – Salaam: E & CE Publishers.

Mlacha, S. A. K. na Madumulla, J. S. (1991). Riwaya ya Kiswahili. Dar es Saalam: DUP.

Mningo, R. A. (2015). Tathmini ya Mwingilianomatini katika Utunzi wa Emmanuel Mbogo: Utafiti Linganishi wa Tamthiliya ya Ngoma ya Ng’wanamalundi na Fumo Liongo. Tasnifu ya Shahada ya Uzamili katika Kiswahili (Haijachapishwa). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Mswahili, A. A. M. na Njonjolo, M. S. (2016). Nje – Ndani. Dar es salaam: Culture Link Africa Ltd.

Muhando, P. (2007). Nguzo Mama (Toleo la Pili). Dar es Saalam: Macmillan Aidan Ltd.

Robert, S. (1951). Kusadikika. London: Nelson.

Robert, S. (1952). Adili na Nduguze. London: Macmillan.

Robert, S. (1967). Kufikirika. Nairobi: OUP.

Robert, S. (1968). Utubora Mkulima. Nairobi: Nelson.

Saleh, K. K. (2015). Ufasihi Simulizi katika Riwaya za Shaaban Robert: Mifano kutoka Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad. Tasnifu ya Shahada ya Uzamili katika Kiswahili (Haijachapishwa). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Semzaba, E. (1988). Ngoswe Penzi Kitovu Cha Uzembe. Dar es salaam: DUP

Shanafelt, R. (2014). Serpent Beings, Sacrificial Brides, Superboy Saviors: Comperative Analysis of African Serpent Lore. Katika Relegere: Studies in Religion and Reception, Juzuu I, Toleo 2.

Taylor, I na Taylor, M. M. (1983). The Psychology of Reading (toleo la kwanza). Cambridge, Massachusetts: Academic Press.

Thomas, R. (2011). Taswira ya Nyoka katika Kigano za Kisambaa. Tasnifu ya Shahada ya Uzamili katika Kiswahili (Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

TUKI. (2013). Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Toleo la 3). Dar es Salaam, Nairobi: Oxford University Press.

Wafula, R. M. na Njogu, K. (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Wamitila, K. W. (2002). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi: Phoenix Publishers.

Wamitila, K. W. (2003). Influence or Intertextuality? A Comparative Study of Kezilahabi’s Nagona and Mzingile and Juan Rulfo’s Pedro Paramo. Katika Kiswahili (Juzuu. 66). Dar es salaam: TUKI.

Wamitila, K. W. (2003). Kamusi ya Fasihi: istilahi na nadharia. Nairobi: Focus Publications Ltd.

Worton, M. na Still, J. (1990). Intertextuality: Theories and Practice. Manchester: Manchester University Press.

Tarehe ya Uchapishaji
18 September, 2020
Jinsi ya Kunukuu
Masatu, F., Hyera, V., Ndunguru, O., & Ponera, A. (2020). Mwingilianomatini katika Tamthilia ya Utangamano Wetu Ushindi Wetu (2017) ya Anitha E. Mgimba. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 2(2), 128-143. https://doi.org/10.37284/eajss.2.2.217