Mahusiano ya Uwezo katika Muwala wa Mada katika Hotuba Teule za Marais Kikwete na Samia, Kenya

  • Sammy Dimbu Chuo Kikuu cha Chuka
  • John Kobia, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
  • Mary Kanyua, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
Keywords: Diskosi za Kisiasa, Hotuba Teule, Muwala, Mada na Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi
Sambaza Makala:

Ikisiri

Muwala huchukuliwa kuwa kipengele cha diskosi ambacho hufasiriwa kulingana na muktadha na hujumuisha dhana zinazohusiana, utathmini na msemezano. Makala hii iliangazia makala muwala wa mada katika hotuba teule za Marais Jakaya Kikwete (Kikwete) na Samia Suluhu (Samia). Nadharia iliyoongoza makala hii ni Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi. Nadharia hii hudokeza kuwa lugha yenyewe haina mamlaka bali huyapata inapotumiwa na wenye mamlaka katika miundo ya kijamii. Sampuli ya makala hii ilipakuliwa kutoka Kumbukumbu za Kudumu za Mabunge ya Kitaifa nchini Kenya zilizoko mtandaoni. Diskosi za hotuba teule zilizo sampuli ya makala hii ni zile zilizowasilishwa kwa lugha ya Kiswahili baina ya miaka (2013-2022). Kipindi hiki ni awamu ya 11 na 12 ya Bunge la Kitaifa na awamu ya 2 na 3 ya Bunge la Seneti nchini Kenya. Jumla ya hotuba 2 ziliteuliwa kimakusudi kwa kujikita kwenye mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo. Muundo wa kimaelezo ulitumika katika kukusanya, kuchambua na kuwasilisha matokeo ya utafiti. Data ya makala hii ilikusanywa kutokana na mchakato wa usomaji wa kina wa hotuba teule. Data iliainishwa kulingana na maswali ya utafiti. Matokeo yalibainisha kuwa vipengele vya  kigezo cha hali, washiriki katika diskosi, madhumuni ya mawasiliano, kitendo neni kilichotendwa na kaida za mawasiliano yalikuza muwala wa mada katika hotuba teule. Makala hii ilibainisha namna masuala ya kimuktadha huchangia muwala wa ndani na wa kijumla ili kuleta uelewaji wa diskosi ili kukuza mahusiano ya uwezo katika diskosi. Makala hii ilipendekeza tafiti za baadae zifanywe kuhusu namna vibainishi vya muktadha wa diskosi hukuza maana ya implikecha.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Bayley, P. (2004). Cross-cultural Perspectives on Parliamentary Discourse. John Benjamins Publishing Company.

Crombie, M. A. (1985). Rhetoric and Coherence: A Case for a Model of Linguistic Interaction. Croom Helm.

Daneš, F. (Ed.). (1974). Papers on Functional Sentence Perspective. Academia.

Daneš, F, (1995). Paragraph – A Central Unit Of The Thematic And Compositional Build-Up of Texts. In: Warwick, B., Tanskanen, S.K., Hiltunen, R. (eds). Organization in Discourse. Proceedings from the Turku Conference. Turku: University of Turku.

Dimbu, S. L. (2021). Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi katika Vikatuni vya Shujaaz [Master's thesis]. Chuka University Repository. http://repository.chuka.ac.ke/handle/chuka/13938.

Dontcheva-Navratilova, O. (2009). Building up discourse coherence: Creating identities in political speeches.‟ In: Dontcheva-Navratilova, O., Povolná, R. (eds) Coherence and Cohesion in Spoken and Written Discourse. Newcastle upon Tyne: Cambridge Scholars Publishing. 97-119.

Dontcheza-Navratilova, O. (2010). Coherence in Political Speeches: Interpreting Ideational, Interpersonal and Textual Speeches Meaning in Opening Addresses. Masarykova Univerzita Filozoficka Fakulta.

Fairclough, N. (2013). Language and Power. (2nd Ed.). Harlow: Routledge.

Fetzer, A., & Meierkord, C. (Eds.). (2002). Rethinking Sequentiality: Linguistics Meets Conversational Interaction. John Benjamins.

Firbas, J. (1992). Functional Sentence Perspective in Written and Spoken Communication. Cambridge University Press.

Fries, P. H. (1995). Themes, Methods of Development, and Texts. In R. Hasan & P. H. Fries (Eds.), On Subject and Theme: A Discourse Functional Perspective (pp. 317–360). John Benjamins Publishing Company.

Gee, P. J. (2014). An Introduction to Discourse Analysis: Theory and Method, Routledge.

Gernsbacher, M. A. (1997). Coherence Cues Mapping During Comprehension. In J. Costermans & M. Fayol (Eds.), Processing Interclausal Relationships in the Production and Comprehension of Text (pp. 3–21). Lawrence Erlbaum Associates.

Givón, T. (1995). Coherence In Text Vs Coherence In Mind. In: Gernsbacher, M. A., Givón, T. (eds) Coherence in Sponateous Text. Amsterdam, Philadelphia: John Benjamins. 59-116.

Givón, T. (2001). Syntax: An Introduction (Vol. I & II). John Benjamins.

Habwe, H. (1999). Discourse Analysis of Swahili Political Speeches, (Unpublished PhD Thesis). University of Nairobi.

Hunston, S., na Thompson, G. (2000). Evaluation: An introduction. In: Hunston, S., Thompson, G. (eds), Evaluation in Text. Authorial Stance and the Construction of Discourse. Oxford: Oxford University Press. 1-27.

Mcleod, N. J., & Paradis, E. (2024). A Meta-Study Analysing the Discourses of Discourse Analysis in Health Professions Education. Medical Education.

Miššíková, G. (2007). Analysing Translation as Text and Discourse. Praha: JTP.

Sperber, D., & Wilson, D. (2010). A Relevance-Theoretic Approach to the Development of Understanding of Others' Mental States. In E. V. Clark & V. Evans (Eds.), The Oxford Handbook of Cognitive Linguistics (pp. 673-693). Oxford University Press.

van Dijk, T. A., & Kintisch, W. (1983). Stragegies of Discourse Comprehension. Academic Press.

van Dijk, T. A., (1995). Aim of Critical Discourse Analysis, Japanese Discourse Journal, 1(1), pp. 17-28.

van Dijk, T. A., (2001). Critical Discourse Analysis, in: D. Schiffrin, D. Tannen and H.E. Hamilton (eds) Handbook of Discourse Analysis. Oxford Press.

van Dijk, T. A. (2015). Critical Discourse Analysis. In D. Tannen, H. E. Hamilton, & D. Schiffrin (Eds.), The Handbook of Discourse Analysis (2nd ed., pp. 466–485). Wiley-Blackwell.

Tarehe ya Uchapishaji
5 September, 2025
Jinsi ya Kunukuu
Dimbu, S., Kobia, J., & Kanyua, M. (2025). Mahusiano ya Uwezo katika Muwala wa Mada katika Hotuba Teule za Marais Kikwete na Samia, Kenya. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 8(2), 283-294. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3587

Makala zilizo somwa zaidi kama hii.