Uchanganuzi wa Athari ya Mageuzi ya Maneno kwenye Muundo wa Sentensi ya Ekegusii

  • Wilfrida Kemuma Momanyi Author
  • Beverlyne Asiko Ambuyo, PhD Maseno University
  • Rocha Mzungu Chimerah, PhD Pwani University
Sambaza Makala:

Ikisiri

Tasnifu hii inachanganua athari ya mageuzi ya maneno kwenye muundo wa sentensi sahili ya Ekegusii ikiangazia sheria na kanuni zinazotawala mageuzi hayo. Mageuzi ya kisintaksia huleta mabadiliko mengi katika sentensi asili. Utafiti huu ulichunguza na kuchanganua athari ya haya mageuzi kwenye muundo wa sentensi. Utafiti huu vilevile ulishughulikia viambajengo vya sentensi sahili ya Ekegusii kwa kudhihirisha kanuni mahususi zinazotawala muundo wa sentensi hiyo. Misingi ya kinadharia ya utafiti huu ni Sintaksia Finyizi kwa mujibu wa Chomsky. Data ilikusanywa maktabani kupitia kwa vitabu teule vya Ekegusii kwa kutumia kifaa cha kudondoa data. Mbinu ya usampulishaji kwa lengo maalum ilitumiwa ili kupata sentensi zilizodhihirisha mageuzi.  Mbinu za maelezo zilitumika katika kuwasilisha data. Vijenzi vya sentensi sahili ya Ekegusii na dhana ya ugeuzi yanashughulikiwa ambapo majopo leksika na majopo amilifu yamejadiliwa kwa kina. Dhana ya ugeuzi na aina za mageuzi zinazojitokeza katika sentensi sahili ya Ekegusii pia imeshughulikiwa. Matokeo ya utafiti yanadhihirisha kwamba mageuzi yanayofanyiwa muundo wa sentensi hayabadilishi maana ya sentensi asili. Matokeo na mahitimisho ya utafiti wetu yanadhihirisha kwamba, suala muhimu linalojitokeza ni kuwa kanuni geuzi zinasababisha mabadiliko katika muundo wa sentensi ingawa maana ya sentensi hubaki ile ile. Pili ni kuwa mageuzi hayafanyiki kiholela; hufuata utaratibu unaokubalika na kutawaliwa na kanuni mahususi. Mwisho ni kuwa utafiti huu unapendekeza kuwa dhana ya mageuzi ya kisintaksia ishughulikiwe katika lugha nyinginezo kwa kurejelea sentensi ambatano na kwa nadharia nyinginezo za kisasa. Utafiti huu utawafaidi waundaji wa mitaala katika lugha ya Ekegusii. Vile vile, utafiti huu utaweka msingi bora katika eneo la isimu linganishi miongoni mwa watafiti wengine mbali na wale watakaoitafitia mada hii katika lugha nyinginezo. Matokeo ya utafiti huu yatachangia katika kuelewa zaidi ubainishi wa miundo mbalimbali ya sentensi za kibantu na kuwafaidi walimu katika ufunzaji wa sintaksia ya kibantu na hasa katika lugha ya Ekegusii.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.
Tarehe ya Uchapishaji
16 September, 2019
Jinsi ya Kunukuu
Momanyi, W., Ambuyo, B., & Chimerah, R. (2019). Uchanganuzi wa Athari ya Mageuzi ya Maneno kwenye Muundo wa Sentensi ya Ekegusii. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 1(3), 98-109. Retrieved from https://journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/35