Tathmini ya Mbinu za Ufundishaji wa Masuala Mtambuko katika Mtaala wa Umilisi: Mfano wa Shule za Msingi Nchini Kenya

  • Ann Wambui Gitau Chuo Kikuu cha Kibabii
  • Eric W. Wamalwa Chuo Kikuu cha Kibabii
  • Stanley Adika Kevogo Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaramogi Oginga Odinga
Keywords: Ufundishaji wa Masuala Mtambuko, Mtaala wa umilisi, Ujifunzaji
Sambaza Makala:

Ikisiri

Masuala mtambuko ni baadhi ya mambo muhimu yanayofundishwa katika mtaala wa elimu. Taasisi ya Ukuzaji wa Mitaala nchini Kenya imejumuisha na kusisitiza ufundishaji wa masuala mtambuko katika Mtaala wa Umilisi. Isitoshe, masuala mtambuko yanajitokeza kuwa muhimu sana katika Mtaala wa Umilisi wa Kiswahili katika shule za msingi. Hata hivyo, tafiti zimebaini kuwa ufundishaji haujatekelezwa inavyostahili. Makala haya yanatathmini ufundishaji wa masuala mtambuko katika Mtaala wa Umilisi wa Kiswahili wa shule za msingi za kaunti ndogo ya Kimilili. Nadharia ya Utekelezaji wa Uvumbuzi iliyoasisiwa na Gross na wenzie (1971) imetumika. Walimu 38 walishirikishwa katika utafiti. Data ilikusanywa kwa kutumia hojaji na uchunzaji. Matokeo ya utafiti yamebainisha kwamba, walimu walitumia mbinu mbalimbali za ufundishaji kwa viwango tofauti. Asilimia100 ya walimu walitumia mbinu ya maswali na majibu kufundisha masuala mtambuko. Aidha, asilimia 63 walitumia majadiliano; nayo asilimia 49 ya walimu walitumia mbinu ya vikundi vya ushirika  Baadhi ya mbinu zilitumika kwa uchache tu na nyingine hazikutumika kabisa. Licha ya hayo, mbinu zilizotumiwa katika ufundishaji hazikutumiwa kwa ufanisi mkubwa. Aidha matokeo yameonesha kwamba walimu walikumbwa na changamoto katika uteuzi na matumizi ya mbinu mwafaka za ufundishaji wa masuala mtambuko. Kutokana na matokeo haya, inapendekezwa kuwa, warsha za mara kwa mara ziandaliwe kwa walimu walio nyanjani kwa minajili ya kuwanoa na kuwapiga msasa kuhusu utekelezaji wa ufundishaji wa mtaala wa elimu ya umilisi, na matumizi ya vifaa mwafaka vya kufundishia vikiwemo vifaa halisi na vya kielektroniki. Pili, inapendekezwa kuwepo kwa tathmini ya mara kwa mara kuhusu ubora na kiwango cha ufundishaji wa masuala mtambuko na utekelezaji wa mtaala wa umilisi  katika shule za msingi

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Chang'ach, J. K. & Kessio, D. K. . (2012). Education for development: Myth or reality? The Kenyan experience. International Journal of Learning and Development, 2(3), 114-163.

Chang'ach, J. K. & Kessio, D. K. (2012). Education for development: Myth or reality? The Kenyan experience . International Journal of Learning and Development, 2(3), 114-163.

Gross, N. Giacquinta, J. B. & Berstein, M. (1971). Implementing Organizational Innovation: A Sociological Analysis of Planned Educational Change. New York: Basic Books.

Kassem, A. K. (1992). Teacher perceptions of Agricultural teaching practices and methods for youths and adult in Lowa. Lowa: Lowa State University.

KICD. (2017). Lower Primary level curriculum design: Volume 1 Kiswahili, Literacy and Indegenous Languages, English Activities. Nairobi: Author.

KICD. (2019). Lower primary level curriculum design: Volume 1 Kiswahili, Literacy and Indegenous Languages, English Activities. NairobI: Author.

Kumar, R. (2005). Reserch Methodology: A step by Step Guide for Beginners . London: Sage Publcations Limited.

Magare, Y. D. (2011). Matumizi ya majadiliano ya vikundi katika kufunza stadi ya kuzungumza katika shule za upili katika tarafa ya Mosocho, Kaunti ya Kisii, Kenya. Nairobi: Kenyattta University.

Mbae, D. K. (2015). Factors influencing implementation of Kiswahili curriculum in public primary schools in Igoji division, Meru county, Kenya. Masters Thesis, University of Nairobi.

Mwangi, S. M. (2013). Responsiveness of primary teachers education to challenges of the 21 century. Phd thesis, Kenyatta University.

NCPPHE. (2008). Partnerships for public purposes: Engaging higher education in societal challenges of the 21st century. San Jose: National Centre fof Public Policy and Higher Education.

Ndege, J., Kea,P., Osoro, E., Waititu, F., Mucheria, Z. na Wafula, W. (2020). Kiswahili Dadisi: Mwongozo wa Mwalimu Gredi ya 4. Nairobi: Oxford University Press.

Nyokabi, K. J. (2018). Teacher Factors Affecting the Implementation of Early Chilhood Development and Curriculum in Mathira East Sub- County, Nyeri County,Kenya. Kenyatta University. Nairobi: unpubished .

Ondimu, S. M. (2018). Teachers' preparedness for the implementation of the Competece Based Curriculum in private pre-schools in Dagoretti sub-county Nairobi city county . Masters' thesis, University of Nairobi, Nairobi. Imechukuliwa toka http://www.res

Owala, O. R. (2021). Success and challenges of implementation of the Competence-Based Curriculum in Kenya.

Ransaw, T. S., & Majors, R. (Eds.). (2017). Emerging issues and trends in education (International Race and Education Series). Michigan: Michigan State University Press. doi:10.14321/j.ctt1qd8zjk

Schleicher, A. (2018). Educating learners for their future not our past. ECNU Review of Education. 1(1), 58-75. doi:10.30926/ecnuroe2018010104

Sifuna,D, N. & Obonyo, M. M. (2019). Competence Based Curriculum in primary schools in Kenya: Prospect and challenges of implementation . 3 (7), 37-50.

UNESCO. (2000). Education in the situations of emergency and crisis: Challenges for the new century. Paris: Author.

UNICEF. (1999). Education; The state of the Word's children. Thailand: Author.

Wasike, M. W. (2015). Tathmini ya matumizi ya nyimbo za kizazi kipya kama mbinu ya kufundishia masuala ibuka katika Kiswahili kwenye shule za upili nchini Kenya. Kibabii University. Bungoma: Kibabii University.

Tarehe ya Uchapishaji
19 December, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Gitau, A., Wamalwa, E., & Kevogo, S. (2023). Tathmini ya Mbinu za Ufundishaji wa Masuala Mtambuko katika Mtaala wa Umilisi: Mfano wa Shule za Msingi Nchini Kenya. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(2), 73-83. https://doi.org/10.37284/jammk.6.2.1645