Mchango wa Mofofonolojia ya Kiduruma kwa Ujifunzaji wa Sarufi ya Kiswahili

  • Noah Munda Majele Chuo Kikuu cha Kibabii
  • Eric W. Wamalwa Chuo Kikuu cha Kibabii
  • Benson Sululu Simiyu Chuo Kikuu cha Kibabii
Keywords: Mofofonolojia, Kiduruma, Ujifunzaji na Mwingiliano
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yamedadavua mchango wa mofofonolojia ya Kiduruma kwa ujifunzaji wa sarufi ya Kiswahili katika shule za msingi za kaunti ya Kwale nchini Kenya. Nadharia ya Fonolojia Zalishi Asilia iliyoasisiwa na Joan Hooper (1971) iliongoza utafiti. Mkabala wa kithamano na muundo wa kiethinografia ulitumiwa katika uchunguzi. Data ilikusanywa kutokana na insha za wanafunzi kwa kutumia mwongozo wa uchanganuzi wa yaliyomo. Matokeo yalionesha kuwa kuna mwingiliano katika vipengele vya mofofonolojia ya Kiduruma na Kiswahili, hali inayoleta uwezekano wa kuendeleza ujifunzaji wa vipengele vya sarufi ya Kiswahili kwa kutumia mofofonolojia ya Kiduruma. Imebainika kwamba ujifunzaji wa vipengele vya sarufi ya Kiswahili kama vile fonimu, miundo ya silabi, ngeli, nyakati mbalimbali na mnyambuliko wa maneno unaweza kufaidi kutokana na mofofonolojia ya Kiduruma. Kutokana na matokeo hayo, uchunguzi huu unapendekeza kwamba, katika eneo la utafiti ambapo asilimia kubwa ya wanafunzi ni Waduruma, mofofonolojia ya Kiduruma inaweza kutumiwa kama wenzo wa ujifunzaji wa vipengele vya sarufi ya Kiswahili.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Agull, N. (2016). Mifanyiko ya Kimofofonolojia ya Ukuzaji na Udunishaji wa Nomino za Kiwanga Kakamega Kenya. Egerton University: Unpublished Masters Thesis.

Akbari, R. (2007). ‘Reflections on reflection: A critical appraisal of reflective practices in L2 teacher education.’ System 35: 192–207.

Bell, J. (2007). ‘The trouble with questionnaires’, in M. Coleman and A.R.J. Briggs (eds) Research Methods in Educational Leadership and Management, 2nd edn. London: Sage Publications.

Garret, A., & Blevins, J. (2018). Analogical Morphophonology. Journal of African Studies, 18-27.

Griffiths, J. B. (1935). Glimpse of Nyika Tribe:Waduruma. Kwale: Bible Transilation & Literacy.

Hamad, S. (2011). Tense and Aspect Representation in Standard Swahili and Kipemba (Tasnifu ya Uzamili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Haijachapishwa).

Hooper, J. (1971). Introduction to Generative Phonology. New York: Academic Press.

Hooper, J. (1971). Introduction to Generative Phonology. New York: Academic Press.

Khasinah, S. (2014). Factors influencing second language acquisation. Journal of mordern lingistics, 3, 18-27.

Larsen-Freeman, D. & Anderson, M. (2011). Techniques and Princips in Language Teaching. Great Clarendon Street: Oxford University Press.

Manundu, A. K. (2019). Uchanganuzi wa Athari za Kimofofonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kisomali Wanapojifunza Lugha ya Kiswahili. Unpublished Masters Theisi: Pwani University.

Mgullu, R.S (1999). Mtalaa Wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers.

Otiende A. M (2013). Athari Za Kimofofonolojia Za Kiolusuba Katika Matumizi Ya Kiswahili Sanifu Kama Lugha ya Pili. Tasnifu iliyowasilishwa katika Chuo kikuu cha Nairobi.

Rutagwerela, D. (2019). Nadharia ya Fonolojia zalishi: Asili, Malengo na Changamoto zake. Dar es Salaam: TUKI.

Saunders, M., Lewis, P & Thornhill, A. (2009). Resaerch Methods for Business Students. Pretence : Hall Publications .

Sharabil, A. B. (2017). Tofauti za Kimofofonolojia baina ya Kipemba kaskazini na Kipemba cha Kusini. University of Tanzania: Unpublished MA Thesis

Tsangwa, J. K. (2017). Ukopaji Maneno ya Kiswahili Sanifu kutoka Lugha ya Kigiriama: Michakato na Kanuni za Kifonolojia. Pwani University: Unpublished Masters Thesis .

Walsh, M. (1992). People and the Environment in the Western Indian Ocean: Mijikenda Origin. Retrieved from https://www.researchgate.net/publication/284574938.

Wamalwa, E. W., Mohochi, E.S., & Odeo, I.I. (2020). Mielekeo ya Lugha na Ujifunzaji wa Kiswahili katika Shule za Msingi za Kaunti ya Siaya. Jarida la Mwanga wa Lugha, 12-16

Willis, J. (2018). The Mijikenda and Mombasa to C.1930. (PHD thesis: Orental and African studies University of London-Unpublished).

Tarehe ya Uchapishaji
30 May, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Majele, N., Wamalwa, E., & Simiyu, B. (2023). Mchango wa Mofofonolojia ya Kiduruma kwa Ujifunzaji wa Sarufi ya Kiswahili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 165-179. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1227