Majina ya Asili ya Watu Katika Jamii-lugha ya Wagogo

  • Jemima Lenjima Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
  • Julius Edmund Frank, PhD Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Keywords: Jina, Majina ya Asili, Jamii-lugha, Wagogo
Sambaza Makala:

Ikisiri

Miaka ya hivi karibuni majina ya asili katika jamii nyingi za kitanzania yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya kupotea kwa kasi hasa kwa vijana kutokana na ujio wa sayansi na teknolojia pamoja na dini. Makala haya yamekusanya na kubainisha majina ya asili ya watu katika jamii-lugha ya Wagogo. Makala yameongozwa na swali moja katika kuandaliwa kwake. Swali hilo linauliza; Majina yapi ya asili ya watu yanayotumika katika jamii-lugha ya Wagogo? Mbali na kujadili swali hilo muhimu, Makala haya pia yametoa mapendekezo kuhusu njia za kuendeleza matumizi ya majina ya asili ya watu katika jamii-lugha husika. Data za makala zimekusanywa kwa mbinu ya mahojiano na majadiliano ya kundi lengwa na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo na majedwali kwa ufafanuzi zaidi. Uchanganuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Uumbaji ya (Sapir-Whorf, 1958) inayosisitiza kwamba, lugha ndio msingi wa kuuelewa ulimwengu. Unapojifunza lugha hiyo hata dunia unayoiumba akilini mwako itatokana na dunia iliyoratibiwa na wasemaji wake. Matokeo ya uchunguzi wa makala haya yamedhihiridha kuwa, majina ya asili ya watu katika jamii-lugha ya Wagogo yapo katika makundi kulingana na jinsi yanavyotolewa au kupatikana. Makundi yamebainishwa kwa kuzingatia sifa zinazofanana katika makundi mbalimbali

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Anusa, H. J. (2016). Maana za Majina ya Watu Katika Jamii ya Wayao. Tasnifu ya M.A Kiswahili Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Dawling, T. (2004). “Uquidisizwe” The Finisher of Nation, Naming and Taking a bout HIV/AIDS and African Languages. ht tp:/www. African voice.co.za/research. Htm.

Koigi. J. (2008). Literary Scene: What is in name. Daily Nation. Nairobi Medi Group, uk 37.

Gray, T. M. (1999). What’s in a name? Some reflection on the Socialogy Annonymity. http//web.ed/gt marx/a non.html.

Kalkanova, T. (1999). Sociology of Proper Names in Sophia since 1970. International Journal of Sociology of Language, 135, 83-98.

Matsimela, A. M. (1997). Sefulediso. Republic of South Africa: Creda Press.

Mbiti, S. (1990). African Religion and Philosoph. USA: Heinemann Educational Books inc.

Mnyampala, M. E (1954). Historia, Mila na Desturi za Wagogo. Dar es Salaam: East African Literature Bureau.

Musere, J. (2010). African Person Names Derived from African Pro. llE line aArhicle. Com/2expert=Jonathan Musere.

Nyangaywa, M. (2013). Uchunguzi wa Kisemantiki na Taratibu za Utoaji wa Majina ya Kijita. Tasnifu ya M.A Kiswahili (Haijachapishwa). Dar es Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Ota, O. (2002). Edo Person Names and World View. New Perspective in Edoed Studies; Nigeria.

Rey, A. (1995). Essay on Teminology. Amsterdam, John Benjamin Publishing Company.

Rugemalira, J. M. (2005). A Grammer of Runyambo. Dar es Salaam: Language of Tanzania Project. University of Dar es Salaam.

Sapir, E. (1921). Language. New York: Harcourt Brace.

Sapir, E. (1958). Language. New York: Harcourt, Brace & Co.

Tegisi, N. M. (2019). Uchunguzi wa Kisemantiki wa Majina ya Asili Katika Ginantuzu. Tasnifu ya Uzamivu (Haijachapishwa). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Whorf, B. L. (1958). Language Thought and Reatily: Selected Writings. Cambridge, Technology Press of Massachusetts Institute of Technology.

Zacharia, M. (2020). Matumizi ya Majina ya Kiswahili Jijini Dar es Salaam, Nchini Tanzania: Uchunguzi Kifani wa Majina ya Watu: Tasnifu M. A Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Tarehe ya Uchapishaji
28 August, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Lenjima, J., & Frank, J. (2023). Majina ya Asili ya Watu Katika Jamii-lugha ya Wagogo. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 303-318. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1396