Usawiri wa Mabadiliko ya Ujumi Mweusi katika Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1990-2000

  • Elihaki Yonazi Chuo Kikikuu Kishiriki cha AMUCTA
  • Julius Edmund Frank, PhD Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Keywords: Nyimbo, Mabadiliko, Ujumi, Ujumi Mweusi, Unusura, Muziki Wa Dansi Wa Tanzania
Sambaza Makala:

Ikisiri

Kila jamii ina ujumi wake. Ujumi wa Afrika huitwa ujumi mweusi. Ujumi wa jamii huweza kupaka mabadiliko kulingana na mpito wa wakati na mwingiliano wa jamii nyingine. Mabadiliko ya ujumi wa kijamii husawiriwa kwenye kazi za kifasihi za jamii hiyo. Makala haya yamechunguza usawiri wa mabadiliko ya ujumi mweusi kwenye nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania. Data ya maktabani ndiyo iliyotumika. Jumla ya nyimbo 20 za kuanzia mwaka 1990-2000 zilikusanywa, ambapo zimetumika nyimbo 5 tu, zilizoteuliwa kimakusudi, kwa kuangalia dhima kuu, na ya kipekee inayojitokeza zaidi kwenye wimbo husika. Nyimbo hizo ndizo zilizotumika katika mjadala wa makala haya. Nadharia ya Unegritudi na Uhalisia zimetumika katika uchambuzi wa data ya utafiti. Nadharia ya Unegritudi ilituongoza katika kuchambua vipengele vya ujumi mweusi vinavyojitokeza kwenye nyimbo teule. Naharia ya Uhalisia ilituongoza katika kujadili uhalisia wa jamii ya Watanzania na nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania. Aidha, katika kubainisha mabadiliko ya ujumi mweusi, na jinsi mabadilko hayo yanavyosawiriwa kwenye nyimbo teule. Matokeo ya utafiti yanabainisha kuwepo kwa mabadiliko mengi ya ujumi mweusi yaliyosawiriwa na nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania kwa mawanda mapana. Mabadiliko hayo ni kama vile, kukosekana/kupungua kwa; maadili mema, umoja na ushirika, utu; heshima, na adabu na utii. Kutokana hayo, watunzi wa nyimbo hizi wanashauriwa kutunga nyimbo zinazosawiri ujumi mweusi, na kuepuka athari hasi za utamaduni wa nje, ili nyimbo hizo ziweze kukubalika na jamii yote, na kuwa na manufaa endelevu katika jamii yao.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Assen, N. V. (2012). Resonation Muziki wa Dansi in Dar es Salaam, Tanzania. Tasinifu ya Umahiri (Haijachapishwa). African Language and Culture: Leiden University/African Study Centre.

Badru, Z. A. (2015). Taswira na Ubainishaji wa Mabadiliko ya Kiujumi katika Vitendawili vya Kiswahili: Mifano ya Vitendawili vya Kiswahili. Tasinifu ya Shahada ya Uzamivu (Haijachapishwa): Chuo Kikuu cha Dodoma, Dododma.

Berrian, A. H. na Long, R. A. (1967). Negritude: Essay and Studies. Hampton Virginia: Hampton Institute Press,

Bukenya, A. S., Gachanja, M. na Nandwa, J. (1997) Oral Literature; A Senior Course. Nairobi: Longhorn

Damrosch, D. (2003). What is World Literature? Princeton: Princeton University Press,

Hoffman, S. (2002). "Clash of Globalizations," Foreign Affairs. Juz. 81:104-115.

John, B. N. (2018) Uwi ni Sifa ya Ujumi wa Kiafrika? Mifano kutoka Diwani ya Mnyampala, Mashairi ya Saadan na Kivuli cha Mvumo. Mkwawa Journal of Education Development, Juz. 2:20-33.

Kabira, M. W. (1987). Theory of Literature. Black Aesthetics. Nairobi: College of Adult and Distance Learning, University of Nairobi.

King‘ei, K. na Kisovi, C. (2005). Msingi wa Fasihi Simulizi. Nairobi: Kenya Literature Bureau,

Laswai, A. (2015). Ujumi katika Muziki wa Dansi: Nyimbo Teule za Marijani na Ally Choki. Tasinifu ya Shahada ya Umahiri (Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dododma.

Luhwago J. N. (2013). Ujumi katika Fasihi Simulizi: Mifano kutoka katika Hadithi za Wahehe. Shahada ya Umahiri (Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dododma.

Mahenge, E.G. (2021) Matumizi ya Mbinu ya Usimulizi katika Kuibua Dhamira ya Ukombozi wa Kisiasa Kusini mwa Afrika: Uchunguzi wa Nyimbo Teule wa Muziki wa Dansi nchini Tanzania 1940-1990. Mulika , Juz 4 (2): 78-94

Mbawala, A. M. (2011). Mabadiliko ya Ujumi wa Kifasihi Kulingana na Wakati: Mfano wa Nyimbo Teule za John Komba Mwaka 1980-2000. Tasnifu ya Shahada ya Umahiri (Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.

Mbiti, J. S. (2011a). African Religion and Philosophy. Kampala: East African Educational Publisher Ltd.

Mhando, P. na Balisidya, N. (1976). Fasihi na Sanaa za Maonyesho. Dar es Salaam. TPH.

Migodela, W. (2020). Kuchunguza Mtindo katika Nyimbo za Tiba Asili: Mifano kutoka Nyimbo za Waganga wa Mkoa wa Ruvuma. Tasinifu za Uzamivu. (Haijachapishwa). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Dar es Salaam.

Mihale, K. P. (2011). Ujumi katika Ushairi wa Mnyampala. Tasinifu ya Shahada ya Umahiri (Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dododma .

Moore, H. T. (1976). Realism and Naturalism. London: Donald Pizzer

Mulokozi, M. M. (1996). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Mulokozi, M.M. (2017). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili, Kozi za Fasihi Vyuoni na Sekondari. Dar es Salaam: Macony Printing.

Ponera, A. S. (2014). Utangulizi wa Nadharia ya Fasihi Linganishi. Dar es Salaam: Kaarljamer Printing Technology.

Ponera, A. S. (2019). Misingi ya Utafiti wa Kitaamuli na Uandishi wa Tasinifu. Dodoma: Central TanganyikaPress

Renatus, S. (2018). Ujumi wa Kiafrika Katika Tamthiliya ya Kiswahili. Mifano kutoka Kinjekitile na Mashetani. Tasinifu ya M.A (Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.

Russell, K. M. (2012) Introduction to African Art. Austin, TX: St. Andrew‘s Samwel, M., Amina, J.S., na Akech, J.K. (2013). Ushairi wa Kiswahili Nadharia, Maendeleo, Mwongozo kwa Walimu wa Kiswahili na Diwani ya MEA. Dar es Salaam: Mevel Publishers.

Sanga, A. N. (2012). Ujumi katika Riwaya Pendwa ya Kiswahili: Mifano kutoka kwa Mohamed Said Abdulla na Arstablius Elvis Musiba. Tasinifu ya Shahada ya Umahiri: Chuo Kikuu cha Dododma, Dodoma.

Sanga, A. N. (2018). Mkengeuko wa Ujumi wa Kiafrika Katika Hadithi Fupi Andishi za Kiswahili Kipindi cha Utandawazi: Mifano Kutoka Magazeti ya Habari Leo, Nipashe na Mwananchi. Shahada ya Uzamivu (Hijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dododma, Dododma

Sanga, A. N. (2021) Thamani ya Ujumi wa Kiafrika katika Hadithi Fupi Simulizi za Kiswahili: Mulika Na. 40(1): 80-96.

Senkoro, F. E. M. K. (1988). Ushairi: Nadharia na Tahakiki. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press & Amin Education and Research Academy.

Senyamanza, C.R. (hnw) Misingi ya Kazi za Kubuni, Nadharia, Mbinu na Mifano ya Kibunilizi. Dar es Salaam: Karljamer Print Technology.

Snow, C. P. (1968). The Realists: Portraits of Eight Novelists. London: Macmillan.

Wafula, R. M. na Njogu, K. (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation.

Wafula, R. M., na Njogu, K. (2007) Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundtion.

Wamitila, K.W. (2003). Fasihi Simulizi. Nairobi: Muwa Publishers Limited.

Wamitila, K.W. (2004). Kichocheo cha Fasihi Simulizi na Andishi. Nairobi: English Press.

Wamitila, K.W. (2010). Kanzi ya Fasihi: Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi. Nairobi: Vude-Muwa Publishers Limited.

Yonazi, E. (2019). Usanaa wa Lugha katika Ujenzi wa Dhima za Nyimbo za Harusi za Waasu. Tasinifu ya M.A Kiswahili (Haijachapishwa). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dar es Salaam..

Zirimu, P. (1973). Black Aesthetics: Papers from a Colloquium Held at the University of Nairobi, June 1971, Nairobi.

Tarehe ya Uchapishaji
28 June, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Yonazi, E., & Frank, J. (2023). Usawiri wa Mabadiliko ya Ujumi Mweusi katika Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1990-2000. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 194-208. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1255