Maumbo na Maana za Majina ya Asili ya Watu Katika Jamii-lugha ya Wagogo

  • Jemima Lenjima Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
  • Julius Edmund Frank, PhD Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Keywords: Jina, Jamii-lugha, Maumbo ya Majina, Maana, Majina ya Asili
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yamechunguza maumbo na maana za majina ya asili ya watu katika jamii-lugha ya Wagogo kwa kuchanganua vijenzi mbalimbali vinavyojenga majina hayo. Data iliyochunguzwa ni sehemu ya data iliyokusanywa kutoka katika wilaya ya Mpwapwa na Chamwino, mkoani Dodoma kwa ajili ya tasnifu ya Uzamivu. Uchanganuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Mofolojia Leksika kwa mujibu wa Kiparsky (1982) inayosisitiza kuwa vipashio vinavyounda maneno vimepangwa kidarajia kimsonge ambapo vipashio vidogo huungana ili kuunda vipashio vikubwa. Data za makala haya zimewasilishwa  kwa majedwali. Hata hivyo, baadhi ya data zimewasilishwa kwa kutumia michoroti ili kudadavua vyema mpangilio wa vipashio vinavyounda majina husika na kuonesha jinsi vipashio hivyo vilivyopangwa kidarajia kimsonge. Matokeo ya uchanganuzi huo yamedhihirisha kuwa majina ya asili ya watu yaliyochunguzwa yameundwa kwa vijenzi mbalimbali ambavyo vimechanganuliwa kimofolojia na kuleta maana. Tofauti na baadhi ya wanaisimu wanaodai kuwa majina ya watu yameundwa na mzizi au mashina tu, makala haya yamedhihirisha kuwa vipo vipashio maalumu vinayounda majina ya asili ya watu na vinaweza kuchanganuliwa kimofolojia

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abdul, A. (2013). Maana na Sababu za Kiisimujamii Kwenye Majina ya Koo za Kiluguru. Tasnifu ya M.A Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Agard, F.B. (1984). A Course in Romance Linguistics: A Synchronic View. USA: Georgetown University Press.

Allen, G. V. (1978). Using the Written Language Creatively. The Ohio State University, Marion.

Anusa, C. A. (2016). Maana za Majina ya Watu Katika Jamii ya Wayao. Tasnifu ya M.A Kiswahili, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Aronoff, M. & Fudeman, K. (2011.) What is morphology? (2nd ed.). USA: Wiley- Blackwell.

Azael, R. (2013). Maana za Majina ya Asili Katika Jamii ya Kiuru (Tasnifu ya M.A Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam).

Baitan, B. (2010). Morphosemantic Analysis of Ruhaya Person Names (M.A Dessertation University of Dar-es-salaam, Tanzania).

Buberwa, A. (2017). Ruwaza za Kimofolojia za Majina ya Mahali ya Kihaya: Mtazamo wa Mofolojia Leksika. Tasnifu ya shahada ya Uzamivu. Dar -es-Salaam, Chuo Kikuu cha Dar -es- Salaam.

Davis, E. M. (2016). Majina ya Asili ya Vitongoji Yanayoitambulisha Jamii ya Wajita. Tasnifu ya M.A Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Gichuru, T.M. (2010). Uchunguzi wa Nomino ambatani za Kiswahili: Mtazamo wa Mofolojia Leksia. Tasnifu ya shahada ya uzamili Chuo Kikuu Cha Kenyatta, Nairobi, ir -library.

Habwe, J., & Karanja, P. (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers.

Kiparsky, P. (1982). Lexical phonology and Morphology. Encyclopedia of Language and Linguistics, 94-97. https//doi.org/10.1016/bo-08-044854-2/0008.

Manyasa, J. (2010). Investigating the Basis of Naming People in Kisukuma. M.A. Dessertation, University of Dar-es-Salaam, Tanzania.

Mascaro, J. (1979). Catalan Phonology and Phonological Cycle. PhD Dissertation, M.I.T. Reproduced by the Indiana University Linguistics Club.

Mcmahon, A. (2000). Lexical Phonology and History of English. Cambridge: Cambridge University Press.

Msanjila & Wenzake, (2009). Isimu Jamii Sekondari na Vyuo. TUKI. Dar es Salaam.

Nyangawa, M. (2013). Uchunguzi wa Kisemantiki na Taratibu za Utoaji wa Mjina ya Kijita. Tasnifu ya M.A Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Pesetsky, D. (1976). “Russian Morphology and Lexical Theory”. Ms. M.I.T.

Resani, M. (2014). Semantiki na Pragmatiki ya Kiswahili, Dar. Karljamer Print Technology.

Rubach, J. (1981). Syclic and Lexical Phonology: The Structure of Polish. USA: Foris Publications.

Rugemalira, J.M (2005). A Grammar of Runyambo, Dar -es- Salaam: Language of Tanzania Project, University of Dar es Salaam.

Salapion, D. (2011). Haja ya Kuunda Kamusi ya Majina ya Watu ya Asili: Majina ya Asili katika Jamii ya Wahaya. Tasnifu ya M.A. Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam.

Siegel, D. (1974). Topics in English Morphology, PhD. Dissertation, M.I.T. Siegel, D. (1977). “The Adjacency Condition and the Theory o f Morphology”. In Proceedings of the Eighth Annual Meeting of the North East Linguistic Society, Amherst, Mass.

Tegisi, N. M (2019). Uchunguzi wa Kisemantiki wa Majina ya Asili Katika Koo za Ginantuzu. Tasnifu ya shahada ya Uzamivu. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

TUKI, (2004). Kamusi ya Isimu na Lugha. Dar es Salaam. Education Publishers and Distributors.

Zubeir, S. Z. (2015). Etimolojia ya Majina ya Mahali ya Kaskazini Pemba kwa Utambulisho wa Utamaduni wa Wapemba. Tasnifu M.A Kiswahili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Tarehe ya Uchapishaji
28 June, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Lenjima, J., & Frank, J. (2023). Maumbo na Maana za Majina ya Asili ya Watu Katika Jamii-lugha ya Wagogo. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 209-232. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1271