Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000

  • Elihaki Yonazi Chuo Kikikuu Kishiriki cha AMUCTA
Keywords: Nyimbo, Ujumi, Ujumi Mweusi, Unusura, Muziki Wa Dansi Wa Tanzania
Sambaza Makala:

Ikisiri

Nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zilianza nchini Tanzania kipindi cha ukoloni. Nyimbo hizi zinasawiri ujumi mweusi kwa kiasi kikubwa, na zina unusura. Ujumi wa kijamii huwa na dhima muhimu katika kazi za kifasihi za jamii husika. Kila jamii ina ujumi wake. Ujumi wa Waafrika huitwa ujumi mweusi. Huu ni ujumi utokanao na utamaduni wa jamii ya Kiafrika pamoja na mazingira yake. Ujumi huu huweza kutumika kuhakikia kazi za kifasihi za Kiafrika. Makala hii imetumia data za maktabani. Jumla ya nyimbo 8 za kuanzia mwaka 1970-2000 zimetumika. Nyimbo hizo zimeteuliwa kimakusudi, kwa kutumia usampulishaji usonasibu. Uteuzi huo umefanywa kwa zingatia dhima kuu, na ya kipekee, inayojitokeza zaidi kwenye wimbo husika. Mbinu zilizotumika kukusanyia data ni; utazamaji makini, udurusu wa matini na mbinu ya kutalii na kukusanya. Data zimechambuliwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli, na nadharia ya Uhalisia imetumika katika uchambuzi wa data ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti wa makala hii yanabainisha kwamba ujumi mweusi una mchango mkubwa katika unusura wa nyimbo teule. Unusura huo umebainika kusababishwa na usawiri, kwa mawanda mapana vipengele mbalimbali vya ujumi mweusi kwenye nyimbo teule. Vipengele hivyo ni; umoja na ushirika, adabu na utii, utu, na matumizi bora ya lugha ya Kiswahili. Hivyo, walengwa wake huvutika kuzisikiliza kwani hugusa mambo yanayojenga ustawi wa jamii yao, hivyo kuwa na unusura. Hivyo, wasanii wanashauriwa kuendelea kutunga nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zenye usawiri wa ujumi mweusi kwa mawanda mapana. Hali hii itasaidia kuendeleza unusura wa nyimbo hizi, kwa ajii ya usatawi wa jamii ya Watanzania na jamii nyinginezo

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abdulhamid, M. & Baruwa, A. (2006). Methali za Kiswahili: Maana na Matumizi. Dar es Salaam: Mkuki na Nyota Publishers.

Askew, K. (2002). Performing the Nation: Swahili Music and Cultural Politics in Tanzania (Vol. 2). University of Chicago Press.

Assen, N.V. (2012). Resonation Muziki wa Dansi in Dar es Salaam Tanzania. Tasinifu ya Umahiri (Haijachapishwa). African Language and Culture. Leiden Universitry /Africa Studie Centre.

Badru, Z. A. (2015). Taswira na Ubainishaji wa Mabadiliko ya Kiujumi katika Vitendawili vyaKiswahili: Mfano wa Vitendawili vya Kiswahili. Tasinifu ya Shahada ya Uzamivu Chuo Kikuu cha Dodoma (Haijachapishwa)

Bukenya, A., Nandwa, J., & Gachanja, M. (1997). Oral Literature, a Senior Course. Nairobi: Longhorn Publishers.

Faustine, S. (2020). Uafrikanishaji katika Riwaya ya Kiswahili. Mulika Journal, 38(1).

Jilala, H. (2016). Misingi ya Fasihi Linganishi, Nadharia, Mbinu na Matumizi. Daud Publishing Company, Dar es Salaam

John, B.N. (2018) Uwi ni Sifa ya Ujumi wa Kiafrika? Mifano kutoka Diwani ya Mnyampala, Mashairi ya Saadan na Kivuli cha Mvumo. Mkwawa Journal of Education and Development, 2, 20-33.

Laswai, A. (2015). Ujumi katika Muziki wa Dansi: Nyimbo Teule za Marijani na Ally Choki. Tasnifu ya Shahada ya Umahiri Chuo Kikuu cha Dodoma, (Haijachapishwa).

Luhwago J. N. (2013). Ujumi katika Fasihi Simulizi: Mfano kutoka katika Hadithi za Wahehe. Shahada ya Umahiri katika Fasihi ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dodoma.

King‘ei, K., & C. Kisovi. (2005). Misingi ya Fasihi Simulizi. Kenya Literature Bureau, Nairobi

Mahenge, E. (2021). Matumizi ya Mbinu ya Usimulizi katika Kuibua Dhamira ya Ukombozi wa Kisiasa Kusini mwa Afrika: Uchunguzi wa Nyimbo Teule za Muziki wa Dansi nchini Tanzania 1940-1990. Mulika Journal, 40(2).

Mbiti, J.S (2011a). African Religion and Philosophy. Kampala: East Africa Education Publishers Ltd

Mihale, K. P. (2011). Ujumi katika Ushairi wa Mnyampala. Tasnifu ya Shahada ya Umahiri Chuo Kikuu cha Dodoma, (Haijachapishwa).

Moore, H. T. (1976). Realism and Naturalism. London: Donald Pizzer

Mulokozi, M.M. (2017). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili, Kozi za Fasihi Vyuoni na Sekondari. Macony Printing, Dar es Salaam.

Ngatungwa, F.J. (2020). Usawiri wa Falsafa ya Kiafrika katika Semi: Mifano kutoka Vitendawili vya Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dodoma Tasinifu ya Umahiri (Haijachapishwa)

Ponera, A.S(2014). Utangulizi wa Nadharia ya Fasihi Linganishi. Kaarljamer Printing Technology, Dar es Salaam

Renatus, R. (2018). Ujumi wa Kiafrika Katika Tamthiya ya Kiswahili. Mfano kutoka Kinjekitile na Mashetani. Tasinifu ya M.A (Haijachapishwa), Chuo Kikuu cha Dododma. Dodoma

Russell, K. M. (2012). Introduction to African Art. Austin, TX: St. Andrew’s

Sanga, A. N. (2022). Thamani ya Ujumi wa Kiafrika katika Hadithi Fupi Simulizi za Kiswahili. Mulika Journal, 40(1).

Samwel, M., Amina, J.S., na Akech, J.K. (2013) Ushairi wa Kiswahili Nadharia, Maendeleo, Mwongozo kwa Walimu wa Kiswahili na Diwani ya MEA. Dar es Salaam: Mevel Publishers (MVT)

Sanga, A. N. (2012). Ujumi katika Riwaya Pendwa ya Kiswahili: Mifano kutoka kwa Mohamed Said Abdulla na Arstablius Elvis Musiba. Tasinifu ya Shahada ya Umahiri Chuo Kikuu chaDodoma, (Haijachapishwa).

Sanga, A.N. (2018). Mkengeuko wa Ujumi wa Kiafrika Katika Hadithi Fupi Andishi za Kiswahili Kipindi cha Utandawazi : Mifano kutoka Magazeti ya Habari Leo, Nipashe Na Mwananchi. Phd Thesis (Haijachapishwa), Chuo Kikuu cha Dododma.

Senkoro, F. E. (1988). Ushairi: Nadharia na Tahakiki. Dar es Salaam University Press.

Senyamanza, C. R.(hnm). Misingi ya Kazi za Kubuni, Nadharia, Mbinu na Mifano ya Kibunilizi. Dar es Salaam: Karlijamer Print Technology.

Snow, C. P. (1968). The Realists: Portraits of Eight Novelists. Macmillan: London.Wafula, R. M., &Njogu, K. (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. The Jomo Kenyatta Foundation, Nairobi.

Wamitila, K.W(2002). Fasihi Simulizi. Muwa Publishers Limited, Nairobi.

Wamitila, K.W. (2003). Fasihi Simulizi. Muwa Publishers Limited, Nairobi.

Yonazi, E. (2019). Usanaa wa Lugha katika Ujenzi wa Dhima za Nyimbo za Harusi za Waasu. Tasinifu ya M.A Kiswahili (Haijachapishwa), Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Zirimu, P. (1973). Black Aesthetics: Papers from a Colloquium Held at the University of Nairobi, June 1971. East African Literature Bureau, Nairobi.

Tarehe ya Uchapishaji
28 August, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Yonazi, E. (2023). Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 289-302. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1395