Dhima ya Matambiko katika Jamii ya Waturkana

  • Hosea Lorot Gogong Chuo Kikuu cha Laikipia
Keywords: Aina ya Matambiko, Wahusika na Vifaa, Dhima ya Tambiko
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inabainisha kuwa jamii ya Waturkana hutekeleza matambiko aina tofauti tofauti. Aidha, matambiko hayo huwa na dhima kubwa katika jamii hiyo. Stadi hii ilichochewa na haja ya kupigania nafasi stahili ya fasihi ya Mwafrika hususan nafasi ya matambiko katika tamaduni ya Waafrika. Makala hii itabaini na kuthibitisha kuwa, Matambiko yana nafasi muhimu sana katika fasihi ya jamii ya Waturkana. Pia, utafiti huu utathibitisha ufasihi wa matambiko. Nadharia za uhalisiajabu zilimwongoza mtafiti kuchunguza suala la matambiko katika jamii ya Waturkana. Pia, nadharia ya utendaji ilimsaidia mtafiti kuchunguza suala la utendaji wakati wa kutambika. Utafiti huu ulichukua muundo wa kimaelezo. Data kuhusu aina za matambiko na dhima yake ilikusanywa kutoka maktabani na nyanjani. Ili kuafikia lengo kuu, mbinu mbalimbali za ukusanyaji data zilitumika ambazo ni mahojiano, usikilizaji, utazamaji na unukuzi daftarini. Sampuli ziliteuliwa kimaksudi, mtafiti alitumia mtindo wa sampuli azimiwa katika kuwateua wazee ishirini na saba (27), wazee wa kiume kumi na nane (18) na wa kike tisa (9)  kutoka katika vijiji tisa ambazo ni Kaenyumae, Moru-lingakirion, Nagetei, Loreng, Nareng-munyen, Nakimak, Edos, Kapoong, na Kadokochini. Wazee wa kiume wawili na wa kike mmoja waliteuliwa kutoka katika kila Kijiji. Vijiji hivi vinapatikana kwenye kata ndogo ya Locher-emoit iliyoko kwenye kata ya Lochwaa-Ngikamatak, eneo la Kaunti ndogo ya Turkana Kusini kwenye Kaunti ya Turkana. Idadi kubwa ya wakazi wa Kaunti ya Turkana ni Waturkana. Isitoshe, umri wa wazee walioteuliwa ulikuwa kuanzia miaka hamsini na tano kwenda mbele. Kigezo cha umri kilitumika kwa sababu inaaminika kuwa wazee wa umri huo ndio wana tajriba katika mchakato mzima wa utekelezaji wa matambiko. Kwa mujibu wa Ramsay (2005), data zilizokusanywa kutokana na mahojiano zilichanganuliwa kwa kuzingatia uchanganuzi wa kithamano. Aidha, data za utafiti huu ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo ya utafiti huu ni kuwa jamii ya Waturkana hutambika na huwa na matambiko ya aina tofauti tofauti. Isitoshe, utafiti huu umesaidia kukusanya data kuhusu matambiko na kuzihifadhi katika maandishi, kwani mambo mengi ya Fasihi Simulizi ya jamii ya Waturkana bado yamehifadhiwa vichwani mwa watu kama sehemu ya kutunzia kumbukumbu.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Alembi, E. (2002). “The Construction of the Abanyole Perceptions on Death through Oral Funeral Poetry.” Tasnifu ya uzamifu, Chuo kikuu cha Helsinki.

Ampim, M. (2003). Africa studies. Five major African initiation rites. https://www.manuampim.com/AfricanInitiationRites.htm

Barrett, A. J. (1998). Sacrifice and prophecy in Turkana cosmology. Paulines Publications Africa.

Bauman, R. (1975). Verbal Art as Perfomance. New Jersey: Blackwell Publishing.

Ejeem. C. (2021, December 10). Turkana Women Rite Of Passage(Akinyonyo). Turkana Diary. https://turkanadiary.com/turkana-woman-rite-of-passageakinyonyo/

Foley, M. (1995). Singer of Tales in Performance Voices in performance and text. Bloomingon: Indiana University Press.

Haen, D. (2005). Magic realism and Postmodernism: Decentering Privileged Centers. Zamora Lois Parkison & Wendy Faris (Eds.) Magic Realism: Theory, History, Community. Durham & London: Duke University Press. pp. 191-208.

Hymes. D. (1974). Foundations in sociolinguistics. An ethnographic approach. Philadelphia. University of Pennsylavia Press.

Oxford University Press. (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu . Oxford University Press. Kenya. Kirama, Kh. (1953) Habari za Wakilindi, Vuga Press.

Kitula, K. & Catherine, N.M.K (2010) Misingi ya Fasihi SimuliziKenya litearure Bereau.

Korobe, B. (2021). The Southern Limits of the Turkana: Ethno-Cultural History, Origin, Migration, and Settlement of three Pastoral Neighbors - the Turkana, Pokot, and Samburu 1700 – 2020. Journal of African Interdisciplinary Studies, 5(5), 35 – 63

Korobe, B. L. (2021). Turkana Kinship System and Social Structure: an Analysis of the Family, Patrilineage, Patriclan, and Phratric Organization. Journal of African Interdisciplinary Studies, 5(10), 99-136.

Lihraw, D. (2010). The Tachoni Peoples: History, Culture and Economy. Entrepreneurship Development Institute (EDS), Nairobi

Louis, Z. (1995). Magical Realism: Theory, History, Community. Duke University Press.

M’Ngaruthi, N. (2008). Fasihi Simulizi na Utamaduni: Kitabu cha Walimu na Wanafunzi (Shule na Vyuo). The Jomo Kenyatta Foundation, Nairobi.

Masebo . A. (2007) Nadharia ya Fasihi Kidato cha Tano na Sita, Nyambari Nyangwine publishers.

Matti, M. (1993). “Sanaa za maonyesho za Kiafrika za jadi: Mfano wa Tohara ya Watharaka” Tasnifu ya uzamili ambayo haijachapishwa. Chuo Kikuu Cha Moi.

Mbatiah, S. (2002). Hatua za maendeleo ya uhakiki wa fasihi ya kiswahili nchini Kenya a publication of the National Kswahili association; Akimeru fork tell. Chuo Kikuu cha Nairobi

Mtega, W. (2021) Ufasihi wa matambiko: Uchunguzi wa matambiko ya Wapangwa: Kioo cha lugha. Jarida la taasisi ya Taaluma za Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mulokozi, M. (2002). The African Epic Contoversy: Historic, Philosophical and Aesthetic Perspectives on Epic Poetry and Performance. Dar es Salaam: Mkuki na Nyota Publishers

Mwiza, P. (2014). Umuhimu wa Fasihi Simulizi katika jamii. Kutoka petermwiza Blogspot.com na Mwaka wa Kogwa. Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Njogu, K. na Wafula, R. M. (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Okpewho, I. (1992). African Oral Literature: Backgrounds, Character, and Continuity. Bloomington: Indiana University Press.

Ramsay, H. (2005, Winter). Preserving the Haida Language. Canadian Teacher Magazine. Retrieved October 1, 2010, from http://www.canadianteachermagazine.com/ctm_first_nations_education/winter05_preserving_haida_language.shtml

Roh, F. (1925). Nach-Expressionismus: Magischer Realismus: Probleme der neuesten europäischen Malerei. Klinkhardt & Biermann.

Samuel, D. (2019). Appreciating Asapan- Turkana initiation ceremonies. St John College at the University of oxford in Uk.

Samwel, M. (2013). Tamthiliya ya Kiswahili: Kutoka Miviga ya Kidini Hadi Filamu. Dar es Salaam: MEVELI Book Publishers.

Samwel, M. (2015). Umahiri katika Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam: MEVELI Book Publishers.

Schechner, R. (2013). (3rd ed). Performance Studies: An Introduction. NewYork: Routledge.

Wamitila, K. (2002). Uhakiki wa Fasihi na Vipengele vyake. Nairobi, Kenya: Phoenix publishers Ltd.

Wanjala, W. (2015). Mwingiliano tanzu katika Fasihi Simulizi ya Kiafrika: Mfano wa Embalu na Mwaka Kongwa. Tasnifu ya uzamifu (Haijachapishwa), Chuo Kikuu cha Kenyatta Nairobi.

Zamora, Lois Parkinson. (1995). Magical Romance/Magical Realism: Ghosts in U.S. and Latin American Fiction. In Lois Parkinson Zamora and Wendy B. Faris (Eds.), Magical Realism: Theory, History, Community (pp. 497–550). Durham: Duke University Press.

Tarehe ya Uchapishaji
5 December, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Gogong, H. (2022). Dhima ya Matambiko katika Jamii ya Waturkana. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(2), 85-99. https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.992