Wingilugha na Maendeleo Endelevu katika Kaunti Nchini Kenya: Hali Halisi katika Kaunti ya Machako

  • Peter Willington Kilonzo Chuo Kikuu cha Marafiki cha Kaimosi
  • Nabeta Sangili, PhD Chuo Kikuu cha Marafiki cha Kaimosi
Keywords: Wingilugha, Maendeleo Endelevu, Kaunti, Mtagusano
Sambaza Makala:

Ikisiri

Ulimwenguni kote, lugha imekuwa na bado inaendelea kuwa raslimali muhimu katika maendeleo ya sehemu yoyote ile. Kwa watu wengine, lugha ni mtaji katika shughuli zozote za kimaendeleo kwa sababu bila lugha inayoeleweka na washiriki husika hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana na iwapo yatafanyika, kasi yake itakuwa ya chini sana. Katiba ya 2010 ilifanya mabadiliko mengi na mojawapo ni kukifanya Kiswahili kuwa lugha rasmi sawa na Kiingereza. Katiba hii pia ilitengeneza serikali 47 za magatuzi ambazo zina upekee wake wa utamaduni, lugha ikiwa sehemu muhimu ya utamaduni wa Kaunti hizi. Hivyo, angalau kila Kaunti ina lugha tatu zinazozungumzwa humo. Zaidi ya lugha husika tatu, shughuli tofauti zimechangia watu wa jamii mbalimbali kuhamia na kutagusana katika Kaunti tofauti na za kwao, jambo linalosababisha wingilugha dhahiri katika Kaunti zote nchini Kenya. Katika hali hii, swali kuu linakuwa ni: je, lugha ikiwa ni raslimali na mtaji muhimu katika maendeleo, wingilugha unaweza kutumika vipi katika muktadha wa Kaunti ili kuhakikisha maendeleo endelevu? Swali hili linakuwa msingi mkuu wa makala haya kuangazia jinsi wingilugha (Kiswahili, Kiingereza, Lugha asili, na lugha nyinginezo) unavyoweza kutumika katika muktadha wa Kaunti nchini Kenya ili kuhakikisha maendeleo endelevu katika kila Kaunti. Utafiti umejikita katika Kaunti ya Machakos.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Chhaya, K. S. (2017). 'Economic development and language: A journey through India'. SSRN Electronic Journal. https://doi.org/10.2139/ssrn.3053765

Crystal, D. (2010) The Cambridge Encyclopedia of Language. Cambridge: Cambridge University Press.

Jain, T. (2011). Common tongue: The impact of language on economic performance. SSRN Electronic Journal. https://doi.org/10.2139/ssrn.1947148

Kanana, F. E. (2013). Examining African Languages as Tools for National Development: The Case of Kiswahili. The Journal of Pan African Studies, 6(6), 41-68.

Kawonga, G. A. (2019). Nafasi ya Kiswahili katika mandhari-lugha: Uchambuzi kifani wa mabango ya matangazo ya makampuni ya mawasiliano ya simu. Apache Tomcat/8.5.60. https://ir.mu.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/3779

Mkwinda-Nyasulu, B. (2013). Role of language in socio–economic development: the semiotics are right. Journal of Humanities, 23, 213-230. https://www.ajol.info/index.php/jh/article/view/151922/141518

Pendakur, K., & Pendakur, R. (2015). Speak and Ye Shall Receive: Language Knowledge as Human Capital. In Economic Approaches to Language and Bilingualism. New Canadian Perspectives (1st ed., pp. 89-120). EDRS.

Saidi, M. V. (2021). Kiswahili na Maendeleo Mashambani nchini Kenya. Jarida la CHAKITA, 1(1), 19-26.

Sridhar, K. K. (2006). Societal Multilingualism. In Sociolinguistics and Language Teaching (11th ed., pp. 47-70). Cambridge University Press.

Walsh, J. (2006). Language and socio-economic development. Towards a Theoretical Framework, 30(2), 127-148. https://doi.org/10.1075/lplp.30.2.03wal

Tarehe ya Uchapishaji
4 December, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Kilonzo, P., & Sangili, N. (2022). Wingilugha na Maendeleo Endelevu katika Kaunti Nchini Kenya: Hali Halisi katika Kaunti ya Machako. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(2), 78-84. https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.991