Je, Kuna Matapo katika Fasihi Simulizi?

  • Kibigo Mary Lukamika, PhD Chuo Kikuu cha Tom Mboya
Keywords: Matapo, Fasihi Simulizi, Usasa, Usasaleo, Ukale, Ujadi, Kiethnografia
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inahusu matapo na namna yanavyojitokeza katika fasihi simulizi. Fasihi ni sanaa inayotumia lugha na vitendo kuwasilisha ujumbe kuhusu maisha ya binadamu. Fasihi simulizi ndiyo fasihi mama na iliyo na historia ndefu. Hata hivyo, wataalamu wengi wamekuwa wakishughulikia dhana ya matapo katika fasihi andishi bila kuzingatia uwepo wa matapo katika fasihi simulizi ya Kiswahili. Makala inalenga kuyaweka wazi matapo ya fasihi simulizi ya Kiswahili ili kubaini mchango wake katika Sanaa. Vilevile, Makala yanalenga kutathmini matapo hayo kwa kutumia mifano kutoka katika mazingira halisi ya jamii. Utafiti ulifanywa kwa kutumia mbinu ya kiethonografia iliyohusisha kushiriki, kushuhudia na kuhoji pamoja na udurusu wa nyaraka zilitumika katika kukusanya nyimbo na vipengele mbalimbali vya fasihi simulizi katika kila tapo au kipindi. Nadharia ya Ujumi wa Kinudhuma na ile ya Wigo au Uigaji (Ethnopoetics and Emic Theory) ndizo zilizotumika katika kufanikisha utafiti huu. Uchanganuzi wa data na matokeo ulifanywa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli. Makala hii imedhihirisha kuwa matapo yaliyopo katika fasihi andishi; Usasa na Usasaleo, ndiyo hujulikana kama Ukale na Ujadi katika fasihi simulizi ya Kiswahili. Aidha, makala imependekeza kufanyika kwa tafiti nyingine mbalimbali katika fasihi simulizi

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abrams, M. H. A. (1993). Glossary of Literary Terms. New York: Holt, Reinehart and Winston.

Balisdya, N. (1991). Shida. Nairobi. Foundation Books.

Finnegan, R. (1970). Oral Literature in Africa. Nairobi: Oxford University Press.

Finnegan, R. (2012). Oral literature in Africa. UK: Open Book Publishers CIC Limited. http://www..open book publishers. com

Foley, J. M. (1995). The Singer of Tales in Performance. Bloomington and Indianapolis.

Harvilahti, L. (2001) Subtrates and Registers: Trends in Ethnocultural Research, katika Wolf Knuts, U. na A. Kaivola-Bregenhoj. (Wah). Pathways: Uk 18-27 Turku)

Jamii ya Biblia ya Kenya na Tanzania (1997). Biblia, Maandiko Matakatifu ya Mungu. The Bible Societies of Kenya & Tanzania. Nairobi & Dodoma.

Kamusi ya Karne ya 21 (2014). Kamusi ya Kiswahili yenye uketo zaidi katika karne hii. Nairobi: Longhorn Publishers (K) Ltd.

Kahigi, K. & M. Mulokozi (1979). Kunga za Ushairi na Diwani Yetu. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House.

Kirumbi, P. S. (1975). Misingi ya Fasihi Simulizi. Nairobi: Shungwaya.

Matei, A. K. (2011). Fani ya Fasihi Simulizi kwa shule za upili. Nairobi: Oxford University Press

M’Ngaruthi, T. K. (2008). Fasihi Simulizi na Utamaduni: Kitabu cha Walimu na Wanafunzi (Shule na vyuo). Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Mrikaria, S. (2007). Fasihi Simulizi na Teknolojia Mpya. Swahili Forum 14: 197-2006.

Msokile, M. (1992). Misingi ya Hadithi Fupi. Dar es Salaam: Dar es Salaam Printing Press.

Njogu, K., Momanyi, C., na Mathooko, M. (wah.) (2006). Fasihi Simulizi ya Kiswahili. Nairobi: Twaweza Communication.

Ntarangwi, M. (2004). The Challenges of Education and Development in Post Colonial Kenya. Africa Development.

Okpewho, I. (1979). The Epic in Africa. Towards a Poetics of the Oral Performance. New York: Columbia University Press. http://www.jstor.org/discover/10.2307/3818229/iud 3/7/2017

Wamitila, K. W. (2006). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele vyake. Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.

Wamitila, K. W. (2003). Kichocheo cha Fasihi Simulizi na Andishi. Nairobi: Focus Publishers.

Wanjala, S. F. (2011). Kitovu cha Fasihi Simulizi: Kwa Shule, Vyuo na Ndaki. Mwanza: Serengeti Educational Publishers.

Wanjala, S. F, (2015). Mwingilianotanzu katika Fasihi Simulizi ya Kiafrika: Mfano wa Embalu na Mwaka Kogwa. Tasnifu ya Uzamifu. Nairobi: Ndaki ya Kenyatta.

Wanjala, S. F. (2020). Safina ya Utafiti wa Fasihi Simulizi. Kakamega: Elgon Epitome Publishers Ltd.

Tarehe ya Uchapishaji
9 November, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Lukamika, K. (2022). Je, Kuna Matapo katika Fasihi Simulizi?. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(2), 58-68. https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.948