Nafasi ya Muktadha katika Utendaji wa Mivigha ya Olubeko Miongoni mwa Abanyala wa Kakamega, Kenya

  • Benard Waswa Chuo Kikuu cha Egerton
  • Furaha Chai, PhD Chuo Kikuu cha Pwani
  • Aswani Buliba, PhD Chuo Kikuu cha Laikipia
Keywords: Fanani, Mivigha, Muktadha, Tambiko, Utendaji
Sambaza Makala:

Ikisiri

Mivigha mara nyingi huangaziwa kwa mtazamo wa kidini au swala la imani. Mtazamo huu umejengwa kwa imani kwamba binadamu hutamani bila kifani kuhusiana na wahenga wake, Mungu wake, na mwishowe nguvu zaidi zilizoko juu yake. Matambiko katika jamii ya Kiafrika ni mengi. Kuna matambiko ya kuzaliwa, matambiko ya kupeana majina, matambiko ya tohara, matambiko ya harusi, matambiko ya kifo, matambiko ya kidini, na matambiko ya kisiasa miongoni mwa mengine katika jamii pana za Kiafrika. Olubeko ni tambiko la kifo linalofanyika siku tatu baada ya mazishi ya mwanamume mwenye umri au mwenye hadhi ya kutambuliwa miongoni mwa Abanyala wa Kakamega.  Mivigha hii huhusisha utendaji mbalimbali. Mojawapo ya utendaji unaohusishwa katika tambiko hili ni nyimbo. Kazi hii inapambanua nafasi ya muktadha katika uteuzi na uwasilishaji wa nyimbo husika kwa kuzingatia miktadha mahususi ya utendaji wa mivigha ya Olubeko miongoni mwa Abanyala wa Kakamega. Nadharia ya utendaji ndio kurunzi ya kazi hii. Nadharia hii inasisitiza kuwa kupitia utendaji, ujumbe huwafikia watu wengi. Matokeo yanaonyesha kuwa kuna miktadha tano mahususi katika mivigha ya Olubeko: omusee (baraza), khusirindwa (kaburi), olukendo (safari) na hango  (nyumbani). Kutokana na miktadha hii fanani aliweza kuteua na kuwasilisha nyimbo faafu za kila hatua ya mivigha hii. Muktadha ndio uliongoza fanani katika uteuzi wa wimbo husika

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abdulla, M. (2016). Athari za Itikadi Katika NYimbo za Harusi za Zanzibar. Chuo Kikuu cha Huria cha Tanzania: Tasnifu ya Uzamili, haijachapishwa.

Alembi, E. (1993). Aspect of Theatre in Pre-Colonial Kenya. Nairobi: French Cultural Centre.

Alembi, E. (1995). Narrative Performance in a changing world: The case of storytellers in Kenya. . 11th Conference of the International Society for Folk Narrative Research. Mysore: International Society for Folk Narrative Research.

Alembi, E. (2002). The Constructions of the Abanyole Perceptions on Death Through Oral Funeral Poetry. Helsinki University: Unpublished PhD Thesis.

Bacon, W. (1984). The Art of Intrepretation: Perfomance of and Literature. Sage: The Sage Handbook of Perfomance Studies.

Duraku, A. (1997). A handbook on Drama and Theater. Oweri: Colon Concept Ltd.

Finnegan, R. (1970). Oral Literature in Africa. Oxford: Clarendon Press.

Layiwola, D. (2010). A Place where Three Roads Meet: Literature, Culture and Society. Nigeria: Ibadan University Press.

Mulokozi, M. (2002). The African Epic Controversy: Historical, Philosophical and Aesthetic Perspective on Poetry and Performance. Dar es Salaam: Mkuki wa Nyota.

Odhiambo, C. & Kweya, D. (2008). Male Corpsing as Perfomance of Masculinity among Abanyole of Western Kenya. Egerton Journal, VII(2), 2-4.

Osogo, J. (1966). A Hisotry of the Baluyia. Nairobi: Oxford University Press.

Ronzani, R. (2007). Christian Initiation: Baptism and Confirmation. Nairobi: Paulines Publication Africa.

Sanka, G. (2010). The Sisaala Dirge: A Critical Analysis . Kwame Nkurummah University: Unpublished PhD Thesis.

Schechner, R. (1985). Between Theatre and Anthropology. Philadelphia: University of Pennsylvania Press.

Schechner, R. (2013). Perfomance Studies: An Introduction (Tol. la 3rd.). Philadelphia: University of Pennsylvania Press.

Sperber, D. & Wilson, D. (1995). Relevance: Communication and Cognition. Oxford: Blackwell.

Turner, V. (1982). From Ritual to Theatre: The HUman Seriousness of the Play. New York: Perfoming Arts Journal.

Wagner, G. (1954). The Abaluyia of Kavirondo, Kenya. London: Blackwell.

Wanjala, F. (2015). Mwingiliano Tanzu Katika Fasihi Simulizi ya Kiafrika: mfano wa Embalu na Mwaka kogwa. Chuo Kikuu cha Kenyatta: Tasnifu Haijachapishwa.

Wasambo, W. (2014). A Traditional Ritual Ceremony as Edurama: A Case Study of Imbalu Ritual among the Bukusu of Western Kenya. Kenyatta University: Unpublished PhD Thesis.

Were, G. (1967a). A History of the Abaluhyia of Western Kenya. Nairobi: Oxford University Press.

Were, G. (1967b). Western Kenya Historical Texts. Nairobi: Oxford University Press.

Tarehe ya Uchapishaji
21 October, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Waswa, B., Chai, F., & Buliba, A. (2022). Nafasi ya Muktadha katika Utendaji wa Mivigha ya Olubeko Miongoni mwa Abanyala wa Kakamega, Kenya. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(2), 29-39. https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.898