Uamilifu wa Kipragmatiki wa Kirai Nomino (KN) Katika Kiswahili

  • Chege Joel Ngari Chuo Kikuu Cha Kenyatta
Keywords: Kishazi, Muundo, Muktadha, Kirai, Kiima, Ufasili, Pragmatiki
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yalitalii uamilifu wa kipragmatiki wa kirai nomino katika sintaksia ya Kiswahili. Pragmatiki hujihusisha na namna watu wanavyotumia lugha katika muktadha na hali halisi ya mawasiliano. Hivyo basi, pragmatiki ni taaluma inayochunguza maana kulingana na muktadha fulani. Miongoni mwa maana za kimuktadha zilizoshughulikiwa ni pamoja na: maana dhanishi, maana tagusanishi na maana matinishi. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni Sarufi Amilifu Mfumo (SAM) iliyopendekezwa na Halliday. Umuhimu wake ni kwamba inaeleza jinsi lugha inavyotumika katika hali halisi ya mawasiliano. Mbinu za utafiti zilizoongoza utafiti huu ni mahojiano na uchunzaji. Mbinu ya uchunzaji ilitumika ambapo maongezi ya wazungumzaji yalirekodiwa. Mbinu hizi zilikamilishana na kujengana kila mojawazo ikisawazisha mapungufu ya nyingine. Data ya maktabani ilitumika kuweka misingi ya ukusanyaji wa data ya nyanjani ambayo ilikusanywa kwa maswali ya mahojiano. Data katika makala haya ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya majedwali na maelezo. Walengwa wa utafiti huu walikuwa ni: wahadhiri na walimu, vijana waliomaliza shule ya upili na vyuo na wanafunzi wa shule za upili na vyuo. Makala haya yaliweka bayana namna kirai nomino kinavyoweza kutumika kufumba ujumbe kipragmatiki katika mawasiliano. Makala haya yanatoa nafasi ya kupigiwa mfano ya kuchangia katika taaluma ya pragmatiki na isimu kwa jumla.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Beck, I. L., McKeown, M. G., & Kucan, L. (2013). Bringing words to life: Robust vocabulary instruction. Guilford Press.

Corder, J. W., Perrin, G. P., & Smith, G. H. (1968). A Handbook of Current English. 3rd ed. Illinois, Scott, Foresman & Company.

Crystal, D. (1985). A Dictionary of Linguistic and Phonetics. Oxford: Basil Blackwell Limited.

Dale, D. J., & Pearson, P. D. (1978). Teaching Reading Vocabulary. New York, Holt, Richard & Winston.

Dooley, D. (1984). Social Research Methods. New Jersey: Prentice Hall inc.

Eggins, S. (2004). An introduction to systemic functional linguistics (2nd ed.). London: Bloomsbury Academic.

Ellis, R. (1992). Learning to communicate in the classroom: A study of two language learners’ requests. Studies in Second Language Acquisition, 14, 1-23.

Finch, G. (2000). Linguistic Terms and Concepts. New York. Palgrave Macmillan.

Habwe, J. na Karanja, P. (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers.

Halliday, M. & Matthiessen, C. (1997). Construing experience through meaning: alanguage-based approach to cognition. Berlin and New York, Walter de Gruyter.

Halliday, M., & Matthiessen, C. (2004). An Introduction to Functional Grammar (2nd ed.). London: Arnold.

Halliday, M. A. K. (1985). An introduction to functional grammar, London: Edward Arnold.

Kothari, C.R. (2009). Research Methodology. Methods and Techniques (Toleo la pili), New Delhi; New Age International (P) Limited Publishers.

Matthiessen, C., & Halliday, M. (1997). Systemic functional grammar (1st ed.).

Mbaabu, I. (1985). Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Kenya Publishing and Book Marketing Co. Ltd.

Radford, A. (1997). Transformational Grammar. Great Britain: Cambridge University Press.

Richards, J., C. Platt, J., & Weber, H. (1985). Longman Dictionary of Applied Linguistics. London: Longman.

Sperber, D., & Wilson, D. (1986). Relevance, Communication and Cognition. Oxford: Blackwell.

Thomas, J. (1995). Meaning in Interaction. Edinburg: Pearson Education.

Tomlinson & Ellis, R. (1992). Learning to communicate in the classroom: A study of two language learners’ requests. Studies in Second Language Acquisition, 14, 1-23

Ullman, S. (1970). Semantics: An Introduction to the Science of Meaning. Oxford: Basil Blackwell.

Yule, G. (1996). Pragmatics. New York: Oxford University Press.

Tarehe ya Uchapishaji
29 Septemba, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Ngari, C. (2022). Uamilifu wa Kipragmatiki wa Kirai Nomino (KN) Katika Kiswahili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 330-340. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.853