Tathmini ya Uamilifu wa Kiswahili Nchini Uganda: Mintarafu, Ueneaji wa Matumizi Yake Kwenye Asasi ya Uchapishaji

  • Abdu Salim Rais Chuo Kikuu Cha Kenyatta
  • Jacktone Onyango, PhD Chuo Kikuu Cha Kenyatta
  • Ireri Mbaabu, PhD Chuo Kikuu Cha Kenyatta
Keywords: Uamilifu, Uchapishaji, Ueneaji
Sambaza Makala:

Ikisiri

Kwa muda mrefu, Kiswahili kilifundishwa nchini Uganda kama taaluma ya Kigeni, licha ya kuwa lugha rasmi ya pili, baada ya Kiingereza (GoU, 1995). Hata hivyo, Kiswahili kina dhima kubwa katika asasi za muziki, ulinzi na elimu ambako Uamilifu wake unadhihirishwa na ueneaji wa matumizi yake (Mbaabu, 1991na Mlacha, 1995). Ingawa Kiswahili kilienea nchini Uganda, kabla ya kufikia mwishoni mwa wakati wa kukamilisha utafiti huu, viwango vya Uamilifu wake vilikuwa havijatathminiwa kitaaluma kupitia asasi ya uchapishaji. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa, kutathmini Uamilifu wa Kiswahili kutokana na ueneaji wa matumizi yake kupitia asasi ya Uchapishaji. Uamilifu wa Kiswahili ulichunguzwa kwa kutumia Nadharia ya Uamilifu iliyoasisiwa na Wanasosholojia Auguste Comte (1787-1857), Herbert Spencer (1830-1903), Vilfredo (1848-1917) na Emile Durkheim (1857-1917) na kuendelezwa na Mesthrie na wenzake (2004). Nadharia ya Uamilifu iliangazia jukumu lililotekelezwa na fani katika jamii mahsusi(Mesthrie et al., 2004).Kiini cha Uamilifu ni uwezekano wa kuweko kwa fani yenye vijisehemu mahsusi ambapo kila kijisehemu huchangia maendeleo kwa kutekeleza jukumu mahsusi katika fani hiyo (Mesthrie et al., 2004).  Nadharia hiyo ilisaidia kutathmini dhima ya ueneaji wa matumizi ya Kiswahili kupitia Asasi ya Uchapishaji nchini Uganda. Istilahi Ueneaji hutokana na kitenzi enea chenye maana ya kuwa kila mahali. Kuenea katika muktadha huo, kulimaanisha kusambaa kwa matumizi ya Kiswahili nchini Uganda kwa kupitia asasi ya uchapishaji. Ueneaji ni hali ambapo fani fulani husambaa ijapokuwa muundo huweza kubadilika kulingana na mazingira. Wataalamu wa Ueneaji walishikilia kwamba, fani huweza kupenya kuta za kikabila na kuzagaa zaidi kutoka jamii zilizoendelea, kuelekea zisizoendelea (Buliba et al., 2014). Ithibati ni kwamba, fani za lugha za Watawala Wakoloni zinapatikana kwa wingi miongoni mwa Waafrika waliotawaliwa, na kinyume chake kikiwa sivyo (Buliba et al., 2014). Upeo wa utafiti huu ulikuwa Uchapishaji baina ya mwaka 2011 na 2018. Uchapishaji ni utoaji wa vitabu na kuvitawanya kwa kuviuzia watu (Bakita et al., 2012). Kihistoria, uchapishaji ulianzishwa nchini Uganda mnamo mwaka 1879 na Mmishonari Alexander Mackay wa ‘Church Missionary Society’ kwa madhumuni ya kufundisha Ukristo (Mbaabu, 1996). Kwa njia hiyo, uchapishaji wa kamusi na vitabu vya tafsiri za Biblia ulianzishwa kwa ajili ya kutaka kukidhi ufundishaji wake (Mbaabu, 2007). Ueneaji wa matumizi ya Kiswahili ulikadiriwa kutokana na ongezeko la Watumiaji wake nchini Uganda. Kwani ongezeko lilikomaa kiasi cha kuvuka mipaka ya awali (Myelimu, 2015). Taratibu za kithamano na kiwingi idadi zilitumika kwa kuzingatia mkabala wa pembe tatu kukusanya, kuchanganua na kuwasilisha data, iliyotokana na nyaraka za Wachapishaji pamoja na maoni ya Wahojiwa nyanjani. Data ilielezwa kwa kutumia asilimia za maratokezi za maoni ya Wahojiwa. Sampuli ya Wahojiwa wa hojaji ilitokana na Wadau wa Kiswahili wasiozidi 100 jijini Kampala. Sampuli hiyo ilibainishwa kupitia kwa kigezo cha Krejcie na Morgan, 1970, (Amin, 2005) kwa kutumia orodha ya Walimu kutokana na jukwaa la Chakitau. Sampuli ya wahojiwa wa ana kwa ana ambao ni Wataalamu na Wakuu wa mawanda iliteuliwa kimaksudi kupitia mbinu ya sampuli mkufu. Matokeo yataongeza maarifa mapya, kupanua upeo wa tafiti za baadaye, kuchangia swala la uteuzi lugha ya taifa na kupima dhima ya Kiswahili nchini Uganda.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Amin, E. M. (2005). Social Science Research conception: Methodology and Analysis. Makerere University Printery Kampala.

Bakita, Emac, & Kicd. (2012). Kamusi ya Karne ya 21 (Toleo jipya). Longhorn. https://kamusi-ya-karne-ya-21.soft112.com/modal-download.html

Buliba, A., Kimani, N., & Mwihaki, A. (2010). Isimu Jamii kwa Wanafunzi wa Kiswahili. Jomo Kenyatta Foundation, Nairobi.

Buliba, A., Mayaka, G., & Matinde, R. (2014). Misingi ya Nadharia na Mbinu za Utafiti. Serengeti Educational Publishers (Tanzania) Ltd Dar esalam.

Crystal, D. (1997). The Cambridge Encyclopedia of Language (2nd ed.). Cambridge University Press New York.

GoU. (1995). The Constitution of the Republic of Uganda, 1995. Uganda Government, c, 1–7. https://doi.org/10.1017/CBO9781107415324.004

Gustro. (2021). Gustro Kiswahili Books. Gusro ltd. https://www.google.com/search?q=gustro+ltd+kiswahili+books&bih=657&biw=1280&rlz

Habwe, J., Matei, Assumpta, K., & Nyonje, J. (2010). Darubini ya Isimujamii kwa shule na vyuo. Phoenix Publishers, Nairobi.

Jjingo, Caesar & Visser, M. (2018). School-Based Kiswahili Teaching Syllabi for Primary Schools in Uganda. Journal of Language Learning, 34(2), 84–96. http://perlinguam.journals.ac.za

Kenya Publishers. (2019). The Publishers Association of Kenya. Nairobi International Virtual Bookfair.

Kobia, J. (2021). Matatizo Yanayowakumba Waandishi wa Vitabu vya Kiswahili Nchini Kenya. Nordic Journal of African Studies 15(2): 143–153 (2006). http://www.njas.helsinki.fi/pdf-files/vol15num2/kobia.pdf

Mallya, J. (2018). Uandishi na Matatizo ya Uchapishaji. Mwalimu Wa Kiswahili. https://mwalimuwakiswahili.co.tz/uandishi-na-matatizo-ya-uchapishaji-tanzania/

Massamba, D, P, B., Kihore, Y. M., & Msanjila, Y. P. (2004). Fonolojia ya Kiswahili sanifu (FOKISA) : sekondari na vyuo. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mbaabu, I. (1978). Kiswahili : lugha ya taifa. Kenya Literature Bureau, Nairobi;1988.

Mbaabu, I. (1991). The impact of language policy on the development of Kiswahili in Kenya, 1930-1990. (Book, 1992) [WorldCat.org]. In Ann Arbor : University Microfilms International, 1991, ©1992.Howard University. https://www.worldcat.org/title/impact-of-language-policy-on-the-development-of-kiswahili-in-kenya-1930-1990/oclc/271449294

Mbaabu, I. (1996). Language Policy in East Africa : a dependency theory perspective (1st ed.). Educational Research and Publications, Nairobi.

Mbaabu, I. (2007). Historia ya usanifishaji wa Kiswahili. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Meaca. (2015). The National Policy on EAC Integration: Embrace Your Opportunity. Ministry of East African Community Affairs. February.

Mesthrie, R., Swann, J., Deumert, A., & Leap, William, L. (2004). Introducing Socialinguistics (SECOND EDI). Edinburgh University Press. www.euppublishing.com

Mglsd. (2006). Uganda National Culture Policy. Social Development, December, 1–32.

Mlacha, S. A. K. (1995). Kiswahili katika kanda ya Afrika mashariki : (historia, matumizi na sera). Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Msanjila, Y. P., Kihore, Y. M., & Massamba, D. P. B. (2009). Isimujamii : sekondari na vyuo. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Msokile, M. (1992). Historia na matumizi ya Kiswahili. Educational Publishers and Distributors.

Mulokozi, M. M. (2000). Language, literature and the forging of a pan-African identity. Kiswahili, 63, 71–80.

Myelimu. (2015). Nadharia ya Ukuaji na Ueneaji wa Lugha. Forums in “GENERAL STUDENTS DISCUSSIONS.” https://myelimu.com/thread-nadharia-ya-ukuaji-na-ueneaji-wa-lugha

Nyachae, Michiri, J., Mwangi, I., & Mbatiah, M. (2014). Dhima na Majukumu ya Asasi mbali mbali katika Ukuzaji Kiswahili. Focus Nairobi.

O’Grady, W., Dobrovolsky, M., & Katamba, F. (1997). Contemporary linguistics : an introduction (Adapted ed.). Longman.

Tanzania Publishers. (2021). Tanzania Publishing House. Tanzania Publishers. Tanzanian Publishers: List of publishers in Tanzania …https://www.publishersglobal.com

TKB. (2021). Tanzania Kiswahili Books. Googlesearch. https://www.google.com/search?sa=X&rlz=1C1VASI_enUG555UG580&source=univ&tbm=isch&q=tanzania+kiswahili+books&ved

UNCDC. (2021). Kiswahili Books (p. 3). Uganda National Curriculum Development Center. https://www.facebook.com/NCDCUg/posts/a-level-set-books-for-kiswahili-2019-2024the-first-examinations-will-be-sat-in-2/2491078610911267/

Tarehe ya Uchapishaji
22 Aprili, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Rais, A., Onyango, J., & Mbaabu, I. (2022). Tathmini ya Uamilifu wa Kiswahili Nchini Uganda: Mintarafu, Ueneaji wa Matumizi Yake Kwenye Asasi ya Uchapishaji. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 73-83. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.641