Mchango wa Kiswahili katika Mofofonolojia ya Nominomkopo za Lubukusu

  • Tom Juma James Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Jacktone Onyango, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Mofofonolojia, Lubukusu, Mlingano Chanzi, Usimilisho, Lugha Chanzi, Lugha Pokezi, Ukopaji
Sambaza Makala:

Ikisiri

Ukopaji wa leksimu baina ya lugha tofauti ni jambo ambalo haliwezi kuepukika. Kwa hivyo, makala haya yamechunguza jinsi lugha ya Kiswahili imechangia katika upanuzi wa Lubukusu kimofofonolojia kupitia ukopaji wa nomino. Hali hii ilisababishwa na dhana kwamba Kiswahili kimeathiri Lubukusu kiisimu kupitia vipengele kama vile fonolojia, mofolojia na sintaksia. Hata hivyo,makala haya yamejikita tu katika viwango viwili vya kiisimu; fonolojia na mofolojia. Malengo matatu yalishughulikiwa katika makala haya ambayo ni: kubainisha mabadiliko ya kifonolojia yaliyojitokeza katika nominomkopo kutoka Kiswahili hadi Lubukusu, kutambulisha mabadiliko ya kimofolojia yaliyojitokeza katika nominomkopo kutoka Kiswahili hadi Lubukusu na kuchunguza ulinganifu wa kifonolojia na kimofolojia uliopo baina ya nominomkopo za Lubukusu na leksimu changizi za Kiswahili. Hatua zote za makala haya zilitimizwa kupitia mihimili ya nadharia ya Mlingano Chanzi, modeli ya kiutohozi iliyoasisiwa na Smith (2009) na ni maendelezo ya Nadharia Upeo (OptimalityTheory) iliyopendekezwa na Prince na Smolensky (1993). Data ilikusanywa kutoka maktabani na nyanjani. Data ya maktabani ilipatikana kupitia udurusu wa vitabu, tasnifu, majarida na makala ya mtandaoni. Nyanjani, sampuli iliteuliwa kimaksudi kupitia mahojiano kwa walengwa 24 wa jamiilugha ya Babukusu kutoka Kaunti Ndogo ya Kiminini, Kauntiya Trans-Nzoia. Mahojiano yalihusu habari za kibinafsi na maswali teule kutoka kwa vikoa 12 vya kisemantiki. Uchanganuzi wa nominomkopo zilizokusanywa kutoka nyanjani ulidhihirisha kwamba kuna mfanano wa kimaumbo kati ya nomino hizo zikiwa katika mazingiraya Kiswahili na hata zinapohamishiwa katika mazingira ya Lubukusu. Uchunguzi wa matokeo ulionyesha kwamba nominokopwa za Lubukusu kutoka Kiswahili hupitia mabadiliko ya kifonolojia, kimofolojia na mabadiliko hayo yaliongozwa na sheria za kimofofonolojia zilizorahisisha usimilisho wa nomino hizo kopwa katika sarufi ya Lubukusu.

 

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Adicka, O.P. (2016). Utohozi wa Maneno-Mkopo katika lugha ya Kijaluo kutoka Kiswahili. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi.

Batibo, H. M. (2017). Evolutionof Tone in Bantu Languages. LiBRI. Linguistic and Literary Broad Research and Innovation, 6(2), pp. 34-40.

Bwayo, J. (2011).Open Source Spell Checker for Bukusu Dialect. Msc thesis. The University of Nairobi.

Cherotich, K.P. (2017). Fonolojia Arudhi ya nominomkopo kutoka Kiswahili hadi Kikeiyo.Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi.

Clements, G. N., & Goldsmith, J. A. (1984). Auto-segmental Studies in Bantu Tone. Dordrecht: Foris Publications.

Downing, L.J. (2019). Tumbuka prosody: Between tone and stress. In Emily Clem, Peter Jenks & Hannah Sande (eds.), Theory and description in African Linguistics: Selected papers from the 47thAnnual Conference on African Linguistics, 75–94. Berlin: Language Science Press.

Garoma, E. T. (2012). Phonology of Yem: Phonological processes. Journal of Language & Culture, 3(6), pp. 117-125

Gesare, E. M. (2020). A Morphophonological Analysis of Ekegusii Borrowed Segments. Ph.D dissertation. Kenyatta University.

Habwe, J.H., &Karanja, P. (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers.

Hyman, L.M. (2017). Bantu Tone Overview.University of California, Berkeley.

Ingonga, L. 1. (1991). A comparative study of Ekegusii, Lulogooli and Lwitakho. MA thesis. Kenyatta University.

Iribemwangi, P. I, Mbatiah, M. na Michira, N. (2013). Ukuzaji wa Kiswahili: Dhima na Majukumu ya Asasi Mbalimbali. Nairobi: Focus.

Iribemwangi, P. I., & Karuru, D. W. (2012). Phonological Adaptation of Kiswahili Loanwords in Gĩ-Gĩchũgũ Dialect of Gĩkũyũ Language. Baraton Interdisciplinary Research Journal (BIRJ) ,2 (2), 49-62.

Kandagor, M. & Sawe, S. (2014). Resyllabification of Loan Words in Kalenjin Phonology. Researchon Humanities and Social Sciences , 4(6).

Karuru, W. (2013). Borrowing and Communication in Language. International Journal of Education and Research, 1(9).

Kisseberth, C. W. & Odden, D. (2003). Tone. In Derek Nurse & Ǵrard Philippson (eds.), The Bantu languages, 1stedn, 59-70. London: Routledge.

Lewis, M., Charles, D.F., Simons, & Paul, G. F. (2016). Ethnoloque: languages of the world (19thed). Dallas: SIL International.

Lwangale, D.W. (2018). Genealogical Reconstruction of the Proto-luhyia language. Ph.D Dissertation. Egerton University.

Majariwa, D. (2021). “Ukubalifu wa Silabi Funge katika Fonolojia ya Kiswahili.” Mwanga wa Lugha, 6(2) kur. 113-128.

Mallya, J.G. (2018). Phonological Processes in Chagga Nativized Lexemes Borrowed from Standard Swahili. M.A Thesis. Sanata Dharma University.

Marlo, M. R., & Kristopher J. E. (2015) Bukusutonology.MidPhon 20.Indiana University.

Mashauri, M. A. (2021). Upitiaji Upya wa Michakato ya Kifonolojia na Kanuni zake katika Kiswahili Sanifu. Jarida la Taasisi ya Taaluma za Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.19(1). 23-39.

Massamba, D.P. (2009). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.

Massamba, D.P.B (2011). Maendeleo katika Nadharia ya Fonolojia .Dar es Salaam: TATAKI

Mberia, K. (2004). The Phonology of Borrowed Words in Kitharaka. Occasional Papers in Language and Linguistics, 2, 45-57.

Mesthrie, R., Leap, W. L., Deumert, A., & Swann, J. (2000). Introducing Sociolinguistics. Edinburgh: Edinburgh University Press.

Mgullu, R. S. (1999). Mtaala wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers.

Mndeme, A. S. (2019). Phonological Processes of Shambaa. M.Athesis. St. Augustine University of Tanzania.

Morara, A. G. (2016). Syllabic Nativization of Ekegusii Loanwords From English: An Optimality Theory Approach. Elixir International Journal. Literature 101 (2016) 44094 -44099.

Morara, A. G. (2017). Phonological and Morphological Nativization of Ekegusii borrowed nouns from English. Ph.D Dissertation. Kisii University.

Msanjila, Y. P., Kihore, Y. M. na Massamba, D. P. B (2007). Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA). Chuo Kikuu cha Dar es Salaam: TUKI.

Msigwa, A. G., & Vavayo, A. S. (2020). Dosari za Kifonolojia zinazojidhihirisha kwa Wajifunzaji wa Kiswahili katika Jamii ya Wamaasai. Jarida la Chalufakita, Juz. Na. 2.

Muambu, W. E. (2014). Morphophonological changesof Lubukusu borrowed words from English. International Journal of English and Literature, 5(2), 45-51.

Muandike, M. F. (2011). Cultural and Linguistic Borrowing of nouns from English to Lubukusu. M.A Thesis. Kenyatta University.

Muhammad, J.Y. (2017). A Morphophonological Analysis of Nouns Borrowed from Arabic in Hausa and Kiswahili. M.AThesis. Kenyatta University.

Mukulo, K.L. (2016). Phonological Analysis of Lukabarasi Loanwords from English. M.A Thesis. Moi University.

Muriira, K. (2017). A Morphonological analysis of Loanwordsin Kitigania from English. M.A Thesis. Kenyatta University.

Mutonyi, N. (1986). A Morphological Study of the Affixation Process of Lubukusu. M. A Thesis. University of Nairobi.

Mutonyi, N. (2000). Bukusu morphology and phonology. Ph.D Dissertation. Ohio State University.

Mutua, N.B. (2013). The analysis of Kikamba Nativized Loanwords. M.A Thesis. Kenyatta University.

Mwaliwa, H. C. (2014). “An analysis of the syllable structure of standard Kiswahili loanwords from Modern Standard Arabic”. Ph.D.dissertation. The University of Nairobi.

Mwita, L.C. (2009). “The Adaptationof Kiswahili Loanwords from Arabic: A Constraint based Analysis”. Journal of Pan-African Studies, 2: 46-61.

Nandelenga, H. S. (2013). Constraint Interaction in the syllabic phonology of Lubukusu. Ph.D dissertation. Kenyatta University.

Nasambu, M.M. (2017). Lexical Variation in Lubukusu Spoken in Bungoma County. M.A Thesis. Kenyatta University.

Ndalila, H. K. (2014). Language Education as A Catalyst in Documenting Local Languages: a case of the lubukusu noun phrase. URI: http://ir.mu.ac.ke: 8080/xmlui/handle/ 123456789 /1913

Nganga, W.S. (2008). The tone structure of Lubukusu verbs and nouns. M.A thesis. Kenyatta University.

Ngowa, N. J.(2008). Mnyambuliko wa Vitenzi vya Kigiryama: Mtazamo wa Fonolojia Leksishi. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Nyabuto, J. C. (2015) Phonological (A) Symmetries of Nasal Prefixesin Bantu. PhD dissertation. Michigan State University.

Obuchi, M. S., & Mukhwana, A. (2010). Muundo wa Kiswahili: Ngazi na vipengele. Nairobi: A~Frame Publishers.

Okal, B.O. (2017). Uhakiki wa Fonimu na Miundo ya Silabi za Kiswahili. African Online Journal volume 13(1).

Owino, A.N. (2016). Mifanyiko ya Kimofofonolojia ya Ukuzaji na Udunishaji wa Nomino za Kiwanga. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Egerton.

Owino, D.(2003). Phonological Nativization of Dholuo Loanwords. Ph.D dissertation. University of Pretoria.

Prince, A., & Smolensky, P. (1993). Optimality Theory: Constraint Interactionin Generative Grammar. Malden, MA: Blackwell.

Riro, M. R. (2020). Linguistic Borrowing in a Language Contact Situation between Igikuria English. M.A Thesis. Kenyatta University.

Rosenberg, E. (2014). Lubuuya Noun Classes: Morphology and Semantic Affiliation. Gothenburg: University of Gothenburg.

Sasala, J. M., Mudogo, B. A., & Alati, R. A. (2019). Lexical Borrowing in Spoken Lukabaras in a Multilingual Context. International Journal of Linguistics, Literature and Translation, 2 (6), 31-37.

Shidiavai, M. (2015). A Phonological Analysis of Lwidakho Loanwords from Kiswahili and English. M.A thesis. University of Nairobi.

Sikuku, M. J. (2011). Syntactic Patterns of Anaphoric Relations in Lubukusu. Ph. D dissertation. The University of Nairobi.

Smith, J.L. (2009). “Source Similarity in loan adaptation: correspondence theory and the posited source – Language representation” In Steve Parker, ed; Phonological. Argumentative Essay. On Evidence and Motivation. London. Equinox.

Tasmia, K. (2016). Isizulu Adoptives from English and Afrikaans. M.A thesis. University of the Witwatersrand.

Tsangwa, K.J. (2017). Ukopaji wa Maneno ya Kiswahili Sanifu Katika Kigiriama. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Pwani.

Uushona, J. (2019). An Investigation into the Phonological and Morphological Integrationof German Loanwords into Oshiwambo. M.A Thesis. The University of Namibia.

Waithaka, N. W. (2010). Mofolojia ya Manenomkopo ya Gikuyu kutoka Kiswahili.Tasnifu ya Uzamili.Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Watulo, A.W. (2018). The Inflectional Structure of Lubukusu Verbs. Ph.D Dissertation.Kenyatta University.

Wohlgemuth, J. (2009). A Typology of Verbal Borrowings. Berlin: Mouton de Gruyter. Tadmor.

Tarehe ya Uchapishaji
10 April, 2023
Jinsi ya Kunukuu
James, T., & Onyango, J. (2023). Mchango wa Kiswahili katika Mofofonolojia ya Nominomkopo za Lubukusu. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 49-67. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1162