Umaratokezi wa Msamiati wa Sheng Katika Upokezilugha wa Kiswahili Miongoni mwa Wanadaraja la Awali Katika Shule za Msingi Mjini Mbale, Kaunti ya Vihiga, Kenya

  • Tim Mwenesi Mugesani Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknologia cha Jaramogi Oginga Odinga
  • Juliet Akinyi Jagero, PhD Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknologia cha Jaramogi Oginga Odinga
  • Naomi Nzilani Musembi, PhD Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknologia cha Jaramogi Oginga Odinga
Keywords: Lugha Ya Msimu, Umaratokezi, Upokezilugha, Kiingizi Cha Kiisimu
Sambaza Makala:

Ikisiri

Lugha ya Kiswahili ndiyo lugha iliyopangwa kisera kufundishwa kama somo la lazima kuanzia kiwango cha awali cha elimu ya shule za msingi nchini Kenya hasa katika mji wa Mbale ambao ndio mji mkuu wa Jimbo la Vihiga. Hata hivyo, kuwepo kwa matumizi ya lugha ya msimu ya Sheng miongoni mwa vijana wa mijini kumesababisha utata katika ufundishaji wa msimbo rasmi wa Kiswahili. Wanadaraja la awali katika shule za msingi hususan zile zinazopatikana mjini Mbale huenda wakaitumia lugha ya msimu ya Sheng katika mawasiliano yao wawapo shuleni. Hali hii inaweza kutatiza upokezilugha wa Kiswahili. Madhumuni ya makala hii ni kutathmini umaratokezi wa msamiati maarufu wa Sheng katika upokezilugha wa Kiswahili miongoni mwa wanadaraja la awali kwenye shule za msingi mjini Mbale. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Msingi wa Matumizi iliyoasisiwa na Tomasello (2003). Data katika utafiti huu ilitokana na utafiti wa nyanjani. Mbinu ya uchunzaji ilitumika katika kukusanya data hususan kwa kutumia mwongozo wa uchunzaji. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba umaratokezi wa juu wa kiingizi cha kiisimu huweza kuchangia katika upokezilugha. Matokeo yanadhihirisha kuwa umaratokezi wa juu wa msamiati maarufu wa Sheng unawezesha upokezilugha wa Kiswahili miongoni mwa wanadaraja la awali. Makala hii ni muhimu kwa vile inadhihirisha mbinu bora ambayo inaweza kutumiwa kushirikisha msamiati maarufu wa Sheng katika upokezilugha wa Kiswahili miongoni mwa wanadaraja la awali kwenye shule za msingi mjini Mbale

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.
Tarehe ya Uchapishaji
29 Septemba, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Mugesani, T., Jagero, J., & Musembi, N. (2022). Umaratokezi wa Msamiati wa Sheng Katika Upokezilugha wa Kiswahili Miongoni mwa Wanadaraja la Awali Katika Shule za Msingi Mjini Mbale, Kaunti ya Vihiga, Kenya. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 39-48. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.578