Michakato ya Kisemantiki Iliyoathiri Nomino za Kikamba Zilizoteuliwa katika Biblia
Ikisiri
Kipengele cha maana ni muhimu sana katika msamiati wa lugha kwa kuwa hufanikisha mawasiliano. Maana ya neno inapobadilika kwa namna yoyote ile huathiri mchakato mzima wa mawasiliano (Crowley, 1997). Iwapo maneno yanayotumiwa na mzungumzaji hayaeleweki na mpokeaji wa ujumbe, basi wawili hao hawataelewana. Biblia za Kikamba zilizoandikwa au kuchapishwa katika karne zilizopita zina maneno ambayo hayaeleweki na kizazi cha karne hii ya ishirini na moja. Biblia hizo zinazidi kutumiwa katika mahubiri makanisani na katika hafla mbalimbali kama vile harusi na mazishi. Makala hii imechunguza michakato ya kisemantiki inayohusishwa na mabadiliko ya maana kwa kuangalia jinsi nomino teule zilivyobadilika maana. Michakato hii imepatikana baada ya kuwahoji wazee na watoto kuhusu maana ya maneno teule ya Kikamba yaliyodondolewa kwenye Biblia ya Kikamba iliyochapishwa mwaka 1974. Majibu yao yamebainisha kwamba maana za nomino hizo zimepitia michakato ya mabadiliko ya maana kama vile upanuzi, ubanaji, usogezi, kusambaratika, tasfida, utowekaji na kuhamisha maana. Nadharia mbili zimetumika katika utafiti huu; Nadharia ya Dhana na nadharia ya Nyanja za Kisemantiki. Nadharia ya dhana imemwezesha mtafiti kupata maana asilia na maana za sasa za nomino kama dhana iliyoibuka akilini mwa wahojiwa baada ya nomino hizo kutamkwa au kuandikwa. Nadharia ya Nyanja za Kisemantiki imetumiwa kubainisha nomino ambazo zilihusiana kimaana na zingine kwa kuwa zilikuwa katika nyanja sawa za maana (Lyons, 1999). Matokeo ya utafiti huu yanakusudiwa kuwawezesha wasomaji wa Biblia za Kikamba kuelewa maana katika Biblia zilizotangulia hasa zile za miaka ya sabini (1970s) na kupunguza utata wa kimawasiliano baina ya wahubiri na waumini wa kizazi cha karne hii ya ishirini na moja. Aidha, wataalamu wa lugha wataweza kuandika kamusi ya visawe na kamusi ya maana za maneno kama inavyoeleweka katika jamii ya leo.
Upakuaji
Marejeleo
Abuga, B. (2013). Mabadiliko ya Lugha: Hali Maalum ya Lugha ya Ekegusii katika Eneo la Goseta kaunti ya Trans- Nzoia (Tasnifu ya Uzamili isiyochapishwa). Chuo Kikuu cha Moi, Eldoret.
Bible Society. (1974). Mbivilia (Kazi asilia iliyochapishwa mwaka 1954). United Bible Society.
Campbell, L. (2004). Historical linguistics. MIT Press.
Crowley, T. (1997). An introduction to historical linguistics. Oxford University Press.
Crystal, D. (2003). Language death. Cambridge University Press.
Ezeanya- Esiobu, C. (Ed.) (2019). Indigenous knowledge and education in Africa. Springer.
Gichuru, T. (2020). Mabadiliko ya maana za leksia za Kiswahili: Mtazamo linganishi wa kikale na kisasa (Tasnifu ya Uzamili isiyochapishwa). Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Hollmann, W. (2009). Semantic change. In J. Culpeper, P. Kerswill, R. Wodak, A. McEnery & F. Katamba (Eds.), English language: Description, variation and context (pp.301-313). Basingstoke: Palgrave
Kothari, C. R. (2004). Research Methodology: Methods and Techniques. Wisha Prakashan.
Lehman, W. P. (1962). Historical linguistics. Holt, Rinehart & Winston Inc.
Lyons, J. (1999). Language and linguistics: An introduction. Cambridge University Press.
Massamba, D. P. B. (2004). Sababu za kubadilika kwa maana za maneno: Mifano katika Kiswahili. Jarida la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Juzuu ya 55, uk.8-13.
McWhorter, J. (2020). The processes of semantic changes in language. Columbia University Publishers
Mojola, A. (2020). God speaks my language. Hippobook.
Nabhany, A. S. (1982). Barua, maoni, mapitio, mashairi… Katika Kiswahili, 49(2). TUKI.
Palmer, F. (1996). Semantics. Cambridge University Press.
Traugott, E. & Richard, B. (2002). Regularity in semantic change. Cambridge University Press.
Ullman, S. (1972). Semantics: An introduction to the science of meaning. Blackwell.
Wardhaugh, R. (2006). An introduction to sociolinguistics (4th ed.). Wiley- Blackwell.
Yule, G. (2000). The study of language. Cambridge University Press.
Copyright (c) 2025 Angela Nthenya Musyok, Vifu Said Makoti, John Musyoka Mutua

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.