Uhakiki wa Mabadiliko ya Kisemantiki katika Baadhi ya Vitenzi vya Kikamba

  • Angela Nthenya Musyoka Machakos University
  • John Musyoka Mutua Machakos University
  • Vifu Said Makoti Machakos University
Keywords: Semantiki, Dhana, Nyanja za kisemantiki, Mabadiliko, Maana
Sambaza Makala:

Ikisiri

Mabadiliko ya maana katika lugha ni jambo lisiloweza kuepukika kwa kuwa lugha ni kiungo hai kinachoathiriwa na wakati, mazingira, jamii na muktadha wa matumizi. Kadri muda unavyopita, maana zaidi huingizwa katika lugha na kusababisha maana za maneno hayo kubadilika. Neno linaweza kudumisha maana ya msingi huku pia likiendelea kupata maana nyingine mpya zinazoibuliwa na mazingira mapya ya kisemantiki (Ullman, 1972). Mabadiliko ya maana yanapotokea huathiri mawasiliano iwapo wazungumzaji wa lugha hawatafahamu mabadiliko yaliyoathiri lugha wanayoitumia. Katika lugha ya Kikamba, mabadiliko ya kisemantiki yanaonekana hasa kupitia matini za zamani kama Biblia ya Kikamba ya mwaka 1974 (Mbivilia). Baadhi ya msamiati uliotumiwa katika Biblia hii hautumiwi katika mazungumzo ya kawaida ingawa Biblia yenyewe inasomwa hadi leo makanisani, nyumbani na katika hafla za arusi au mazishi. Waumini wengi wanaosikiliza mahubiri kutoka Biblia hizo hawaelewi maana iliyokusudiwa ya baadhi ya vitenzi. Hali hii huleta utata wa mawasiliano kati ya vizazi. Makala hii imechunguza mabadiliko ya kisemantiki ya vitenzi kumi vilivyochaguliwa kutoka Mbivilia (1974). Nadharia ya Dhana imetumika kutathmini maana ya vitenzi hivyo kwa kutumia usaili wa wazee kumi na watoto kumi. Utafiti umefanywa kwa njia ya mahojiano na usomaji maktabani. Matokeo yameonyesha kuwa baadhi ya vitenzi vimepanuka maana, vingine vimebanwa, baadhi ya maana zimepotoshwa na zingine zimetoweka kabisa. Vitenzi kama vile vuta na mumunya vimepata maana mpya huku maana ya awali ikisahaulika. Watoto wa sasa hawatambui maana asilia ya vitenzi hivyo. Jambo hili linaashiria pengo la kiisimu kati ya vizazi. Matokeo ya utafiti huu yanakusudiwa kuwasaidia wasomaji wa matini za Kikamba hususan zilizoandikwa au kuchapishwa kabla ya karne ya ishirini na moja kuelewa maana ya vitenzi ili kuondoa utata wa mawasiliano baina ya vizazi

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abuga, B. (2013). Mabadiliko ya Lugha: Hali Maalum ya Lugha ya Ekegusii katika Eneo la Goseta kaunti ya Trans- Nzoia (Tasnifu ya Uzamili isiyochapishwa). Chuo Kikuu cha Moi, Eldoret.

Ashworth, E. J. (2020). Locke on Language. Canadian Journal of Philosophy, 14(1), 45-73. https://doi.org/10.1080/00455091.1984.10716368

Gichuru, T. (2020). Mabadiliko ya Maana za Leksia za Kiswahili: Mtazamo Linganishi wa Kikale na Kisasa. (Tasnifu ya Uzamili isiyochapishwa). Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Habwe, J. na Karanja, P. (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Phoenix Publishers.

Bible Society. (1974). Mbivilia (Kazi asilia ilichapishwa mwaka 1954). United Bible Society.

¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬Campbell, L. (2004). Historical Linguistics. MIT Press.

Crowley, T. (1997). An Introduction to Historical Linguistics. Oxford University Press.

Palmer, F. (1996). Semantics. Cambridge University Press.

Ullman, S. (1972). Semantics: An Introduction to the Science of Meaning. Barnes & Noble.

Tarehe ya Uchapishaji
20 October, 2025
Jinsi ya Kunukuu
Musyoka, A., Mutua, J., & Makoti, V. (2025). Uhakiki wa Mabadiliko ya Kisemantiki katika Baadhi ya Vitenzi vya Kikamba. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 8(2), 397-405. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3854