Uchambuzi wa Mtazamo wa Jamii Kuhusu Matumizi ya Taswira ya Mwanamke katika Nyimbo za Singeli za Wasanii Amani Hamisi (Manfongo) na Selemani Jabiri (Msagasumu) kwa Jamii ya Watanzania

  • Neema Alson Mtwale Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
  • Jacob Leopard Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
  • Hadija Jilala Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Keywords: Taswira ya wanawake, Nyimbo za Singeli, Jamii ya Watanzania, Ufeministi, Jamii ya Kiswahili
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inahusu Uchambuzi wa mtazamo wa jamii kuhusu matumizi ya taswira ya mwanamke katika nyimbo za singeli za wasanii Amani Hamisi (Manfongo) na Selemani Jabiri (Msagasumu) kwa jamii ya Watanzania. Utafiti ulifanyika katika Maktaba ya Chuo Kikuu Huria, Tawi la Mbeya, ambapo sampuli ya nyimbo saba kutoka kwa wasanii wawili ilichaguliwa kwa usampulishaji lengwa kutokana na umaarufu na maudhui yanayomhusu mwanamke. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Ufeministi ambayo imewezesha kuchambua namna wanawake wanavyosawiriwa na changamoto wanazokabiliana nazo katika jamii kinzani za kijinsia. Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa nyimbo teule zinatumia taswira mbalimbali za mwanamke kama vile “msambwanda”, “kitasa”, “chura” na “mkufunzi” ambazo zimegawanyika katika makundi ya taswira za uoni, masikizi, mguso na kimaaelezo. Taswira hizi zina uhalisia wa maisha ya wanawake katika jamii ya Kiswahili. Utafiti pia ulibaini kuwa baadhi ya taswira hizo zinakubalika kijamii kwa kuwa zinadumisha maadili, kuonya na kuelimisha, ilhali nyingine zinapotosha kwa kudhalilisha wanawake na kuendeleza mitazamo hasi. Aidha, dhima za taswira hizo zimehusisha kuonyesha maisha halisi ya mtaani na kijamii, kuonesha umuhimu wa familia, kudhalilisha wanawake wanaojiuza na kuonesha madhara ya kushindwa kujitawala. Utafiti umehitimisha kuwa nyimbo za singeli ni nyenzo muhimu ya fasihi ya Kiswahili, lakini zinahitaji mwelekeo chanya wa kijinsia. Mapendekezo yametolewa kwa wasanii, jamii na taasisi za utamaduni kuhakikisha matumizi ya taswira yanazingatia maadili, utu na usawa wa kijinsia.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Beauvioir, S. (1952). The Second Sex. London: Pan Book Publishers.

Caleb, C.W. (2013). Taswira ya Mwanamke katika Tamthilia ya Nguzo Mama na Mama Ee. Nairobi: Chuo Kikuu cha Nairobi.

Dawson, C. (2002). Practical Research Methods. How to Books Ltd: United Kingdom. Delhi: Wishwa Prakashan.

Ellman, M. (1969). Thinking about Women. New York: Published by Harcount Brace Jovanorich

Evans, J. (1995). Feminist Theory Today: An Introduction to Second-Wave Feminism, New Park, CA: Sage.

Farley, M. (2003). Prostitution, Trafficking and Traumatic Stress

Finnegan, R. (1977). Oral Poetry: Its Nature, Significance, and Social Context. Nairobi: Oxford University Press.

Frencher. P, (1962). Books of the Eskimo. London: Arthur Burker.

Gandhi, M. K. (2000). The Story of My Experiment With Truth. Porbandar: Beacon Press.

Githici. M. C. (2013). Ujagina wa mwanamke katika Pango.Tasinifu ya Shahada ya Uzamili (Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Nairobi.

Graham, J. (2011). The Psychology of Risk: Perception and Precautionary Behavior Risk. Analysis Journal.

Graham, J. D. (2011). The precautionary principle and risk analysis. In Risk Analysis and Society (pp. 33–47). Cambridge University Press.

Guston, D. H. (2004). Principles of Precaution: The Role of Precautionary Approaches in Risk Management. A Study of Legal and Ethical Conceptions.

Hook, B. (2000). Feminism Is for Everybody: Passionate Politics. South End Press.

Kant, I. (1985). Groundwork for the Metaphysics of Moral. London: Cambridge University Press

Kimaro, F.A. (2016). Kuchunguza Taswira ya Mwanamke na Mbinu za Kifani katika Mashairi: mfano wa Diwani ya Midulu. Tasnifu ya Shahada ya Uzamili (Haijachapishwa) katika Chuo Kikuu Huria Tanzania.

Kombo, D., & Tromp, D. L. A. (2006). Proposal and Thesis Writings, an Introduction. Africa: Nairobi Pauline’s Publications.

Kothari, C. R. (2008). Research Methodology: Methods and Techniques. New Delhi: New Age International Publishing.

Mackinnon, C. A. (1991). Towards a Feminist Theory of the State, London Havard University Press.

Matteru. M. (1982). “The Image of the Women in Tanzania Oral Literature” “A Survey” Katika Kiswahili Jarida la TUKI Chuo Kikuu cha Dar es Salaam vol 41 (2).

Mavisi, R. (2018). “Usawiri wa Wahusika wa Kike katika Riwaya Teule za Zainabu Burhan”. Katika S. Omary na R. P. Kidami (Wah) Kioo cha Lugha. Juz 16 (16), 65-80.

Mekacha, R. D. K. (1993). Muziki wa dansi na taswira ya mwanamke: Mtazamo wa kijinsia katika vyombo vya habari. Jarida la Kiswahili, 60(1), 51–66.

Mgalula, H. (2020). Dhima ya taswira katika nyimbo za muziki wa kizazi kipya [Tasnifu ya Shahada ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Dodoma].

Mligo, E. S. (2012). Jifunze Utafiti: Mwongozo Kuhusu Utafiti na Uandishi wa Ripoti Yenye Mantiki. Dar es Salaam: Ecumenical Gathering.

Mong’eri, O. B. W. (2000b). Utetezi wa Maadili katika Fasihi-Nathari ya Shaaban. Chuo Kikuu cha Nairobi

Mong’eri, R. (2000a). Maadili katika fasihi ya Kiswahili. Taasisi ya Elimu ya Kiswahili.

Mulokozi, M. M. (2017). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Musembi, N. N. na Mahero, T. (2022b) Nafasi ya Faisihi SAimulizi katika Karne ya 21: Tathmini ya Nyimbo za Jando za Jamii ya Wakamba. Mulika 2022.

Musembi, R., & Mahero, M. (2022a). Mchango wa nyimbo za kisasa katika malezi ya kijamii. Kiswahili Journal, 89(2), 115–132.

Mwari, A. (2016). Taswira za Hali na maana katika nyimbo za kizazi kipya. Kundi la Offiside Trick katika Mulika 2017, Toleo maalumu. Dar es salaam TATAKI.

Ntarangwi, M. (2004), Uhakiki wa Kazi za Fasihi. Augustana College; Rock Island.

Nyangweso, S. M. (2017). Nafasi na athari ya kiongozi wa kike katika tamthiliya teule za Kiswahili [Tasnifu ya Shahada ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Kenyatta].

Nyerere, J. K. (1973). Ujamaa: Essays on socialism. Oxford University Press.

Phil, J. (2005). Infidelity and betrayal in intimate relationships. Journal of Relationship Research, 9(3), 211–225.

Ponera, A. S. (2019). Misingi ya Utafiti wa Kitaamuli na Uandishi wa Tasinifu. Dodoma: Central Tanganyika Press.

Prusak, L. (1998). Working knowledge: How organizations manage what they know. Harvard Business Press.

Robson, C. (2007). How to do a Research Project: A guide for undergraduate students Cariton Victoria: Blackwell Publishing.

Sami, F. (2020). Utamaduni na maendeleo ya jamii: Nadharia na vitendo. Mkuki na Nyota Publishers.

Wafula, R. M. na Njogu, K. (2007) Nadharia za Uhakiki wa Fasihi, Nairobi. Jomo Kenyata Foundation.

Wamitila, K. W. (2003), Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Nairobi: Kenya Focus.

Walker, A., 1992. Possessing the Secret of Joy. New York: Harcourt, Brace, Jovanovich Press.

WHO. (2021). Sexual and reproductive health and rights: Defining the conceptual framework. World Health Organization. https://www.who.int/ reproductivehealth

Yego, M. (2013). Nafasi ya mwanamke katika nyimbo za taarab. Tasnifu ya Shahada ya Uzamili (Haijachapishwa), Chuo Kikuu cha Moi.

Yesaya, S. (2019). Ufemerali katika Muziki wa Bongo Fleva Tanzania. Tasnifu ya Uzamivu (Haijachapishwa). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Tarehe ya Uchapishaji
8 October, 2025
Jinsi ya Kunukuu
Mtwale, N., Leopard, J., & Jilala, H. (2025). Uchambuzi wa Mtazamo wa Jamii Kuhusu Matumizi ya Taswira ya Mwanamke katika Nyimbo za Singeli za Wasanii Amani Hamisi (Manfongo) na Selemani Jabiri (Msagasumu) kwa Jamii ya Watanzania. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 8(2), 370-383. https://doi.org/10.37284/jammk.8.2.3781