Nafasi ya Tashbihi katika Kufanikisha Maudhui katika Fasihi ya Watoto

  • Ibrahim Matin Chuo Kikuu cha Rongo
  • Simiyu Kisurulia Chuo Kikuu cha Kabianga
Keywords: Fasihi Ya Watoto, Nafasi, Tashbihi, Kufanikisha, Maudhui
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yalichunguza jinsi wasanii wa vitabu vya fasihi ya watoto wamefuma tashbihi katika kazi zao ili kueleza maudhui yanayowalenga watoto kwa kuongozwa na nadharia ya umuundo iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure (1916). Kupitia kwa njia ya kiupekuzi na uchanganuzi matini, vitabu vya Kisasi Hapana, Nimefufuka, Sitaki Iwe Siri, na Wema wa Mwana viliteuliwa kimakusudi, vikasomwa na kuchanganuliwa. Tashbihi mbalimbali na maudhui ya familia, elimu, nidhamu, bidii, ugonjwa na kifo yalitambuliwa na kujadiliwa kwa undani. Uhusiano kati ya tashbihi na maudhui hayo ulidhihirishwa. Matokeo ya jinsi tashbihi zinavyofanikisha kueleza maudhui yaliwasilishwa kithamano. Utafiti huu umeonyesha tashbihi na maudhui katika kazi tulizohakiki na pia unachochea washikadau katika uwanda wa fasihi ya watoto kuhakiki kazi za watoto kabla kuwateulia kuzisoma.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Andrea, A. (2011). Social Issues in Contemporary African American Young Adult Ficton: Iliyopakuliwa kutoka http://is.muni.cz/th/183848/pedf_m/social.

Bakize, L. H. (2014). Utangulizi wa Fasihi ya Watoto. Dar es Salaam: Moccony Printing Press.

Bakize, L. H., Ngugi, P. M. Y., & Lyimo, E. B. (2018). Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili ya Watoto nchini Tanzania na Kenya: Mkabala Linganishi. Kiswahili, 80(1).

Cass, J. E. (1967). Literature and the Young Child. London: Longman Group Ltd.

Chimera, R. & Kimani, N. (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi: Jommo Kenyatta Foundation.

Gall, D. M., Borg, R. W., na Gall, P. G. (1996). Education Research: An introduction (6thed.) New York: Longman Publishers.

Gatere, L. N. (2020). Usawiri wa Familia ya Kisasa katika Fasihi ya Watoto Nchini Kenya. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi.

Gituku, N. (1990). “Maigizo ya Kienyeji ya Watoto Nchini Kenya”.Tasnifu ya M A, Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Huck, C. (2001). Childrens Literature in the Elementary School. 7thed. New York: McGraw-Hill Company.

ILO. (2017). Global Estimates of Child Labour: Results and Trends, 2012-2016. Geneva(…..)

Kothari, R. C. (2008). Research Methodology: Methods and Techniques. New Delhi: New Age International Publishing Ltd.

Miricho, M., & Mbuthia, E. M. (2017). The impact of the depiction of children in selected Swahili children stories. International Journal of Contemporary Applied Sciences, 4(1), 8-20.

Miricho, E. M. (2015). Usawiri wa Watoto katika Hadithi za Mwepesi wa Kusahau na Likizo ya Mkosi.Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Moi.

Miricho, M., Sheila, P. Wandera, S. na Nabea, W. (2019). Fasihi ya Watoto ya Kiswahili na Mshikamano wa Kitaifa katika Mwanga wa Lugha- Makala Teule ya Kongamano la Chakita 2018. Moi University Press.

Msokile, M. (1993). Misingi ya Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: East African Educational Publishers.

Ntarangwi, M. (2004).Uhakiki wa Kazi za Fasihi. Rock Island: IL 61201

Senkoro, F.E.M.K. (2011). Fasihi. Dar es Salaam. KAUTTU LTD.

Syambo, K. na Mazrui, A. (1992). Uchambuzi wa Fasihi. Nairobi: East African Educational Publishers.

Truex, D. (1996). Text-based analysis: A brief introduction. College of Business Administration: Georgia State University. Retrieved on, 10(07), 05.

Tucker, N. (1981). The Child and the Book.Apsychological and Literary Explanation.Cambridge: Cambridge University College.

Verma, R. G (2019) Women Writers for Children in India: A Kaleidospic View. Sharma, V. (ed), Feminist Discourses in Indian Context: Assertion, Identity and Agency. New Delhi: Authorpress.

Wambua, M. S. (2001). Mtindo wa nyimbo za Kakai Kilonzo. Tasnifu ya Uzimili, Kenyatta University.

Wamitila, K. W. (2010).Kanzi ya Fasihi 1 Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi. Nairobi: Wide-Muwa.

Wamitila, K. W. (2003). Kamusi ya Fasihi. Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Books.

Wamitila, K. W. (2003). Kichocheo Cha Fasihi Simulizi na Andishi. Toleo la Pili. Nairobi: Focus Books.

Wamitila, K. W. (2002). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi: Phoenix Publishers Limited.

Tarehe ya Uchapishaji
8 Julai, 2021
Jinsi ya Kunukuu
Matin, I., & Kisurulia, S. (2021). Nafasi ya Tashbihi katika Kufanikisha Maudhui katika Fasihi ya Watoto. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 3(1), 58-69. https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.355