Ubunifu na Mwonoulimwengu wa Mwandishi: Mifano ya Kazi za Ken Walibora

  • Ibrahim Matin Chuo Kikuu cha Rongo
  • Simiyu Kisurulia Chuo Kikuu cha Kabianga
Keywords: Ubunifu, Mwonoulimwengu, Mwingilianomatini
Sambaza Makala:

Ikisiri

Katika kazi ya fasihi, mawazo, mafunzo na falsafa ya msanii hubainisha msimamo wake kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii. Msimamo ni ile hali ya mwandishi kuamua kufuata na kushikilia jambo fulani. Jambo hili huweza kukataliwa na wengi lakini akalishikilia tu. Msimamo ndio huweza kuwatofautisha wasanii wawili au zaidi wanaoandika kuhusu mazingira yanayofanana. Hili ambalo msanii anashikilia sana ndilo tunaloita katika utafiti huu kuwa mwonoulimwengu wa mwandishi. Ni vyema kujiuliza ni mambo gani yanayomsukuma na kuchochea mwandishi Ken Walibora kuchukua mawazo, msimamo na mkondo fulani katika uandishi wake. Uchanganuzi huu ulinuia kuchunguza mwonoulimwengu wa Ken Walibora kwa kujaribu kudokoa mawazo na falsafa zake kama zinavyojitokeza katika kazi zake za kisanaa. Huu ulikuwa utafiti wa maktabani ulioongozwa na nadharia za uhalisia na mwingilianomatini kuchunguza mwonoulimwengu wa Ken Walibora kupitia yale anayosema kujihusu na yale wengine wanasema kumhusu kisha kuyalinganisha na kazi za fasihi alizoandika kwa lengo la kuona mfanano wa mwonoulimwengu wake kwa sababu mwonoulimwengu unaonekana kutokana na maudhui yanayoendelezwa katika kazi za kisanaa. Kwa kutumia mbinu ya uteuzi sampuli maksudi tuliteua vitabu sita: Siku Njema (1996), Damu Nyeusi (2008), Kidagaa Kimemwozea (2012), Nasikia Sauti ya Mama (2014), Mbaya Wetu (2014) na Kisasi Hapana (2008). Tulivilinganisha ili kutambua mfanano wa mwonoulimwengu wa Ken Walibora katika vitabu hivi. Tulitathmini mwonoulimwengu huu kwa kujaribu kuelewa namna anavyosuka maudhui katika kazi zake kwa sababu mwonoulimwengu hudhihirika katika maudhui. Utafiti huu utachangia katika kufanyiza akili, kupanua uelewaji, kunoa nguvu za kufikiri, kupanua mwono, kukuza uwazaji na hisi ya ujumui ambalo ni lengo kuu la kazi yoyote ile ya fasihi. Wasomaji wa kazi za Ken Walibora watapata kuelewa kazi zake vizuri zaidi kwa kuwa na picha kubwa ya msanii huyu akilini. Pia inaweza kuwa kichocheo kwa wasanii wapya ili kujua namna ya kupata maoni ya kusuka kazi zao

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Allen, G. (2000). Intertexuality. New York: Routledge.

American Heritage Dictionary of The English Language (2022). Boston: Houghton Mifflin.

Beck, D. (Ed). (1991). Opening the American Mind. Grand Rapids, Michigan: Baker Book House.

Coombes, H. (1953). Literature and Critism. Chatto and Windus: Australia.

Bertoncini, E. Z. (2007). A Friend in Need is a Friend Indeed: Ken Waliboras Novel Kufa Kuzikana. Katika Swahili forum 14 (153-163).

Gall, D. M., Borg, R. W., na Gall, P. G. (1996). Education Research: An introduction (6th ed.) New York: Longman Publishers.

Hill, C. (2O19). A Worldview Approach to Science and Scripture. Grand Rapids Michigan: Kregel Academic.

Kothari, R. C. (2008). Research Methodology: Methods and Techniques. New Delhi: New Age International Publishing Ltd.

Kristeva, J. (1986). The Kristeva Reader, edited by T. Moi. Oxford: Basil Blackwell.

Leland, R. (1976). The Literature Of The Bible. Grand Rapids, Michigan: Zondervan.

Neuman, W. L. (2006). Social Research Methods Qualitative And Quantitative Approach (6th Ed). Upper Saddle River: Pearson.

Ntarangwi, M. (2004). Uhakiki wa Kazi za Fasihi. Rock Island: IL 61201

Raj, P. P. E. (2015). “Text/Texts: Interogating Julia Kristevas Concept of Intertextality”. Research Journal of Humanities and Social Sciences 2319-7889 (3) (2015): 77-80.

Samples, K. R. (2007). A World of Difference: Putting Christian Truth-Claims to the Worldview Test (Reasons to Believe). USA: Baker Books Publishing Group.

Sire, J. W. (2010). Why Should Anyone Believe Anything at All? Westmont Illinois: Intervarsity Press.

Spirkin, A. (1990). Fundamentals of Philosophy. Moscow: Progress Publishers.

Truex, D. P. (1996). Text Based Analysis: A Brief Introduction. Accessed on 25 august 2023.

Walibora, K. W. (2014). Nasikia Sauti ya Mama. Nairobi: Longhorn Publishers (Kenya) Ltd.

Walibora, K. W. (2014). Mbaya Wetu. Nairobi: Moran Publishers.

Walibora, K. W. (2012). Kidagaa Kimemwozea. Nairobi: Spotlight Publishers (EA) Limited.

Walibora, K.W. (2010). Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine. Nairobi: Longhorn publishers.

Walibora, K. W. (2008). Kisasi Hapana. Nairobi: Oxford University Press East Africa LTD.

Walibora, K (2003). Kufa Kuzikana. Nairobi: Longhorn Publishers (Kenya) Ltd.

Walibora, K. W. (2001). Ndoto ya Amerika. Nairobi: Sasa Sema Publications.

Walibora, K. W. (1996). Siku Njema. Nairobi: Longhorn Publishers (Kenya) Ltd.

Wamitila, K.W. (2003). Kamusi ya Fasihi, Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Publications Ltd.

Wamitila, K.W. (2002). Uhakiki wa Fasihi. Misingi na Vipengele vyake. Nairobi. Phoenix Publications Ltd.

Wellek, R. na Warren, A. (1949). Theory of Literature. New York: Penguin.

Tarehe ya Uchapishaji
27 May, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Matin, I., & Kisurulia, S. (2024). Ubunifu na Mwonoulimwengu wa Mwandishi: Mifano ya Kazi za Ken Walibora. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 253-271. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1954