Usawiri Wa Vyanzo Vya Dhuluma Za Kijinsia Katika Riwaya Teule Za Kiswahili

  • Pamella Tsiyeli Ngeleso Chuo Kikuu cha Mount Kenya
  • Alex Umbima Kevogo Chuo Kikuu cha Garissa
Keywords: Usawiri, Dhuluma za Kijinsia, Riwaya Teule
Sambaza Makala:

Ikisiri

Ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya 2020 inatoa takwimu za kusikitisha kuhusu idadi ya waathiriwa wa dhuluma za kijinsia duniani. Data hii ilichochea utafiti huu kuhusu dhuluma za kijinsia na zinavyosawiriwa katika kazi za fasihi. Kimsingi utafiti huu ulikuwa wa maktabani; ambapo watafiti walisoma na kuhakiki riwaya teule za ‘Nyuso za Mwanamke’ ya Said Ahmed Mohamed na ‘Unaitwa Nani?’ ya Kyalo Wadi Wamitila. Uteuzi wa sampuli wa kimakusudi ulitumika ili kuchagua riwaya moja ya kila mwandishi kwa mujibu wa mada ya dhuluma za kijinsia. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Ufeministi Mamboleo iliyoasisiwa na Jacques J. Zephire mwaka wa 1982. Aidha, utafiti huu ulizingatia pia Nadharia ya Hegemonia ya Ubabedume iliyoasisiwa na Raewyn Connell mnamo 1987. Kimsingi, utafiti huu ulilenga kubainisha vyanzo vya dhuluma ya kijinsia na namna vinavyosawiriwa katika riwaya ‘Nyuso za Mwanamke’ na ‘Unaitwa Nani?’. Matokeo ya utafiti yanayohusu data ya kiuthamano yaliwasilishwa kupitia kwa maelezo na ufafanuzi unaotolewa kwa kuegemea mihimili ya Nadharia ya Ufeministi Mamboleo na Nadharia ya Hegemonia ya Ubabedume. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa riwaya hizi zinasawiri wahusika mbalimbali wanaokuza maudhui ya dhuluma ya kijinsia. Utafiti huu utawafaa wahakiki wengine wa kazi za fasihi kupata maarifa mapya yanayohusu masuala ya kijinsia. Aidha, wanaharakati wanaopambana na suala la dhuluma za kijinsia watapata mapendekezo ya waandishi na watafiti kuhusu njia za kupambana na tatizo hili. Isitoshe, serikali na vyombo visivyo vya kiserikali vinavyoshughulikia suala la dhuluma za kijinsia vitashauriwa kuhusu njia mwafaka za kudumisha utangamano na mahusiano ya kijinsia duniani, Afrika, Afrika Mashariki na hata nchini Kenya

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Chimerah, R. & Njogu, K. (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi. Jomo Kenyatta Foundation.

DuBois, E. C. (1997). Harriot Stanton Blatch and the Winning of Woman Suffrage. New Haven, Conn.: Yale University Press.

Flexner, E. (1996); Century of Struggle: The Woman's Rights Movement in the United States. The Belknap Press.

Goodman, R. T. (2010). Feminist Theory in Pursuit of the Public: Women and the 'Re-Privatization' of Labor. New York: Palgrave Macmillan.

Kibigo, M. L. (2019). Ubabedume katika Majigambo ya Miviga ya Shilembe na Mchezaji wa Mayo ya Wahusika Nchini Kenya Kwa Mtazamo wa Kisemantiki. (Tasnifu ya Uzamifu Chuo Kikuu cha Masinde Muliro) Kakamega, Kenya.

Malenya, M. M. (2012). Matumizi ya Lugha katika Fasihi Simulizi. Mwanza: Inland Press.

Masibo, B. (2009). Gendered Perspectives in Novels of Ngugi wa Thiong’o and Walker A. (Phd Thesis, University of Nairobi. Unpublished).

Njogu, K. & Wafula, R.M. (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi. Jomo Kenyatta Foundation.

Pilcher, J. & Welchan, M. (2004). Fifty Key Concepts in Gender Studies. London: Sage Publications.

Beauvoir S.(1949). The Second Sex. London: Pan Books Publishers.

Nyangweso M. S.(2017). Nafasi na Athari za Kiongozi wa Kike katika Tamthilia Teule za Kiswahili. Tasnifu; Chuo Kikuu cha Maasai Mara.

Mboya L.A. (2018). Dhuluma kama Kichocheo cha Mzinduko wa Mwanamke Katika Riwaya ya Kiswahili.

Khamis S. A. (2012). 'Riwaya Mpya ya Kiswahili. Utandawazi au Utandawazi? Jinsi Lugha ya Riwaya mpya ya Kiswahili Inavyodai.' Bayreuth University.

WHO (2020) World Report on Gender Based Violence. Geneva: World Health Organisation

Tarehe ya Uchapishaji
5 July, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Ngeleso, P., & Kevogo, A. (2024). Usawiri Wa Vyanzo Vya Dhuluma Za Kijinsia Katika Riwaya Teule Za Kiswahili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 308-318. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.2024