Taswira ya Distopia katika Riwaya ya Kimajaribio ya Kiswahili: Mfano wa Riwaya ya Bina-Adamu na Dunia Yao

  • Mwove Phyllis Mwende Chuo Kikuu cha Mount Kenya
  • Alex Umbima Kevogo Chuo Kikuu cha Garissa
Keywords: Distopia, Riwaya ya Kimajaribio, Taswira, Utandawazi
Sambaza Makala:

Ikisiri

Mustakabali wa Bara la Afrika umekuwa suala la msingi katika maudhui ya riwaya ya kisasa ya Kiswahili. Fasihi ya kimajaribio inayoakisi hali za kidistopia inachora taswira hasi za mustakabali wa Bara la Afrika. Mazingira ya kidistopia ni mandhari yanayokabiliwa na kila aina ya matatizo au uovu uliokithiri ambayo huwa ya kiubunifu. Dhana hii hutumiwa kueleza jamii ambayo sheria zake hubadilishwa na kuishia kuwa za kuwadhalilisha wanajamii kupita kiasi. Kwa ujumla, wanajamii wanaojipata kwenye ulimwengu wa aina hii huwa kwenye njiapanda. Wanajamii hao huwa wamekwisha poteza tumaini la kuishi kutokana na dhuluma zinazowakabili. Baadhi yao hutamaushwa na ugumu wa maisha na kutamani kuangamia au kujiangamiza ili kuepuka ulimwengu huo wa shida. Kazi za fasihi zinazofuata mkondo wa kidistopia hudhamiria kutoa tahadhari au kuhamasisha jamii kuwajibika ili kuepuka maangamizi yanayokuja. Kazi hizo ni za utabiri wa mambo yanayoweza kutokea baadaye. Makala hii inakusudia kuonyesha jinsi taswira ya kidistopia inavyojitokeza katika riwaya ya kimajaribio ya Kiswahili kwa kutumia Nadharia ya Usasabaadaye ilioasisiwa na Linda Hutcheon na kufafanuliwa zaidi na Patricia Waugh. Riwaya mbili za kimajaribio; Dunia Yao (2006) ya Said Ahmed Mohamed na Bina-Adamu! (2002) ya Kyallo Wadi Wamitila zilitueliwa kimaksudi ili kuonyesha jinsi taswira ya distopia inavyobainika. Utafiti ulifanywa maktabani. Data ilikusanywa kutokana na usomaji wa kina wa riwaya teule ulioongozwa na mihimili ya Nadharia ya Usasabaadaye. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya kimaelezo kwa mujibu wa Nadharia ya Usasabaadaye. Matokeo ya utafiti yanabainisha kuwa waandishi wana sababu za kimsingi za kusawiri mandhari ya kidistopia ili kutoa taswira kamili ya nchi za Kiafrika katika muktadha wa baada ya ukoloni chini ya utandawazi, mfumo wa soko huria, ubeberu mpya, ubinafsi, taathira za kigeni na uporomokaji wa kasi wa nguzo za maisha ya Kiafrika

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Barth, J. (1984). The literature of replenishment. In The Friday Book: Essays and Other Fiction. London: The Johns Hopkins University Press.

Baudrillard, J. (1988). America. London: Verso.

Bertoncini, E. (2016). Postmodernism in Swahili fiction and drama. In Vierke, C. & Greven, K. (Ed.), Utopia/distopia in Swahili fiction. Koln: Rudiger Koppe Verlag.

Diegner, L. (2016). Dunia Yao: Critical visions of the future in Swahili fiction. In Vierke, C. & Greven, K. Utopia/distopia in Swahili fiction. Koln: Rudiger Koppe Verlag.

Gromov, M. D. (2016). ‘Local Achievement’ or ‘External Influence’? Intertextuality and Political Satire in the ‘New’ Swahili Novel in Kenya. Dunia Yao: Utopia/Dystopia in Swahili Fiction, 57-71.

Hutcheon, L. (1988). A poetics of postmodernism: History, theory, fiction. New York: Routledge.

Ignatowicz, A. (2007). Depictions dystopia in Brave New World, 1984 and Handmaid’s Tale. Unpublished thesis.

Kevogo, U.A. (2016). Taswira ya utandawazi katika riwaya mpya ya Kiswahili: Mfano wa riwaya ya Dunia Yao. Kioo cha Lugha, Juzuu 5, 108-126.

Longhorn Publishers (2019). Kamusi ya Karne ya 21. Nairobi: Longhorn Publishers Limited.

Mohamed S.A. (2006). Dunia Yao. Nairobi: Oxford University Press East Africa Ltd.

Rettova, A. (2016). From memis to mize: Philosophical implications of departure from literary realism. In Vierke, C. & Greven, K. Utopia/distopia in Swahili fiction. Koln: Rudiger Koppe Verlag.

Traore, F.A. (2015). Postmodernism as seen through the Swahili Novel: A reading of Babu Alipofufuka and Dunia Yao by S.A. Mohamed. Journal of African Cultural Studies, 27:1, 20-29.

Wafula, R. na Njogu, K. (2007). Nadharia na Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Longhorn Publishers.

Wamitila, K. W. (2002). Bina-Adamu. Nairobi: Phoenix Publishers.

Waugh, P. (2002). Metafiction: Theory and practice of self conscious fiction. London: Routledge.

Tarehe ya Uchapishaji
5 November, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Mwende, M., & Kevogo, A. (2023). Taswira ya Distopia katika Riwaya ya Kimajaribio ya Kiswahili: Mfano wa Riwaya ya Bina-Adamu na Dunia Yao. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 435-447. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1556