Athari za Mtagusano wa Lugha ya Kiswahili na Kikuyu kwa Lugha ya Kishona

  • Mercy Moraa Motanya Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Stephen Njihia Kamau, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Boniface Ngugi, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Athari, Jamiilugha, Kishona, Washona, Mtagusano, Uthabiti wa Kiisimujamii
Sambaza Makala:

Ikisiri

Utafiti huu unalenga kuchunguza athari zinazotokana na mtagusano wa lugha ya Kiswahili na Kikuyu kwa lugha ya Kishona. Shona ni kabila mojawapo la Wabantu ambao asili yao ni nchini Zimbabwe na walifika nchini Kenya zaidi ya miaka sitini iliyopita kama wamishenari. Kufikia sasa, Washona wametagusana na jamiilugha mbalimbali nchini Kenya katika Kaunti ya Kiambu inayojulikana kwa wingilugha hasa kwenye mitaa ya Kinoo, Kikuyu, Kiambaa, Gitaru, na Githurai. Mtagusano wa lugha unapotokea, lugha husika huathirika kwa viwango mbalimbali kama vile kwenye fonetiki, kifonolojia, kimofolojia, kisintaksia na hata kisemantiki. Utafiti  huu uliongozwa na nadharia ya uthabiti wa kiisimujamii wa lugha iliyoasisiwa na Giles, Bourhis na Taylor (1977) na kuendelezwa na Landweer (2000) na nadharia ya uzalishaji kijamii ya Bourdieu (1977). Mawanda mawili yalihusishwa ambayo ni utafiti wa maktabani na wa nyanjani. Utafiti wa nyanjani ulifanyika katika makazi ya wanajamiilugha ya Kishona ili kupata data ya moja kwa moja iliyojibu swali la utafiti. Jumuiya ya utafiti ilikuwa kabila la Washona wanaoishi katika mitaa mitano ya kaunti ya Kiambu.Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kimaksudi na kwa njia elekezi. Mbinu zilizotumiwa katika ukusanyaji data ni pamoja na hojaji, mahojiano, uchunzaji, mijadala ya vikundi vidogovidogo na maswali mepesi yaliyoandaliwa kimbele. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kutumia mbinu changamano. Matokeo yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo, takwimu na asilimia huku yakiongozwa na nadharia mbili za utafiti. Kufuatia juhudi za UNESCO za kudumisha lugha asilia, utafiti huu ulikuwa wa manufaa kwa taifa la Kenya na mataifa mengine kwa kuwa uliongezea data muhimu katika kuhifadhi utamaduni wa Washona na mwelekeo wa udumishaji kwa lugha za kabila mbalimbali

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Appel, R., & Muysken, P. (2005). Language contact and bilingualism. Amsterdam University Press.

Auer, P., & Wei L. (2009). Code-switching/mixing. The SAGE handbook of sociolinguistics, 460-478.

Best, W., & Kahn, J. (2010). Research in Education, New Jersey U.S.A: Person Prentice.

Bichang’a, W. N (2019) “Language Shift or Maintainance? A Sociolinguistic Analysis of the Ilwana Language of Tana River County,” Les Cahiers d’Afrique de l’Est/The East African Review[online],53|2019 URL:http://journals.openedition.org/eastafrica/839;DOI:https://doi.org/10.4000eastafrica.839

Chambers, J. & Jack, K. (1995). Sociolinguistic theory: Linguistic variation and its social significance. Oxford: Blackwell.

Cook, V. J. (2010). The relationship between first and second language acquisition revisited. The Continuum companion to second language acquisition, 137-157.

Denzin, K., & Lincoln, Y.(2011). The SAGE Handbook of Qualitative Research. U.S.A: SAGE Publication, Inc.

Fishman, J. (1991). Reversing Language Shift: Theoretical and Empirical Foundations of Assistance to Threatened Languages. Clevedon: Multilingual Matters Ltd.

Florian, L. (1998) ‘Inclusive practice: what, why and how?’ in C. Tilstone, L. Florian and R. Rose (eds) Promoting Inclusive Practice. London: Routledge.

Giles, H., Taylor, D. M., & Bourhis, R. Y. (1977). Dimensions of Welsh Identity. European Journal of Social Psychology, 7(2), 165-174

Grosjean, F. (1982). Life with two languages: An introduction to bilingualism. Harvard University Press.

Heine, B. (1992). Language Policies in Africa. In: R. Herbert (ed.), Language and

Society in Africa. The Theory and Practice of Sociolinguistics, pp. 23–35. Cape Town: Witwatersrand University Press.

Holmes, J. (2001). An introduction to sociolinguistics. New York; Harlow, Eng: Longman.

Kamau, S. (2015) Taathira za Kiswahili na Lugha Nyingine kwa Uthabiti wa Kiisimujamii wa Lugha za Mama Mijini Nairobi, Kiambu na Thika. Chuo Kikuu cha Kenyatta.Tasnifu ya Uzamifu.

Kerswill, P., & Williams, A. (2000). Creating a new town koine: Children and language change in Milton Keynes. Language in society, 29(1), 65-115.

Krauss, M. (1992). ‘The World’s Languages in Crisis’, Language 68:4-10

Landweer, L. (2000). Indicators of Ethno Linguistic Vitality’. Notes on Sociolinguistics pg 5 – 22 [Online:http//www.s.l. org /socialx/ndg-lg-indicators.html]

Lune, H. et al. (2010). Perspective in Social Research Methods and Analysis. Thousand Oaks: SAGE Publication Inc.

Malechova, M. (2016) Multilingualism as a Sociolinguistic Contact Phenomenon With Regard to Current Forms of Multilingual Communication: Codeswitching as One of The Contemporary Communication Trends. Informatologia,49(1-2), 86-93. Retrieved from http://hreak.srce.hr/161904

Malik, T. G. (1994). Lexical Borrowing: A Study of Punjabi and Urdu Kinship Terms. Language in India, 10(8).

Mberia, K. (2014). The place of indigenous languages in African development. Language, 2, L2.

Milroy, L., & Muysken, P. (Eds.). (1995). One speaker, two languages: Cross-disciplinary perspectives on code-switching (Vol. 10). Cambridge University Press.

Mirvahedi, S. (2014). Language policy, language practices and language shift in tabriz., Victoria University of Wellington, Australia. Unpublished doctoral dissertation.

Mufwene, S. S. (2014). Language ecology, language evolution, and the actuation question. The sociolinguistics of grammar, 13-36.

Mugaddam, A. R. (2006). Language maintenance and shift in Sudan: the case of migrant ethnic groups in Khartoum. International journal of the sociology of language, (181), 123-136.

Nagy, G. (2010). Language and Meter. A companion to the ancient Greek language, 370-387.

Ngure, K (2012). From Rendille to Samburu: A Language Shift Involving Two Mutually Unitelligible Languages of Northern Kenya. University of Nairobi: Tasnifu ya Uzamifu.

Obiols, M. (2002). “The Matched Guise Technique: A Critical Approcimation to a Classic Test for Formal Measurement of Language Attitudes.

Orodho, J. (2004). Elements of Educational Research and Social Science Research Methods. Nairobi: Masola Publishers.

Pfaff, C. W. (1979). Constraints on language mixing: Intrasentential code-switching and borrowing in Spanish/English. Language, 291-318.

Poplack, S. na Meechan, M. (1998). Introduction: How languages fit together in codemixing. International journal of bilingualism, 2(2), 127-138.

T’sou, B. K. (2001). Language contact and lexical innovation. In New Terms for New Ideas (pp. 35-56). Brill.

Thomason, S. G., & Kaufman, T. (1988). Language contact (Vol. 22). Edinburgh: Edinburgh University Press.

UNESCO (2003). Language vitality and endangerment: UNESCO ad hoc expert group on endangered languages. Paris: UNESCO.

Wagalla, S. (2019). Citizens or Refugees? The Case of the Shona in Kenya (1962-2017) (Doctoral dissertation, University of Nairobi).

Weinreich, U (1953). Languages in Contact. NewYork: Linguistic Circle of New York

Tarehe ya Uchapishaji
22 January, 2024
Jinsi ya Kunukuu
Motanya, M., Kamau, S., & Ngugi, B. (2024). Athari za Mtagusano wa Lugha ya Kiswahili na Kikuyu kwa Lugha ya Kishona. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 7(1), 39-55. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1703