Mchango wa Tasinia ya Sheria katika Ukuzaji na Uenezaji wa Kiswahili Tanzania: Mifano kutoka Mahakama ya Tanzania na Taasisi za Wadau wa Sheria

  • Joseph Hokororo Ismail, PhD Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto
Sambaza Makala:

Ikisiri

Kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania kunategemea mambo mbalimbali kama vile kutumika katika maeneo na mifumo rasmi kwenye jamii husika. Historia ya lugha ya Kiswahili inaonekana kukua tangu wakati wa biashara ya watumwa, Waarabu, kipindi cha ukoloni wa Wajerumani na kipindi cha ukoloni wa Waingereza. Harakati za kusanifisha lugha ya Kiswahili kwa hatua mbalimbali za usanifishaji wake (1928- 1930) zilichapuza kukua na kusambaa kwa lugha ya Kiswahili. Baada ya uhuru wa Tanzania, Tanganyika wakati huo, lugha ya Kiswahili ilizidi kukua hasa baada ya serikali katika mwaka 1962 kuifanya kuwa lugha ya Taifa na lugha rasmi ya mawasiliano katika shughuli mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali. Vyombo mbalimbali vya kukuza Kiswahili viliundwa kama vile Baraza la Kiswahili la Tanzania (BAKITA), Taasisi ya Ukuzaji wa Kiswahili (TUKI) kutokana na kamati iliyokuwa ya usanifishaji wa lugha ya Kiswahili ya Afrika Mashariki na Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, kuvitaja kwa uchache. Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilikuwa na jukumu la kufundisha somo la Kiswahili na wataalamu wake kuandika masuala mbalimbali ya lugha ya Kiswahili. Mazoea yamekuwa kuviangalia vyombo hivi na serikali kwa ujumla kama ndio vyombo pekee vyenye wajibu wa kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili Tanzania. Tukiachilia mbali vyombo hivi tulivyovitaja, yapo maeneo mengine yanayoweza kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili ambayo ama hayajaangaliwa kwa kiasi cha kutosha au yamesahaulika. Moja ya maeneo ambayo matumizi ya lugha ya Kiswahili yanaweza kusukuma kukua na kuenea kwake ni eneo la tasinia ya sheria. Lengo la makala haya ni kubainisha namna tasinia ya sheria na taasisi za sheria zinavyosaidia kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini Tanzania. 

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Carroll, J. (1995). The use of interpreters in court. International Journal of Speech, Language and the Law, 2(1), 65-73.

Knappert, J. (2001). Law Glossary of Islamic Terms in Swahili. Mtwara: Benedictine Publications Ndanda.

Malangwa, P. S. (2016). Terminological Challenges and their Impact on the Translation of Specialized Texts: An Analysis of Pharmaceutical Translations from English into Kiswahili. Kioo cha Lugha, 16(1), 126-138.

Mukoyogo, M. C. (1991). Can law be taught in Kiswahili?. Eastern Africa Law Review, 18(2), 227-246.

Rwezaura, B. (1993). Constraining Factors to the Adoption of Kiswahili as a Language of the Law in Tanzania. Journal of African Law, 37(1), 30-45.

Vlachopoulos, S. (2004). Translating the untranslatable? The impact of cultural constraints on the translation of legal texts. In J. Gibbons, J., Nagarajan, H., Prakasam, V., & Thirumalesh, K. V., (Eds.) Language in the Law (pp. 100-115). Delhi: Orient Longman.

Wanitzek, U., & Twaib, F. (1996). The Presentation of claims in matrimonial proceedings in Tanzania: a problem of language and legal culture. AAP, 47, 115-137.

Tarehe ya Uchapishaji
9 Juni, 2020
Jinsi ya Kunukuu
Ismail, J. (2020). Mchango wa Tasinia ya Sheria katika Ukuzaji na Uenezaji wa Kiswahili Tanzania: Mifano kutoka Mahakama ya Tanzania na Taasisi za Wadau wa Sheria. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 2(2), 11-22. https://doi.org/10.37284/eajss.2.2.160