Uchunguzi wa Changamoto za Walimu na Wanafunzi wa Kiswahili katika Shule za Upili Nchini Kenya

  • Linnah Apondi Okeyo Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • John N. Kimemia, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
  • Sophia M. Ndethiu, PhD Chuo Kikuu cha Kenyatta
Keywords: Changamoto, Visababishi, Mikakati, Ufunzaji na Ujifunzaji, Mwelekeo mseto, Kiswahili na Matokeo
Sambaza Makala:

Ikisiri

Lengo la utafiti ni kuchunguza changamoto walizokabiliana nazo walimu na wanafunzi wa Kiswahili katika shule za upili nchini. Kiswahili ni lugha rasmi na ya taifa nchini Kenya tena ni somo la lazima linalofundishwa na kutahiniwa katika shule za msingi na za upili. Kimataifa, ni lugha inayotambuliwa kama chombo cha mawasiliano. Kuimudu lugha hubainika kupitia ujuzi wa mtu katika stadi zake kuu; kusoma, kuandika, kusikiliza, na kuongea. Umilisi na utendaji katika lugha hata hivyo huweza kuathiriwa pakubwa na mambo kadhaa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Utabia na Utambuzi. Muundo wa utafiti ulikuwa usoroveya na ulinganishi, vifaa vilivyotumiwa kukusanya data vilikuwa hojaji, mahojiano, mtihani wa insha na uchunguzi darasani. Sampuli lengwa ilifikiwa kwa kutumia usampulishaji maksuudi na nasibu. Data ilichanganuliwa kitakwimu kwa kutumia uchanganuzi wa tarakimu na maelezo. Utafiti huu uligundua kuwa wanafunzi pamoja na walimu walipata shida kadhaa hali iliyoathiri kwa njia hasi ufunzaji na ujifunzaji wao. Licha ya kutambua umuhimu wa mwelekeo mseto katika ufunzaji, walimu wengi hawakutumia mbinu hii kufunza kutokana na ukosefu wa vifaa na nyenzo za kufunzia, uhaba wa muda, idadi kubwa ya wanafunzi madarasani mwao, uhaba wa walimu pamoja na ukosefu wa ujuzi maalum katika mbinu mseto. Pana haja kuu walimu waelekezwe vilivyo katika mbinu mwafaka za kufunzia, wanafunzi wahamasishwe kuhusu umuhimu wa somo hili, wachapishaji kuelekezwa vilivyo katika maswala yanayofunzwa katika kila kiwango na ukaguzi wa kina kufanywa ili kuondoa mambo yanayoweza kuwakanganya walimu na wanafunzi. Utafiti zaidi unaweza kufanywa katika vipengele vya Lugha na Fasihi ya Kiswahili ili kutambua changamoto zinazoshuhudiwa katika ufunzaji wao ili kuzitatua ipasaavyo

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Aggarwal, J. C. (2001). Principles, Methods and Techniques of Teaching. New Delhi: Vikas Publishing House Ltd.

Akaka, L.(Haijulikani). Changamoto zinazowakabili Walimu katika Ufundishaji wa Kiswahili katika shule za Upili Nchini Kenya. Research Article Kioo cha Lugha Juz 11.

Alharbi, A. H. (2015). Improving Students’ English Speaking Proficiency in Saudi Public Schools. International Journal of InstructionVol. 8, No. 1 Jan 2015.

Al Hosni, S. (2014). Speaking Difficulties Encountered by Young EFL Learners. International Journal on Studies in English Language and Literature (IJSELL), 2(6), 22-30.

Ambuko, B. S. (2008). Selection and use of media in teaching Kiswahili in secondary schools in Emuhaya District Kenya. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Maseno (Haijachapishwa).

Babusa, H. O. (2010) Uchanganuzi Linganuzi wa Mielekeo na Umilisi wa Lugha ya Kiswahili wa Wanafunzi Katika Mikoa ya Pwani na Nairobi Nchini Kenya.Tasnifu ya Uzamifu, Chuo Kikuu cha Kenyatta (Haijachapishwa).

Baumgartner, L. M., Lee, M. Y., Birden, S., & Flower, D. (2003). Adult Learning Theory: A Primer Center on Education and Training for Employment. College of Education, The Ohio University.

Birzer. M. L.(2003). The theory of andragogy applied to police training. Bradford, 26(1), 29.

Chacha, S. (2016). Uhusiano wa Mikakati ya Ufundishaji wa Fasihi ya Watoto ya Kiswahili na Umilisi wa Kusoma Katika Shule za Msingi, Kasarani, Kaunti ya Nairobi, Kenya. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Kenyatta.(Haijachapishwa).

Chika, P. O. (2012). The Extent of Students’ Responses in the Classroom. International Journal of Academic Research in Business and Social Sciences, 2 (1). www.hrmars.com/journals on 02/10/2015.

Dawning, J., Keating, T., & Bennett, K. (2005). Effective Reinforcement Techniques in Elementary Physical Education: The Key to Behavior Management. Physical Educator, Indianapolis, 62(3), 114.

Dewald, N. H. (1999). Web-based Library Instruction: What Is Good Pedagogy? Information Technology and Libraries, Chicago, 18(1), 26.

Earthman, G. I. (2004). Prioritization of 31 Criteria for School Building. Adequacy: American Civil Liberties Union Foundation of Maryland Assessed. <http://www.actomd.org.

Gathumbi, A.W., & Ssebbunga, C. M. (2005). Principles and Techniques in Language Teaching; a Text for Teachers Educator, Teachers and Pre-service Educators. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Gekombe, C. M. (2015). Factors affecting teaching and learning of Kiswahili comprehension in secondary schools in Wareng Sub-County Uasin Gishu County, Kenya (Doctoral dissertation, Moi University).

Gudu, B. O. (2015).Teaching Speaking Skills in English Language using Classroom Activities in Secondary School Level in Eldoret Municipality, Kenya. Journal of Education and Practice, 6(35).

Hakielimu “Citizens for Quality basic Education and democracy in Tanzania, program Strategy and Description January 2008 to December 2011,” 2008.

Hunsen, J. (1977). International Study of Achievent in Mathematics; A Comparison of twelve Countries. Johan Wiley and Sons.

Kang’ahi, M., Indoshi, F. C., Okwach, T. O., & Osodo, J. (2012). Teaching Styles and Learners’ Achievement in Kiswahili Language in Secondary Schools. International Journal of Academic Research in Progressive Education and Development, 1(3). www.hrmars.com/journals on 02/10/2015

Kavoi, J. M. (2019). Mielekeo ya Wanafunzi kuhusu Ufundishaji wa Stadi za Mawasiliano kwa Kiswahili Katika Taasisi za Kiufundi za Kitaifa Nchini Kenya. Tasnifu ya Uzamifu, Chuo Kikuu cha Rongo.

Kerlinger, N. F. (1978). Foundation of Behavioral Research. New Delhi, Surjeet Publicatio

K.I.E. (2002). Secondary Education Syllabus, Volume one. Nairobi: K.I.E.

Kimani J. N.(2015). Uhusiano wa Mbinu za Kufundisha Sarufi na Umilisi wa Mazungumzo ya Wanafunzi wa Sekondari, Kaunti ndogo ya Thika Magharibi, Kenya. Tasnifu ya Shahada ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Kenyatta, Kitivo cha Elimu (Haijachapishwa).

Kobia, J. M., & Ndiga, T. K. (2013). The Influence of Secondary School students’ Attitude towards implementation of Kiswahili Curriculum in Igembe South District, Meru County, Kenya. International Journal of Education and Research, 1(12).

Kolawole C.O.O. (2002). An Examination of the National Policy of Language Education in Nigeria and its Implication for the Teaching and Learning of English Language. Ibadan Journal of Education Studies.

Koross, R., & Murunga, F. (2017). Mbinu za Kufundishia Kiswahili katika K21. Eldoret, Utafiti foundation.

Liu, C. H., & Mathew, R. (2005). Vygotsky’s Philosophy: Constructivism and Its Critics Examined. International Education Journal, 6(3), 386-399.

Lumala, P. F. M. (2007). Towards the reader-text interactive approach to teaching imaginative texts: the case for the integrated English curriculum in Kenya (Doctoral dissertation, University of Nottingham).

Mbito, J. K. (2013). Challenges facing teachers and students in the process of teaching and learning Kiswahili in public secondary schools in Kiambu district in Kiambu County, Kenya. Unpublished research project submitted to Kenyatta University.

Melly, K. J. (2019). Matumizi ya vifaa vya kisasa katika ufundishaji na ujifunzaji wa Sarufi:Mfano wa Shule za Upili Kaunti ndogo ya Moiben, Kenya. Tasnifu ya uzamili, Chuo Kikuu cha Kibabii (Haijachapishwa).

Miima, F. A. (2014). Integration of Information Communication Technologies in teaching and learning of Kiswahili language in public secondary schools in Kakamega County, Kenya. Kenyatta University, Nairobi, Kenya

Mlay, N. (2010). The influence of the language of instruction on students' academic performance in secondary schools: A comparative study of urban and rural schools in Arusha-Tanzania (Master's thesis, University of Oslo).

Munawaroh, N. (2017). The Influence of Teaching Methods and Learning Environment to the students’ Learning Achievement of Craft and Entrepreneurship Subjects at Vocational High School. International Journal of Environmental and Science Education. Vol. 12 No.4. pg 665-678 .

Muruguru, S. K. P. (2000). Students’ performance in Kiswahili: A study of selected secondary Schools in Nakuru District, Kenya. Unpublished M. Phil. Thesis. Moi University, Eldoret, Kenya.

Mutsotso, S. na Nasongo, J. (2013). The adequacy of instructional materials and physical facilities and their effects on quality of teacher preparation in emerging private primary teacher training colleges in Bungoma County, Kenya. International Journal of Science and Research, 2(1), 403-408

Mwakarayz (2011). Athari za Lugha ya Kijita katika Kujifunza Kiswahili. Tasnifu ya Uzamili (M.A. Kswahili). Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. (Haijachapishwa).

Ng’ong’a (2002). An Assessment of University English Language Teacher Education in the light of Classroom needs. A case study of Maseno Unviversity. Unpublished PhD Thesis, Maseno University.

Njagi na wengine (2014). Effectiveness of Professional Development on English and Literature teachers in selected schools in Tharaka-Nithi and Meru County, Kenya. American International Journal of Contemporary Research Vol. 4. No. 8, 2014.

Njoroge, F. K., & Ndirangu. M. (2018). Influence of Selected Factors on the Performance of Kiswahili Language at KCSE in Secondary Schools in Njoro Sub- County, Nakuru County, Kenya. International Journal of Education and Research, 6(2). ISSN: 2411-5681 (www.ijern.com).

Ngugi wa Thiongo (2009). Remembering Africa. East African Educational Publishers. Nairobi, Kenya.

Nwanekezi, A. U. (2006). Effects of Individualistic Learning Strategy on Students’ Interest in Agricultural Science. Journal of Technology and Education in Nigeria, 11(1).

Odhiambo, (2012). Taskforce on the Realignment of the Education Sector to the Constitution of Kenya 2010: Towards a Globally Competitive Quality Education for Sustainable Development. Report of the Task Force- MOE, Kenya.

Ogero, J. O. (2012). Institution based factors influencing students’ performance in Kiswahili at KCSE in public schools in Sameta Division, Kisii County: Kenya. Unpublished Masters Thesis Kenyatta University.

Ogott, G. O., & Odera, F.Y. (2012) Integration of Media and Technology in Teaching and Learning Kiswahili Language in Secondary Schools in Siaya County, Kenya. International Journal of Information and Communication Technology Research, 2(10).

Oloo, M. A. (2018). Masuala yanayoathiri Ufunzaji na Ujifunzaji wa somo la Ufahamu katika shule za upili katika kaunti a Kisumu nchini Kenya. Unpublished Med Thesis Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro (MMUST)

Onyango, J. (2008). Second Language Learning. Unpublished module, Kenyatta University.

Opunde, S. (Haijulikani). Mwelekeo Mseto katika Ufundishaji wa Lugha ya Kiswahili.Karatasi ya utafiti. Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro (MMUST).(Haijachapishwa).

Owala, J. A. (2014). Mitazamo kuhusu Kiswahili miongoni mwa wazungumzaji wa Kijaluo: Kifani cha shule za msingi katika kaunti ya Migori. Tasnifu ya Uzamili: Chuo Kikuu Cha Nairobi.

Plotkin, H. (2003). We-intentionality: An essential element in understanding humanculture. Perspectives in Biology and Medicine.Chicago, 46(2). 283.

Roblyer, M.D. (2006). Intergrating Educational Technology in Teaching. (Sixth Edition).Pearson Education Limited. Edinburg Gate Harlow.www.pearsoned.co.uk.

Ruddell, R.B. (2002) Teaching Children to read and write: Becoming an Effective Literacy teacher (Third Edition). Boston:Allyn and Bacon.

Rutere, J. K. (2012). Effects of teacher related factors on implementation of integrated Kiswahili curriculum in public secondary schools in Nkuene Division, Imenti South district, Kenya (Doctoral dissertation, University of Nairobi, Kenya).

Schultz, A. & Schultz, F. (1987). A Neural Substrate of Predication and Reward. Science.275:1593-1598.

Simiyu, M.N. (2013). Factors Affecting Academic Performance in Secondary Schools in Kenya: A case of Trans-Nzoia West District. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Moi (Haijachapishwa).

Tume ya Koech (1999). Report of the Commission of Inquiry on the Education system in Kenya. Nairobi; Government Printer Kenya.

Wambua na wengine (2019).Teaching and Learning Resources in Kiswahili in Secondary Schools. Journal of Pedagogical Sociology and Psychology Volume 1, Issue 2, 2019 pg 64-79 www.j-psp.com

Wanyama, P.O. (2007). Silabasi Mpya: I Wapi Tofauti? Education Insight, 4(2).

Tarehe ya Uchapishaji
26 October, 2023
Jinsi ya Kunukuu
Okeyo, L., Kimemia, J., & Ndethiu, S. (2023). Uchunguzi wa Changamoto za Walimu na Wanafunzi wa Kiswahili katika Shule za Upili Nchini Kenya. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 6(1), 412-434. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1538