Utathmini wa Ujenzi wa Motifu ya Mgogoro wa Ardhi Kupitia Wahusika: Mfano Kutoka Chozi la Heri na Kovu Moyoni

  • Mercy Karimi Nthia Chuo Kikuu cha Mlima Kenya
  • Onesmus Gitonga Ntiba, PhD Chuo Kikuu cha Mlima Kenya
Keywords: Ardhi, Migogoro, Motifu, Uhalisia na Wahusika
Sambaza Makala:

Ikisiri

Suala la ardhi limekuwa nyeti tangu jadi. Wahusika hutumiwa na wasanii kubainisha suala hili. Tafiti za awali zilijikita katika motifu ya safari, siri na maisha ya dunia. Hata hivyo, hakuna utafiti umefanywa kutathmini ujenzi wa motifu ya mgogoro wa ardhi kupitia wahusika. Makala hii imelenga kuziba pengo hili. Utafiti huu ni kutathmini ujenzi wa motifu ya suala la mgogoro wa ardhi kupitia wahusika; mfano kutoka Chozi la Heri na Kovu Moyoni. Motifu hii ni kurudiwarudiwa kwa suala la mgogoro wa ardhi baina ya wahusika katika matini teule. Makala hii iliongozwa na nadharia mbili; Nadharia ya Uhalisia wa Kijamaa na Nadharia ya Sosholojia ya Fasihi. Nadharia ya Uhalisia wa Kijamaa iliwaongoza watafiti kuweza kubainisha suala la ardhi kama lilivyoangaziwa na waandishi katika uhalisia wake. Hata hivyo, nadharia hii ilipungukiwa kubainisha jinsi matabaka katika jamii huendeleza suala la ardhi. Nadharia iliyofidia pengo hili ni Sosholojia ya Fasihi. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani ambapo matini teule ziliteuliwa kimaksudi. Mpango wa kimaelezo ulitumika kuchanganua na kuwasilisha matokeo. Matokeo ya makala hii ni kuwa motifu ya mgogoro wa ardhi imekuzwa kupitia kwa wahusika antagonisti, protagonisti, tuli na bui. Kwa hivyo, utachangia katika uhakiki wa kazi za baadaye za nathari za fasihi ya Kiswahili. Aidha, walimu na wanafunzi wataelewa namna wahusika hujengwa. Makala hii ilipendekeza tafiti za baadaye zifanywe kutathmini motifu ya wahusika katika sekta ya uchumi na siasa.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Barasa, N. (1993). Of Ethnicity and Leadership in Kenya. The Daily Nation, 3rd April, Nairobi.

Castelli, F. (2018). Drivers of migration: why do people move?. Journal of travel medicine, 25(1), tay040.

Chome, N. (2020). Land, livelihoods and belonging: negotiating change and anticipating LAPSSET in Kenya’s Lamu county. Journal of Eastern African Studies, 14(2), 310-331.

Cuddon, A. (2013). A Dictionary of Literary Terms and Literary Theory. Wiley: Blackwel

Ertiftik, H., & Zengin, M. (2015). Effects of increasing rates of potassium and magnesium fertilizers on the nutrient contents of sunflower leaf. Selcuk Journal of Agriculture and Food Sciences, 29(2).

Gambrah, A. (2002), “Improving Land Transfer Procedures in Ghana”, Journal of Kwame Nkrumah University of Science and Technology, Kumasi, Vol. 22, pp. 22-24.

García, N. (2016). Moral emotions, antiheroes and the limits of allegiance. In Emotions in contemporary TV series (pp. 52-70). Palgrave Macmillan, London.Global land programme.

Golla, B. (2021). Agricultural production system in arid and semi-arid regions. International Journal of Agricultural Science and Food Technology, 7, 234-244.

Gyamera, E., Duncan, E. E., Kuma, J. S. Y., & Arko-Adjei, A. (2018). Land acquisition in Ghana; Dealing with the challenges and the way forward. Journal of Agricultural Economics, Extension and Rural Development, 6(1), 664-672.

Habwe, J. (2014). Kovu Moyoni. Bookmark Africa.

Karnawat, M., Trivedi, S. K., Nagar, R., & Nagar, D. (2020). Role of monsoon in Indian agriculture. Biotica Research Today, 2(10), 1019-1021.

LaFrancesca, Joanna. "Land grabs and implications on food sovereignty and social justice in Senegal." (2013).

Makunike, B. (2014). Land reform and poverty alleviation in Mashonaland East, Zimbabwe (Doctoral dissertation, University of the Free State).

Matei. K. (2017) Chozi la Heri. One Planent & Media Services Limited.

Morgan, D. O. (1995). Principles of CDK regulation. Nature, 374(6518), 131-134.

Mugenda, O. M., & Mugenda, A. G. (1999). Research methods: Quantitative and qualitative approaches. Acts press.

Mulokozi, M. (1996). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili: Dar es Salaam.

Nyiri, K. (2014). The impact of ethnic conflict on economic development: the case of post-election violence in Kenya, 2007-2014 (Doctoral dissertation, University of Nairobi).

Ryan-Collins, J. (2021). Breaking the housing–finance cycle: Macroeconomic policy reforms for more affordable homes. Environment and Planning A: Economy and Space, 53(3), 480-502.

Sarah. S. (2011) AL-Shabaab makes it hard for internally displaced Somalis to access aid-One

Saraswati, K. P. (2019). Analysis of Characters and Characterization in the Compilation of Malay Poetry “Mirror. Shahada ya Uzamili (Haijachapishwa), Chuo Kikuu cha Negeri Semarang.

Scott, G. (2015). Migogoro ya Kisaikolojia katika Riwaya ya Mkamandume na Unaitwa Nani. Chuo Kikuu cha Kenyatta, Kenya.

Taifa la Kenya. (2010). Katiba ya Kenya. Nairobi: Government Printer.

Wamitila, K. W. (2002). Uhakiki WA fasihi.

Wamitila, W. (2003). Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia, Nairobi; Focus Publication Ltd.

Wien, N. R. (1916). Karl Marx und Friedrich Engels über die Polenfrage. Archiv für die Geschichte des Sozialismus und der Arbeiterbewegung, (6), 175.

Wizara ya Ardhi, (2009). Sessional paper No.3 of 2009. Nairobi: Government Printers.

Zhang, K., Yu, Z., Li, X., Zhou, W., & Zhang, D. (2007). Land use change and land degradation in China from 1991 to 2001. Land Degradation & Development, 18(2), 209-219.

Tarehe ya Uchapishaji
22 December, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Nthia, M., & Ntiba, O. (2022). Utathmini wa Ujenzi wa Motifu ya Mgogoro wa Ardhi Kupitia Wahusika: Mfano Kutoka Chozi la Heri na Kovu Moyoni. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(2), 142-154. https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.1019