Utu wa Wahusika Viumbe wa Kiuhalisiajabu: Mtazamo wa Mwandishi Said Ahmed Mohamed

  • Peres Akello Obondo Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaramogi Oginga Odinga
  • Juliet Akinyi Jagero, PhD Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaramogi Oginga Odinga
  • Naomi Nzilani Musembi, PhD Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaramogi Oginga Odinga
Keywords: Utu, Uhalisiajabu, Riwaya Mpya na Mhusika
Sambaza Makala:

Ikisiri

Utu ni sifa mojawapo muhimu katika mahusiano mazuri maishani mwa binadamu. Utu huhusisha wema. Utu ni sifa ambayo huhusishwa na wahusika mbalimbali katika dunia halisi na hata kwenye dunia ya fasihi. Wahusika ni muhimu katika fasihi kwa vile kupitia kwao, mwandishi huweza kupitisha ujumbe aliokusudia kwa wasomaji. Wahusika huwa wa aina mbalimbali wakiwemo wahusika wa kiuhalisiajabu ambao pia huchangia katika kupitisha ujumbe wa mwandishi sawia na wahusika wa kihalisia. Tafiti za awali zimewasawiri wahusika binadamu wakionyesha utu kwa sababu ni sifa muhimu anayopaswa kuwa nayo binadamu. Hata hivyo, waandishi wa Kiswahili akiwemo Said A. Mohamed wamesawiri wahusika wa kiuhalisiajabu wakionyesha utu kwa viumbe wengine. Huu ni mtindo ambao umeanza kutumiwa katika riwaya mpya na waandishi wa fasihi ya Kiswahili. Hivyo basi, utafiti huu ulichanganua kiuhakikifu wahusika viumbe wa kiuhalisiajabu katika riwaya teule za Said A. Mohamed ili kudhihirisha kwamba hata viumbe wasio binadamu huwa na sifa ya kibinadamu ya utu. Lengo mahususi lililoongoza utafiti huu lilikuwa kufafanua jinsi viumbe wa kiuhalisiajabu wanavyodhihirisha utu katika riwaya za Said A. Mohamed. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya kiuhalisiajabu kama inavyofafanuliwa na Zamora na Wendy (1995). Nadharia hii hueleza matukio katika hali ya kutisha, kushangaza na kuogofya kwa kuziwasilisha kana kwamba ni hali ya kawaida. Eneo la utafiti likiwa fasihi ya Kiswahili, utanzu wa Riwaya. Sampuli ya kimakusudi ilitumika kuteua riwaya tatu za Said A. Mohamed hususan: Babu Alipofufuka (2001), Dunia Yao (2006) na Nyuso za Mwanamke (2010). Data ilikusanywa kutokana na kusoma riwaya hizo tatu zilizoteuliwa na kudondoa sehemu zinazolingana na lengo la utafiti. Data ilidondolewa, ikanukuliwa, ikapangwa kisha kuchanganuliwa. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa kwa kweli viumbe wa kiuhalisiajabu wana sifa za utu kama upendo, ukarimu, kusamehe miongoni mwa mengine.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Chepkoech, T. (2018) “Usawiri wa maudhui yenye kufunza wanafunzi wa vyuo maadili mema: Tathmini ya Alidhani Kapata na Damu Nyeusi.” (Tasnifu ya Uzamili). Chuo Kikuu cha Nairobi.

Cornevale, J. M. (2006). International Journal of ethics, 16 (4), 424-429.

Cooper, B. (1998). Magical Realism in West African Fiction. New York: Routledge.

Danow, K. (1995). The Spirit of the Carnival; Magical Realism and the Grotesque. Kentucky University of Kentucky Press.

Gilbert, E. (2010). Magical Realism and Visionary Materialism in Okri and Blake. Dreams of Freedom, 15 (1), 18-32.

Habwe, J. (1987). “Euphrase Kezilahabi: Mwandishi aliyekata tamaa.” Unpublished BA dissertation. University of Nairobi.

Mbatia, M. (2002). Kamusi ya Fasihi. Nairobi: Standard Textbooks.

Mbiti, J. S. (1980) The Encounter of Christian Faith and African Religion. Retrieved 25/08/2019 On-line version published by Religion Online.

Mbiti, J. S. (1990). African Religion and Philosophy. Nairobi. Heinemann.

Mohamed, S. A. (2001). Babu Alipofufuka. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Mohamed S. A. (2006). Dunia Yao. Nairobi: Oxford University Press.

Mohamed, S. A. (2010). Nyuso za Mwanamke. Nairobi: Oxford University Press.

Msokile, M. (1999). Misingi ya Hadithi Fupi. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.

Mwangi, J. (2013). Uhalisia na Uhalisiajabu katika Riwaya Mpya. (Tasnifu ya Uzamili). Chuo Kikuu cha Kenyatta, Nairobi. (Haijachapishwa)

Njogu, K. & Chimerah, R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi Nadharia na Mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation Ltd

Oruka H. O. (1990). Ethics, Nairobi: Nairobi University.

Pietersen, H. J. (2005). Western Humanism, African Humanism and Work Organization. SA Journal of Industrial Psychology, 31(3), 54-61.

Samba, R. (2018) “Uhusika katika mashairi ya Kiswahili: Malenga wa Vumba, Kichomi na Utenzi wa Fumo Liyongo.” (Tasnnifu ya Uzamili) Chuo Kikuu cha Maseno, Kisumu.

Tutu, D. (2004). God has a Dream: A Vision of Hope for Our Time: New York Doubleday.

Vutagwa (2013). “Sifa za uhalisiajabu katika Utenzi wa Mwana Fatuma.” ( Tasnifu ya Uzamili). Chuo Kikuu cha Kenyatta, Nairobi.

Wamitila, K. (2003). Kamusi ya Fasihi Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Publications Ltd.

Wamitila, K. W. (2010). Kichocheo cha Fasihi: Simulizi na Andishi (chapa ya tano). Nairobi: Focus Publicationa Ltd.

Wanjiru, M. J. (2013). Uhalisia na Uhalisiajabu katika Riwaya za Babu Alipofufuka na Watu wa Gehhena. (Tasnifu ya Uzamili). Chuo Kikuu cha Kenyatta, Nairobi.

Zamora, L. P. & Wendy, B. S. (1995). Magical Realism Theory, History, Community. London: Duke University Press.

Tarehe ya Uchapishaji
26 December, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Obondo, P., Jagero, J., & Musembi, N. (2022). Utu wa Wahusika Viumbe wa Kiuhalisiajabu: Mtazamo wa Mwandishi Said Ahmed Mohamed. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(2), 131-141. https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.1014