Tathmini ya Taashira za Wahusika Katika Tamthilia ya Sudana

  • Antony Kago Waithiru Chuo Kikuu cha Laikipia
Keywords: Taashira, Umitindo, Wahusika, Mbinu, Ukoloni mamboleo
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala haya yanahusu uhakiki wa taashira za wahusika katika tamthilia ya Sudana. Makala haya yalinuia kubaini wahusika wanaosawiriwa kitaashira na waandishi. Pia, yalinuia kujadili namna waandishi walivyowatumia wahusika kitaashira kuwasilisha ujumbe lengwa. Makala haya yaliyojikita katika nadharia ya umitindo yanadhihirisha kuwa taashira imetumika katika tamthilia husika kama mbinu fiche na kwepi ya kuikosoa na kuielekeza jamii. Baadhi ya masuala ambayo yameangazia ni pamoja na viongozi dhalimu, ubaguzi, ukabila, tamaa na ubinafsi. Kadhalika, yanaeleza kuwa taashira imetumika vyema katika tamthilia hii madhali imeauni waandishi kuepuka uwezekano wa kusawiri masuala yanayokumba jamii paruwanja, jambo ambalo lingenyima kazi yenyewe mnato. Badala yake, kazi yenyewe imeonyesha kuwa waandishi walifinyanga lugha na kuwasawiri wahusika wa kawaida kwa njia mpya na ya kutendesa kupitia taashira. Yanaonyesha tadi na inda zinazotumiwa na baadhi ya watawala katika mataifa yanayoinuka kiuchumi kujinufaisha kibinafsi pamoja na vikaragosi wao. Isitoshe, makala haya yamedhihirisha jinsi viongozi wa mataifa hayo hudhibitiwa na watawala katika mataifa yaliyoinuka kiuchumi na kusababisha ulofa wa wananchi katika mahusiano yanayofichika katika ukoloni mamboleo. Yaliongozwa na nguzo kuu za nadharia ya umitindo. Nadharia ya umitindo ina nguzo kadhaa muhimu lakini makala haya yaliongozwa na nguzo tatu kuu ambazo ni ile ya kiwango cha umbo, ya kiwango cha kisemantiki, pamoja na ile ya mazungumzo na mbinu za uwasilishaji usemi na mawazo baina ya wahusika

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

BAKITA (2016). Kamusi Kuu ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers.

Coombes, H. (1953). Literature and Criticism. London: Penguin books.

Hamad, M.A. (2017).“Muundo wa Lugha Katika Mashairi ya Watungaji Wateule wa Zanzibar”. Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, Phd Thesis (Published).

King’ora, M. N. (2014). “Utendaji Katika Tamthilia za Sudana na Kimya Kimya Kimya”. Tasnifu ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Nairobi (Haijachapishwa).

Indangasi, H. (1988). Stylistics. Nairobi. Nairobi University Press.

Leech, G. (2008). (1st ed.). Language in Literature: Style and Foregrounding. London:Routledge.

Mazrui, A. M. na Njogu, K. (2006). Sudana. Nairobi: Longhorn Publishers.

Madumula, J. S. (2009). Riwaya ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.

Mbuvi, F. K. (2014). Mwongozo wa Kidagaa Kimemwozea ya Ken Walibora. Spotlight Publishers (EA) Limited. Nairobi.

Mdee, S., Shafi, A., Kiango, J., & Njogu, K. (2009).Kamusi Kamili ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers (K) Ltd.

Nauta, D. Jr. (1972). The Meaning of Information. The Haque: Mouton.

Waithiru, A. K., Nabea, W. K., na Onyango, J. O. (2021). Uamilifu wa Taashira Katika Tamthilia za Zilizala na Sudana Mwanga wa Lugha Jarida la Idara ya Kiswahili na Lugha Nyingine za Kiafrika Chuo Kikuu cha Moi, Juzuu la 6 Na. 1, 43-54. ISSN 2412-6993

Waithiru, A. K. (2022a). Symbols of the Sentient House of Usher: An Ecocritic Approach East African Journal of Education Studies, 5(2), 369-376. https://doi.org/10.37284/eajes.5.2.812

Waithiru, A. K. (2022b). An Evaluation of Environmental Symbolism used in Children Literature: Case Study of Kijiji Cha Ukame and Mazingira Maridadi East African Journal of Education Studies, 5(3), 1-10. https://doi.org/10.37284/eajes.5.3.846

Wamitila, K. W. (2003). Kamusi ya Fasihi; Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Publications Ltd.

Wilson, E. (1998). The Theater Experience. New York: The McGraw-Hill Companies Inc.

Tarehe ya Uchapishaji
16 December, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Waithiru, A. (2022). Tathmini ya Taashira za Wahusika Katika Tamthilia ya Sudana. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(2), 124-130. https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.1010