Sayansi katika Tamthiliya ya Kiswahili: Uchunguzi Kifani wa Tamthiliya ya Orodha

  • Deogratius Francis Mkawe Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge
  • Mohamed Omary Maguo, PhD Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Keywords: Sayansi, Mbinu ya Utatuzi wa Tatizo, Mtindo wa Usayansi, Orodha, Mwingiliano matini, Mtindo wa Uhakiki, Ujaribizi na Taarifu
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inahusu uhakiki wa Sayansi katika Tamthiliya ya Kiswahili, mifano kutoka tamthiliya ya Orodha. Ni moja ya makala chache katika mfululizo wa uchambuzi wa masuala ya kisayansi katika Tamthiliya na Fasihi ya Kiswahili kwa ujumla. Lengo la makala hii ya utafiti ni kueleza sifa fumbatwa za kisayansi zitakazopelekea kuundwa kwa mtindo mpya wa uhakiki. Mitindo ya uhalisia, uhistoria, sosiolojia, umuundo, saikolojia, falsafa, uhalisia mazingaombwe kutaja chache, imetumika kwa muda mrefu katika ulimwengu wa uhakiki. Nadharia ya mwingiliano matini imeongoza uchambuzi huu hususani kupitia usemezano wa matini. Maelezo ya ufafanuzi wa masuala ya sayansi kutoka katika taaluma za fizikia, baiolojia na kemia yalitumika kumuongoza mwandishi kuweka alama na kudondoa nukuu zilizofumbata sayansi. Data kuhusu masuala ya sayansi kutoka taaluma za sayansi kavu na taarifu ya tamthiliya zilikusanywa kupitia mbinu ya usomaji makini. Matokeo yameonesha kuwa, juhudi za kuisaka orodha au barua iliyoelezwa na mtunzi, mfasiri na wahakiki wa tamthiliya kuwa ya kuchekesha ni ya kisayansi. Wahusika Padri James, Bw. Chaka Ecko, Salimu, Juma na Kitunda wanaisaka orodha kwa kutumia mbinu ya sayansi ya utatuzi wa tatizo. Wahusika hawa wanahaha kutatua tatizo la kuipata orodha iliyoandikwa na Furaha, binti waliyetembea naye kimapenzi. Msako unatokana na hofu yao kubwa ya kutajwa kwa majina kuwa walimuambukiza ugonjwa wa UKIMWI. Mwanasayansi hufanya uchunguzi hatua kwa hatua pindi anapokabiliwa na tatizo ili kulitatua, hivyo Padri James, Bw. Chaka Ecko, Salimu, Bw. Juma na Kitunda ni wanasayansi. Sayansi hii haitajwi wazi na wahusika, mwandishi, mfasiri au wachambuzi tangulizi. Tamthiliya hii pia haikupewa sifa ya kuwa na sayansi, hadhi inayopewa na makala hii. Makala imeuweka katika ujaribizi uchambuzi wa mtindo wa usayansi kupitia mbinu ya sayansi ya utatuzi wa tatizo. Tabia hii jaribizi ya uchambuzi inasaidia wasomaji kuelewa wahusika wanavyotatua matatizo binafsi na, au jamii ambayo kwa kiasi kikubwa ni malengo ya uandishi wa kazi ya fasihi.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Eddington, D. (2008). Linguistic and the Scientific Method. Katika Southwest Journal of Linguistics, Volume 27, number 2. https://www.researchgate.net/publication/228848641_Linguistics_and_the_scientific_method

Haberer, A. (2007). Intertextuality in theory and practice. Katika Journal of Literatura, 49(5), 54-67.https://www.researchgate.net/publication/330572602_Intertextuality_in_Theory_and_Practice

Kiango, S. D. (2006, mfasiri). Orodha. Tamthiliya ya Kitanzania. Macmillan Aidan Ltd, Dar es Salaam, Tanzania.

Kumar, V. (2012). Mathematics is Science: A Topic Revisited in Context of FCS of India. Katika Journal of ijmecs, 2012, 6, 17-26. https://www.researchgate.net/publication/272852982

Mhilu, G., Nyangwine, N. na Kanyuma, Y. (2013). Tahakiki vitabu teule vya fasihi kidato cha 3 na 4: nadharia, uhakiki na maswali. Nyambari Nyangwine Publisher, Dar-es-Salaam.

Okpewho, I. (1992). African oral literature: Backgrounds, character, and continuity. Bloomington and Indianapolis:Indiana University Press.

Madumulla, J. S. (2009). Riwaya ya kiswahili: Nadharia, historia na misingi ya uchambuzi. Dar es Salaam: Mture Educational Publishers Limited.

Mucee, F. M., King’ei, G. K. na Wafula, K. W. (2018). Mbinu ya Ubunilizi wa Kisayansi katika Riwaya: Bina-Adamu (K. W. Wamitila) NA Babu Alipofufuka (S. A. Mohamed). Katika International Academic Journal of Social Sciences and Education / Speciala Issue 1, pp. 1 – 38. https://www.iajournals.org/articles/iajsse_si1_1_38.pdf

Mulokozi, M. M. (1996). Utangulizi wa fasihi ya kiswahili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania: -.

Nichols, A. J. na Stephens, A. H. (2013). The Scientifc Method and the Creative Process: Implications for the K-6 Classroom. Katika Journal for Learning throgh the Arts. 9(1). https://files.eric.ed.gov/fulltext/EJ1018325

Passer, M. W. na Smith, R. E. (2008). Psychology: The study of the mind and behavior. New York: McGraw-Hill Education.

Roberts, A. (2002). Science fiction: The new critical idiom (2nd ed.). London and New York: Routlage.

Singh, Y. K. (2006). Fundamental of research methodology and statistics. New Delhi, New Age International Publishers

Wafula, R. M. na Njogu, K. (2007). Nadharia za uhakiki wa fasihi. Nairobi, the Jomo Kenyata Foundation.-

Tarehe ya Uchapishaji
13 December, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Mkawe, D., & Maguo, M. (2022). Sayansi katika Tamthiliya ya Kiswahili: Uchunguzi Kifani wa Tamthiliya ya Orodha. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(2), 100-109. https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.1003