Maudhui Katika Nyimbo za Tohara Zilizodenguliwa na Nyimbo za Dini za Kiigembe katika Kuafikia Maendeleo Endelevu kwa Waigembe

  • Eliud Miriti Josphat Chuo Kikuu cha Chuka
  • Ntiba Gitonga, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
  • Dorcas Musyimi, PhD Chuo Kikuu cha Chuka
Keywords: Udenguzi, Kiigembe, Nyiso, Nyidini
Sambaza Makala:

Ikisiri

Waigembe wana utamaduni ambao unafungamana na nyimbo ambazo zinaimbwa katika hafla tofauti tofauti. Nyimbo za tohara pamoja na nyimbo za kidini za Kikristo ni baadhi ya zile zinaimbwa. Nyimbo za tohara zinaimbwa wakati wa kutahiri wavulana na za kidini wakati wa shughuli za kidini ya Kikristo. Hata hivyo, hatua ya waimbaji wa nyimbo za dini ya Kikristo kubadilisha nyimbo za tohara kimaudhui, kimtindo na kiutendakazi ili kuzitumia upya katika mazingira ya kidini ili kusaidia katika maenezi ya injili ya Kikristo kwa wengi na kutumika katika hafla zingine za kijamii kando na tohara ni jambo ambalo ni mpya katika jamii ya Waigembe. Hiki ndicho kiliwachochea watafiti kutafiti udenguzi wa nyimbo za tohara za Waigembe na nyimbo za dini ya Kikristo ili kuweza kutumika katika hafla tofauti kando na tohara.   Makala haya yalilenga kubainisha maudhui ambayo nyimbo za tohara zilizodenguliwa na nyimbo za dini ya Kikristo huwa nayo katika jamii ya Waigembe. Watafiti waliongozwa na nadharia ya udenguzi. Data ya nyimbo kumi na nane imetumika katika makala haya. Awamu tatu ambazo nyimbo hizo hufuata zilichanganuliwa na kuwasilisha maudhui kwa njia ya maelezo. Makala haya yanachangia katika kuongeza maarifa ya kiutafiti kuhusu nyimbo zilizodenguliwa za tohara za Kiigembe, pamoja na kuhifadhi fasihi simulizi ya Kiafrika ili itumike na vizazi vijavyo katika kuafikia maendeleo endelevu.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Chesaina, C. (1997). The song as a medium of Expression of gender solidarity for Embu and Mbeere Women; In contesting social death; Essays on Gender and culture. Nairobi. K.O.L.A.

Daniel, N. (1986). Mikarire na mituurire ya Amiiru: Nteto chia bajuju beetu. Nairobi: East Africa Educational Publishers.

Derrida, J. (1967). Of Grammatology. Trans. Gayatri Spivak.Baltimore: Johns Hopkins.

Elizabeth, W (2018). Mielekeo na mtindo wa Shafi Adam Shafi katika riwaya za Kuli na Haini (Tasnifu ya uzamili isiyochapishwa) Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Evaline, K. (2015). Maudhui ya Uadilifu katika Nyimbo za Joseph Ngala, (Tasnifu ya uzamili isiyochapishwa) Chuo Kikuu Cha Kenyatta.

Finnegan, R. (1970). Oral literature in Africa. London. Oxford University Press.

Kanake, A. K. (2001). Changes and continuity in the practice of clito A case study of the Tharaka of Meru East. M.A Thesis, Kenyatta University.

Kitundu, A. (2011). Athari za Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwenye fasihi Simulizi Nyimbo za ibada ya dini ya Kikristo Tanzania.

Kobia, J. (2008). Taswira za kiuana katika nyimbo za Tohara za wanaume miongoni mwa Waigembe, (Tasnifu ya uzamifu isiyochapishwa) Chuo kikuu cha Kenyatta.

Mburu, J. (2014). Fani katika nyimbo teule za Anastacia Mukabwa, (Tasnifu ya uzamili isiyochapishwa) Chuo Kikuu Cha Nairobi.

M'Imanyara, A. (1992). The Restatement of the Bantu origin and Meru History. Nairobi, Longman.

Mutwiri, G. (2005). Mitazamo ya utendakazi wa nyiso katika jamii ya Watigania, (Tasnifu ya uzamili isiyochapishwa) Chuo Kikuu Cha Kenyatta.

Ngugi, P. (2000). Nafasi ya Muziki uliopendwa katika Fasihi ya Kiswahili. AAP64. Swahili Forum VII.

Njiru, E. (1981). Indigenous Education as practiced by the Ameru with special reference to circumcision ceremonies. M. A. Thesis, University of Nairobi.

Njue, M. (2016). Usawiri wa mwanamume katika methali za Kimeru nchini Kanya, (Tasnifu ya uzamili isiyochapishwa) Chuo Kikuu cha Pwani.

Nyaga, D. (1986). Mikarire na miturire ya Amiru. Nteto cia Bajuju Betu. Nairobi. EAPP.

Regina, W. W. (2009). Mitindo katika nyimbo za Tohara za jamii ya Wakamba wa Masaku, (Tasnifu ya uzamili isiyochapishwa) Chuo kikuu cha Kenyatta.

Wambua, S. (2001). Mitindo na Matumizi ya Lugha katika Nyimbo za Kakai Kilonzo, (Tasnifu ya uzamili isiyochapishwa) Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Tarehe ya Uchapishaji
29 Septemba, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Josphat, E., Gitonga, N., & Musyimi, D. (2022). Maudhui Katika Nyimbo za Tohara Zilizodenguliwa na Nyimbo za Dini za Kiigembe katika Kuafikia Maendeleo Endelevu kwa Waigembe. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 273-287. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.813