Mchango wa Mashairi ya Kiganda katika Kuendeleza Muundo wa Ushairi wa Kiswahili Kupitia Ufunzaji na Ujifunzaji

  • Edwine Atukunda Chuo Kikuu cha Maseno
  • Owen McOnyango, PhD Chuo Kikuu cha Maseno
  • Deborah Amukowa, PhD Chuo Kikuu cha Maseno
Keywords: Ushairi, Muundo, Kiganda, Mchango, Ufunzaji
Sambaza Makala:

Ikisiri

Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa vizuri katika mtihani wa kitaifa. Upande wa Kiswahili, kuna ugumu katika ujifunzaji wa ushairi wa Kiswahili na ugumu huu umesababisha matokeo mabaya katika mtihani wa kitaifa katika somo la ushairi wa Kiswahili nchini Uganda. Wanafunzi hawa wanasomea katika mandhari sawa, kwa hivyo utendaji wao kwenye mtihani unastahili kuwa sawa. Kwa hivyo, makala hii imechanganua mchango wa ushairi wa Kiganda katika maendeleo ya ushairi wa Kiswahili kimuundo. Madhumuni ya makala hii ni: Kufafanua jinsi muundo wa ushairi wa Kiganda unavyoweza kuendeleza muundo wa ushairi wa Kiswahili kupitia ufunzaji na ujifunzaji. Kudadavua jinsi muundo wa ushairi wa Kiswahili unavyoweza kuvunja mipaka iliyowekwa na kupanuka. Makala hii imeongozwa na nadharia ya umuundo ambayo iliasisiwa na Ferdinanda De Saussure (1909) Mihimili ya nadharia hii ni fasihi inastahili kuchunguzwa kama muundo mmoja uliojengwa kwa vipengele tofauti vinavyoshirikiana kukiunda kitu kizima. Pili, huchunguza vipengele mbalimbali vya mfumo wa fasihi kwa kuchunguza jinsi vinavyohusiana na kuchangiana katika kukamilisha kazi husika. Tatu, hulenga maana katika matini ya kifasihi na kupuuza maswala mengine ya nje kama muktadha. Mashairi yalikusanywa kutoka diwani mbili za Kiswahili na mbili za Kiganda. Mashairi 60 yalikusanywa; yaani, 30 ya Kiganda na 30 ya Kiswahili na 15 yalichaguliwa kutoka kila diwani kwa kutumia uteuzi nasibu. Mashairi yatatolewa kwenye diwani za Kiswahili; “Malenga wa ziwa kuu” na “Malenga wa karne moja” na za Kiganda; “Ab’Oluganda ab’Enda emu” na “Balya n’ensekeezi”. Kundi lengwa ni walimu watano wa Kiganda na watano wa Kiswahili ambao walichaguliwa kimakusudi na kushiriki katika uchambuzi ambao uliandamana na maoni yao kuhusu ujifunzaji na ufunzaji wa ushairi. Makala hii ilifafanua jinsi mwalimu wa ushairi wa Kiswahili anavyoweza kuhamisha maarifa kutoka ushairi wa Kiganda hadi wa Kiswahili.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abdilatif A. (1973) sauti ya dhiki. Nairobi; oxford press.

Chraghdin & Ahmed S. (1989) Malenga Wa Karne Moja. Nairobi; Longman Kenya.

Culler J. (1975) structuralist poetics; structuralism, linguistics, and the study of literature. Wisconsin; University of Wisconsin press.

Fokkema D.W. (1995) STRUCTURALISM; its rise influence and aftermath. London; Cambridge university press.

Hassan, S. F. (2013). “Analysing the Language of Poetry from a Perspective of Linguistics”. International Journal of English and Education. 2 (2): 394-405.

Hugo E. S.B (2003) Aboluganda Abendaemu. Kampala; Fountain publishers.

Kihore, Y. M., Massamba, D. P. B., na Msanjila, Y. P. (2003). Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA) Sekondari na Vyuo. Dar es salaam: TUKI.

Masagazi, K. (1992) balya ne’ensekeezi (abayiiya abajja). Kampala;Luganda consultancy bearau.

Massamba, D. P. B., Kihore, Y. M. na Hokororo, J. I. (2009). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA) Sekondari na Vyuo. Dar es salaam: TUKI.

Massamba, D. P. B., Kihore, Y. M. na Msanjila, Y. P. (2004). Fonolojia ya Kiswahili Sanifu (FOKISA) Sekondari na Vyuo. Dar es salaam: TUKI.

Mnyampala, M. (1970). Diwani ya Mnyampala. Nairobi: East African Literature Bureau.

Mnyampala, Mathias. (1965). Diwani ya Mnyampala. Dar es Salaam: East African Literature Bureau.

Robert, S. (1958). “Hotuba juu ya Ushairi”. Journal of the East African Swahili Committee. 28 (1): 37-42.

Saussure F.D (1909) Diuxieme cours de lingustique generale. D’pres les ca hiers. Newyork; Oxford press.

Saussure F.D (1910) Notes Preparotoires Pour Le Cours De Linguistique Generale. London; Oxford Press.

Saussure, F. (1959). A Course in General Linguistics. New York: Philosophical Library.

Schole R. (1974) structuralism in literature. London; oxford university press.

Shaaban R. (2003) barua za shaaban Robert, 1931-1958. Dar-es-salaam; TUKI

Wallah B.W (1988) Malenga Wa Ziwa Kuu. Nairobi; East African Educational Publishers.

Wamitila K.W (2002) Uhakiki Wa Fasihi; Misingi Na Vipengele Vyake. Nairobi; Phoenix Publisher.

Tarehe ya Uchapishaji
27 June, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Atukunda, E., McOnyango, O., & Amukowa, D. (2022). Mchango wa Mashairi ya Kiganda katika Kuendeleza Muundo wa Ushairi wa Kiswahili Kupitia Ufunzaji na Ujifunzaji. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 171-182. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.724