Propaganda Kama Mkakati wa Kuhimili Hejemonia: Mfano wa Dharau ya Ini, Msimu wa Vipepeo, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi

  • Harrison Onyango Ogutu, PhD Chuo Kikuu cha Laikipia
Keywords: Propaganda, Hejemonia, Hejemonia ya Kisiasa, Hejemonia ya Kijamii, Hejemonia ya Kiuchumi, Kuhimili Hejemonia
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii imechunguza suala la propaganda kama mkakati wa kuhimili hejemonia katika riwaya teule za Kiswahili. Mtafiti amejadili namna propaganda inatumiwa kudumisha na kuimarisha utawala wa viongozi mintarafu ya riwaya teule. Ili kutimiza lengo lake, mtafiti amehakiki riwaya nne: Msimu wa Vipepeo, Dharau ya Ini, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi. Nadharia ya hejemonia inayoweka wazi suala la utawala wa mabwanyenye juu ya raia na kueleza udumishaji wa uwezo na mamlaka juu ya watawaliwa ni mwafaka katika utafiti huu. Mintarafu ya nadharia hii, hejemonia huendelezwa na kudumishwa sio tu kwa ushurutishaji bali pia kupitia maafikiano, lugha, wataalamu, siasa, maagizo, burudani, ujumbe na nyenzo nyingine za kielimu. Riwaya teule ziliteuliwa kimakusudi kwa kudhamiria kuwa zimesheheni masuala ya uhimili wa hejemonia. Kutokana na riwaya hizo, mtafiti alipata mitazamo mipana na tofauti ya propaganda kwa mujibu wa nguzo za nadharia na madhumuni ya utafiti. Utafiti huu ni wa maktabani ambako usomi mpana na wa kina wa riwaya teule, vitabu vya ziada, majarida na tasnifu mbalimbali ulitekelezwa. Utaratibu wa upekuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data huku mbinu ya kiuthamano ikitumika kuchanganua data hiyo. Muundo wa kimaelezi ulitumika kuchanganua data na kueleza matukio kwa uyakinifu. Utafiti umeonesha kuwa propaganda ni mkakati muhimu unaotumiwa na watu wenye uwezo na mamlaka kudumisha na kuhimili hejemonia katika jamii. Matokeo ya utafiti yanatoa maarifa zaidi kuhusu matumizi ya propaganda kama mkakati wa kuhimili hejemonia katika fasihi. Aidha, matokeo haya ni marejeleo muhimu kwa wahakiki na watafiti hususan wale wanaotafitia masuala ya hejemonia katika fasihi

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Agnew, J. (2005). Hegemony: The New Shape Of Global Power. PHILADELPHIA: Temple University Press. http://www.jstor.org/stable/j.ctt14bsxmk

Artz, L., & Murphy, B. O. (2000) Cultural Hegemony in the United States. California: Sage Publications.

Bartlett, F. C. (1940) The aims of Political Propaganda. Octagon: New York.

Bernays, E. (1928) Propaganda. New York: Liveright.

Chomsky, N., & Herman, E. (1988) Manufacturing Consent: The Political Economy of the Mass Media. New York: Pantheon.

Fontana, B. (2008) ‘Hegemony and Power in Gramsci’ in Howson, R. and Smith, K. (eds), Hegemony: Studies in Consensus and Coercion, Routledge, New York.

Gramsci, A. (1995) Further selections from the prison Notebooks. Edited and translated by Derek Boothman. Minneapolis: University of Minnesota press.

Gramsci, A. (1978) Selections from the Political writings 1921-1926, Lawrence and Wishart, London.

Gramsci, A. (1971) Selections from the prison Notebooks. Q. Hoare and G.N. Smith, eds and trans. London. Lawrence and Wishart.

Hummell, W. &, Huntress K. (1949) The Analysis of Propaganda. New York: Holt, Rinehart and Winston.

Lee, A. (1953) How to Understand Propaganda. New York: Rinehart.

Lippmann, W. (1927) The Phantom Public. New York: Macmillan.

Nella, P. (2017) The Many Faces of Power: The Portrayal of Hegemony in Fight Club by Chuck Palahniuk and American Psycho by Bret Easton Ellis. University of Tamperes Press.

Ross, S. T. (2002) Understanding Propaganda: The Epistemic Merit Model And its Application to Art. The Journal of Aesthetic Education. Spring 2002, Vol 36. No 1 pp. 16-30. University of Illinois Press.

Tarehe ya Uchapishaji
30 Mei, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Ogutu, H. (2022). Propaganda Kama Mkakati wa Kuhimili Hejemonia: Mfano wa Dharau ya Ini, Msimu wa Vipepeo, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 142-150. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.686