Muundo wa Mazungumzo ya Uuzaji na Ununuzi wa Nguo za Mitumba katika Soko Mjinga Kaptembwo
Ikisiri
Mazungumzo ndio njia mojawapo ya kuchochea maingiliano baina ya watu. Lugha ya mazungumzo hutokea katika miktadha mbalimbali kama vile shuleni, hospitalini na hata nyumbani. Utafiti huu uliangazia mpangilio na nafasi ya muundo wa mazungumzo. Wanaojihusisha na mazungumzo haya ni muuzaji na mnunuzi. Lengo la makala haya ni kubainisha namna matumizi ya lugha ya kuafikiana bei wakati wa kuuza na kununua huathiri muundo wa mazungumzo. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni Uchanganuzi wa Mazungumzo iliyoasisiwa na Sacks (1960). Kuonyesha kuwa, mazungumzo yanayotekelezwa na binadamu huwa na mpangilio maalum. Utafiti huu ulichunguza muundo wa mazungumzo katika soko la mtumba. Matokeo yake yalibainisha kuwa muundo wa mazungumzo haukuweza kufuatwa kwa wakati mwingi kikamilifu, kupashana zamu katika mazungumzo kulipewa kipau mbele, nguo za wanawake na watoto zilinunuliwa sana zikilinganishwa na za kiume na tabia za wanunuzi kutoka katika jamii na kabila tofauti kimazungumzo zilijikita katika utamaduni aliolelewa nayo.
Upakuaji
Marejeleo
Garfinkel, H. (1952). Ethnomethodology and Workplace Studies. Sage Journals, 233-261.
Goffman, E. (1967). Interaction ritual: essays on face-to-face interaction. Aldine: American Psychological Association.
Grundy, P. (2000). Doing Pragmatics 2nd. London: Arnold Publishers.
Heritage, J. (1984). Garfinkel and ethnomethodology. Cambridge: Policy Press.
Liddicoat, J. (2000). Everyday Speech as culture: Implications for language teaching, in Teaching Languages, Teaching cultures (eds. A.J Liddicoat and C.Crozet), Applied Linguistics Association of Autralia, Canberra, pp 51-64.
Sacks, H., Schegloff, E., & Jefferson, G. (1974). A simplest systematics for the organisation of turn taking for conversation. Language, 696-735.
Shegloff, E. A. (2007). Sequence Organization in Interaction: A Primer in Conversation Analysis: Vol.I. Cambridge, New York: Cambridge University Press.
Schegloff, A., & Sacks, H. (1973). Opening up closings. Semiotica, 289-327.
Schegloff, E., Jefferson, G., & Sacks, H. (1977). The preference for self-correction in organisation of repair in conversation. Language, 361-382.
Yule, G., & Brown, G. (1983). Discourse Analysis. United Kingdom: Cambridge University Press.
Yule, G. (1972). Pragmatics. New York: Oxford University Press.
Copyright (c) 2022 Gideon K ipyegon Rono, Catherine Kitetu, PhD, Abdulrahim Hussein Taib Ali

This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.