Utomilisi wa Lugha kama Chanzo cha Ubadilishanaji Msimbo Miongoni mwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu katika Kaunti ya Kiambu

  • Beatrice Njambi Mwai Chuo Kikuu cha Umma
  • Leonard Chacha, PhD Chuo Kikuu Cha Kenyatta
Keywords: Kubadili msimbo, Umilisi wa Lugha, Utomilisi wa Lugha, Wingi Lugha
Sambaza Makala:

Ikisiri

Utafiti huu ulichunguza swala la kubadili msimbo miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu Kaunti ya Kiambu. Fikra kuu iliyoongoza utafiti huu ni kuwa wanafunzi hao hubadili msimbo kwa sababu ya utomilisi wa lugha. Hawana umilisiwa lugha mojaKwa mfanoutafiti huu umeangazia lugha za Kiingereza na Kiswahili. Tumedhihirisha kuwa hawa ni wanafunzi wa chuo kikuu lakini hawawezi kuwasiliana kwa lugha moja kwa ufasahalazima waingie katika lugha nyingine ili kufanikisha mawasiliano. Kwaanokama wanatumia lugha ya Kiswahili wanabadilisha na kuingia katika lugha ya Kiingereza kwa sababu wameshindwa kuendeleza mazungumzo katika lugha ya Kiswahili. Utafiti huu umeongozwa na nadharia tambulishi iliyopendekezwa na Myers-Scotton (1983). Kulingana na Myers-Scottonkatika mawasiliano yoyote, kuna hali ya alama inayotambulika na isiyotambulika. Katika kuchagua alamamzungumzaji huchagua alama kulingana na mahitaji ya kijamii. Pia huonyesha kuwa kubadili msimbo ni kwa sababu ya ugumu wa watu kutumia lugha moja na ugumu huo uko akilini mwa mzungumzaji. Utafiti huu umeegemea maktabani na nyanjani. Maktabaniutafiti huu umenufaika kwa kupata data kutoka kwa machapisho, vitabu na majarida kuhusu dhana ya kubadili msimbo, uwili lugha na misingi ya nadharia. Nyanjaniutafiti huu umefanywa katika Kaunti ya Kiambu, Utafiti huu umehusisha matumizi ya vifaa kama vile mwongozo wa mahojiano na kuhudhuria vikao rasmi ambavyo vijana wanawasiliana. Data iliyochanganuliwa kwa mujibu wa nadharia tambulishi imewasilishwa kwa njia ya maelezo

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Appel, R., & Muysken, P. (1987). Language contact and bilingualism. London: Edward Arnold. When contact speakers talk, linguistic theory listens, 239.

Gachinu, J. N. (1996) Linguistic Aspects of Code switching in Gikuyu, Kiswahili and English. (Unpublished MA Thesis Kenyatta University).

Gumperz, J. (1982). Discourse Strategies. Cambridge: Cambridge University Press.

Hudson, R. (1980). Sociolinguistics. Cambridge : Cambridge University Press.

Kachru, B. B. (1977). “Code- switching as a Communicative Strategy in India”. Saville- Troike, Muvie (wah). Linguistics and Anthropology. Washington. Georgetown University.

Kanana, F. E. (2003). “Code Switching in Business Transactions. A Case Study of Linguistic Repetroire in Maasai Market in Nairobi”, Kenya. (Unpublished M.A. Thesis) Kenyatta University.

Munuku, A. W. (2005). Code Switching in the Contemporary Kiswahili Rap Song. (Unpublished M.A. Thesis) Kenyatta University.

Muthuuri, D. G. (2000). Code Switching Among Kenyatta University Multilingual Community. Nairobi, Kenya. (Unpublished M.A. Thesis) Kenyatta University.

Muthwii, M. J. (1986). Language Use in Pluri-lingual Societies. The Significance of Code Switching English/Kalenjin. (Unpublished M.A Dissertation) University of East Angalia.

Myers-Scotton, C. (1993). Social Motivations for Code Switching. Evidence from Africa. Oxford: Clarendon Press.

Ndegwa, A. F. (2009). Functional and Patterns of Code Switching in Nairobi Based Radio Stations. (Unpublished M.A Thesis) Kenyatta University.

Nthiga, P.M. (2003). Patterns and Functions of Code Switching in Pre- Primary classroom Discourse in selected schools at Kasarani Division Nairobi. (Unpublished M.A Thesis) Kenyatta University.

Scotton, M. and Ury, W. (1977). “Bilingual Strategies: The Social Functions of Code Switching”. International Journal of the Sociology of Languages, vol.1

Parkin, D. J. (1974). Language switching in Nairobi. Nairobi: Oxford University Press.

Tarehe ya Uchapishaji
21 Aprili, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Mwai, B., & Chacha, L. (2022). Utomilisi wa Lugha kama Chanzo cha Ubadilishanaji Msimbo Miongoni mwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu katika Kaunti ya Kiambu. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 64-72. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.627