Utekelezaji wa Mitalaa ya Kiswahili Vyuoni na Namna Unavyoathiri Utendakazi wa Walimu Wanaofundisha katika Shule za Upili

  • Jackline Mwanzi Chuo Kikuu cha Kibabii
  • Odeo Isaac Ipara, PhD Chuo Kikuu cha Kibabii
  • Kenneth Inyani Simala, PhD Chuo Kikuu cha Kibabii
Keywords: Mitalaa, Utekelezaji, Utendakazi, Walimu
Sambaza Makala:

Ikisiri

Walimu wanaofundisha katika shule za upili hupata mafunzo yao ya kitaaluma kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali. Wanapoandaliwa vyuoni, walimu hawa hupewa mafunzo kwa kutumia mitalaa tofauti inayoandaliwa katika vyuo vikuu hivyo. Baada ya kuhitimu, wao hutarajiwa kuutekeleza mtalaa mmoja unaoandaliwa na Taasisi ya Ukuzaji Mitalaa nchini Kenya (TUMIKE) ili ufundishwe katika shule zote za upili. Utafiti ulifanywa ili kudhihirisha iwapo mafunzo ya kitaaluma yanayotolewa vyuoni kuwaandaa walimu wa somo la Kiswahili yanawapa maarifa na stadi wanazohitaji kufundisha katika shule za upili baada ya kuhitimu. Makala haya yametokana na utafiti uliofanywa ili Kutathmini uhusiano baina ya mitalaa ya Kiswahili inayotumika katika vyuo vikuu vya umma nchini  Kenya na mtalaa ambao umeandaliwa na TUMIKE ili kutekelezwa katika shule za upili. Utafiti ulifanyika katika vyuo vikuu vitano vya umma nchini Kenya. Muundo wa utafiti ulikuwa usoroveya elezi. Data ilikusanywa kwa njia ya usaili, uchanganuzi wa nyaraka na hojaji. Uchanganuzi wa data ulikuwa wa kitakwimu na kimaelezo. Utafiti uligundua kuwa uhusiano baina ya mitalaa rasmi ya Kiswahili ya vyuo vikuu vya umma na mtalaa wa Kiswahili wa shule za upili siyo wa moja kwa moja. Hali hii iliathiri utendakazi wa walimu walipotekeleza mtalaa wa shule za upili. Uhusiano mdogo uliopo baina ya mitalaa rasmi ya vyuo vikuu na mtalaa rasmi wa TUMIKE ulidhihirika kwa kuchunguza vipengele vikuu vya mtalaa ambavyo ni: malengo, mada, utekelezaji na tathmini. Utafiti unapendekeza pafanyike marekebisho ya mara kwa mara ya mtalaa wa TUMIKE kwa kuwahusisha walimu na waandalizi wao ili wakadirie malengo, mada, mbinu za utekelezaji na tathmini mintarafu maandalizi yanayotolewa kwa walimu.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Adegoke, K. A. (2010). Why Teacher Education Model Holds the Most Promise for the Nigerian Educational System? Convocation Lectures for St. Augustines College of Education Akoka, Lagos, Nigeria, pp. 1-23.

Asiimwe, C. (2019). Mikabala ya Kufundisha. Katika: Simala, K. I (Mh.). Mitaala ya Kiswahili katika Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki. Zanzibar: Kakama.

Bilbao, P. P., Lucido, P. I., Iringan, T. C., and R. B. Javier (2008). Curriculum Development. Quezon city: Lorimar Publishing, IncBobbit F. (1918). The Curriculum. Boston: Houghton Mifflin.

Brown, J. D. (1995). The Elements of Language Curriculum. A Systematic Approach to Program Development. Boston, MA: Heinle publishers.

Eisner, E (2002). The Educational Imagination: On The Design and Evaluation of School Programs. Upper Saddle River, N. J.: Prentice Hall.

Eshiwani, G.( 1993) Education in Kenya Since Independence. East African Educational Publishers, Nairobi.

Flowerdiew, J and Peacock, M. (Eds.). (2001). Research Perspectives on English for Academic Purposes. Cambridge. Cambridge University Press.

Goodlad, J. I. (1995). Ralph Tyler: The Educators’ Educator. Educational Policy, 29(1), 75-81

Goodlad, J. I. (1984). A Place Called School: Prospects for the Future. New York: McGraw Hill.

Hedge, T. (2002). Teaching and Learning in the Language Classroom (3rd Ed). Oxford: Oxford University Press.

Kafu, P. A. (2013). Teacher Education: the Incubator of Science and Technology for Development in Africa. African Journal of Education Science of Technology (AJEST), 1(1), 1-14.

King’ei, K. (2001). From the Real to the Ideal: Survey of Kiswahili Curricular in East Africa’s Universities. Kiswahili in the 21st Century,179 2000 Publisher for Advanced Studies of African Society.

Lynch, D. E. (2003). So You Want to Make a Real Difference: An Introduction to Learning Management for the Teacher in Training. Monograph: Central Queensland

Makoti, V. (20017). Ufundishaji wa Kiswahili na Changamoto zake Mintaarafu Chuo Kikuu cha Moi. Katika Jarida la Mwanga wa Lugha. Juzuu Na. 1, uk. 111 – 122.

Mbuthia, F. K. (1996). Comparative Study of the Effects of Two Instructional Approaches on Students’ Performance in Kiswahili Poetry in Selected Secondary Schools in Eldoret Municipality. Unpublished Master’s Thesis, Moi University.

McArthur, L. Z. and Baron, R. M. (1983). Toward an Ecological Theory of Social Perception. Psychological Review, 90(3), 215–238.

Miller, L and Silvernail, D. (2000). Learning to Become a Teacher: the Wheelock way. In L. Darling Hammond (Ed), Studies of Excellence in Teacher Education. Preparation in the Undergraduate Years. Washing D.C: American Association of college for teacher education.

Musau P. (2002). Polemics Versus Reality: Bridging the Gap in Kiswahili Research. In: K.Inyani Simala(Mh.) Utafiti wa Kiswahili.CHAKITA. Eldoret, Moi University Press.

Musungu, L. L. and Nasongo, J. W. (2008). The Head-teacher’s Instructional Role in Academic Performance in Secondary Schools in Vihiga District, Kenya. Educational Research and Review, 3(10), 316-323.

Mutiga, J. (2008). Nature and Nurture: Tenets in the Acquisition of Kiswahili as a Second Language in the Kenyan Bilingual System of Education. In: Ogechi,N. et.al (eds).Nadharia katika Taaluma ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika (pp.397-405) ISBN 9966-854-47-9, Moi University.

Nasimiyu, G, (2017). Preparation of Teacher Trainees in Pedagogy in Kenyan Universities. Journal of Education and Practice,V8 n 13 pg 28-34.

Oliver, A. I. (1982). Curriculum improvement. A guide to problems, principles and processes. (2nd ed.) New York: Harper & Row Publishers.

Oluoch G. P. (2006). Essentials of Curriculum Development. Nairobi Longhorn Publishers.

Otunga, R. N. (2010). The Dilemma of Curriculum Relevance in Kenya. Eldoret: Moi University Press.

Oyedeji, N. B. (1998). Management in Education, Principles and Practice. Lagos: Aras Publishers.

Shiundu, J. S. and Omulando, S. J. (1992). Curriculum: Theory and Practice in Kenya. Nairobi: Oxford University Press.

Simala K. I. (2019). Uhuishaji wa Mitaala ya Kiswahili katika Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki. Katika: Simala, K. I. (Mh.). Mitaala ya Kiswahili katika vyuo vikuu vya Afrika Mashariki. Zanzibar: Kakama.

Simala, K. I. (2013). Critical Pedagogy and Kiswahili Education. Challanges and way Forward. In: Egara K. na wengine. New Horizons in Pedagogy. Kakamega. MMUST University, Kenya.

Simala, K. I. (2002). Miradi ya Utafiti katika Vyuo Vikuu Mnamo Karne ya Ishirini na Moja. Katika: Simala K. I. (Mh) Utafiti wa Kiswahili. Eldoret: Moi University Press

Sitima, T. M. (1995). Maintainance of Standards in Teacher Education. In: Ministry of Education. Report of Proceedings of the 3rd Teacher Education Conference. Nairobi, Jomo Kenyatta Foundation.

Taba, H, (1962). Curriculum Development. New York: Hacourt, Brace and World.

Taba, H. (1962). Curriculum Development Theory & Practice. New York. Harcourt: Brace & World.

Tyler, R. W. (1949). Basic Principles of Curriculum and Instruction. Chicago: University of Chicago Press.

University of Nairobi. (1978). A Review of Graduate Teacher Evaluation in Kenya. Nairobi: University of Nairobi.

UNESCO (2011). The Hidden Crisis: Armed Conflict and Education. Background paper prepared for Education for All Global Monitoring Report.Paris, UNESCO.

Urevbu, A. O. (1994). Curriculum Studies (2nd ed.). Singapore: Longman.

Urevbu, A. O. (1985). Curriculum Studies. Ikeja: Longman.

Wagari, S. (2003). Problems Facing Teacher Education in Kenya: A Case Study of Teaching Practice in the University of Nairobi. Unpublished Master’s Thesis, University of Nairobi.

Tarehe ya Uchapishaji
29 September, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Mwanzi, J., Ipara, O., & Simala, K. (2022). Utekelezaji wa Mitalaa ya Kiswahili Vyuoni na Namna Unavyoathiri Utendakazi wa Walimu Wanaofundisha katika Shule za Upili. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 5(1), 25-38. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.556