Ishara Bwege Katika Diwani ya Kichomi

  • Chibayi Jason Poyi Chuo Kikuu cha Laikipia
Keywords: Ishara, Ubwege, Mtindo, Sawiri
Sambaza Makala:

Ikisiri

Wasomi na watafiti wanadai kwamba ishara ni sehemu muhimu ya mtindo. Wanakubaliana kwamba ishara ni kigezo muhimu katika kufasiri maisha bwege. Ishara huonyesha hali halisi ya maisha bwege ya binadamu. Kwa hivyo, makala haya yananuia kuhakiki ishara zilizotumika kuashiria ubwege wa maisha katika diwani ya Kichomi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Mtindo iliyoasisiwa na Leech ambayo itasaidia katika kuhakiki ishara zilizotumika kuibua ubwege wa maisha katika mashairi teule ya diwani ya Kichomi.  Ishara zilifafanuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo yaliyoegemezwa kwenye mihimili teule ya nadharia ya Mtindo. Uchanganuzi wa ishara uliongozwa na mbinu ya uhakiki matini. Katika diwani ya Kichomi, Kezilahabi anaangazia ubwege kwa njia ya kifalsafa na usanii wa hali ya juu kwa kutumia ishara maalumu. Mtafiti alihakiki matumizi ya ishara kwa namna ambavyo yalitumika kuangazia ubwege. Makala haya yatawafaa waandishi wa fasihi hasa ushairi kwani yatawawezesha kuelewa mbinu mbalimbali za kuandika matini zenye mvuto wa kisanaa ili kuwasilishia jamii ujumbe kwa ubunifu mkubwa.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.
Tarehe ya Uchapishaji
26 October, 2021
Jinsi ya Kunukuu
Poyi, C. (2021). Ishara Bwege Katika Diwani ya Kichomi. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 4(1), 12-29. https://doi.org/10.37284/jammk.4.1.446