Mwanamke wa Kiswahili katika Utenzi wa Mwanakupona

  • Sheila Pamela Wandera-Simwa, PhD Chuo Kikuu cha Laikipia
Keywords: Mwanamke wa Kiswahili, Uhalisia, Karne ya Kumi na Tisa, Utamaduni wa Waswahili
Sambaza Makala:

Ikisiri

Makala hii inahakiki taswira ya mwanamke wa Kiswahili katika Utenzi wa Mwanakupona kwa kuzingatia utamaduni wa Waswahili wa karne ya kumi na tisa, ambao ndio wakati uliotungwa utenzi huu. Picha ya mwanamke huyu imehakikiwa kwa namna ambavyo inamulika mwanamke wa Kiswahili wa karne hiyo. Pamoja na kuusoma Utenzi wa Mwanakupona, tutahakiki kuhusu utenzi huu, na maandishi kuhusu utamaduni wa Waswahili wa karne ya kumi na tisa, mtafiti aliwahoji Waswahili watajika, wake kwa waume, kuhusu mwanamke katika utamaduni wa Waswahili. Pia, aliwasaili washairi wasifika na wanawake wa Kiswahili kuhusu uelewa wao wa utenzi huu. Yote haya kwa pamoja yalitoa mwanga kuhusu nafasi ya mwanamke katika utenzi huu maarufu. Nadharia ya uhalisia ilitumikizwa katika uhakiki huu na ilibainika kuwa mwanamke katika Utenzi wa Mwanakupona ni picha halisi ya mwanamke wa tabaka la juu, wa karne ya kumi na tisa.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abdulaziz, M. H. (1979). Muyaka 19th Century: Swahili Popular Poetry. Nairobi: Kenya Literature Bureau

Allen, J. W. T. (1971). Tendi. Bungay: Richard Clay Ltd.

Bakari, M. (1978) “The State of the Art: Swahili Literature in the Nineteeth Century”. Journal of Historical Association of Kenya..

Doi, A. R. I. (1994). Woman in Shariah (Islamic Law). London: Ta-Ha Publishers Ltd.

Gibbe, A. G. (1993). “Women and the Making of Swahili Literature in East Africa”. Makala ya OSSREA

Herilinger, M. (1979). Women and State Socialism. London:Macmillan Press.

Jahadhmy, A. A. (1975) Kusanyiko la Mashairi. Kenya Litho Ltd.

Kateregga, D. B. (1984). “Teaching on the Status of Women in Islam” katika The Islamic Journal, 2/6/84. Ramadhani 104.

Kenyatta, J. (1938). Facing Mount Kenya: The Tribal Life of the Kikuyu. London: Secker and Warbug

Khatibu, M. S. (1985). “Utenzi wa Mwanakupona”. Makala katika MULIKA Na. 17. TUKI

Maududi, M. (1972). Purda and the Status of Women in in Islam. Lahore: Islamic Publications.

Mohammed, S. A. (1980). Utengano. Nairobi. Longman Publishers

Momanyi, C. (1991). “Matumizi ya Taswira kama Kielelezo cha Uhalisi katika Utenzi wa Al-Inkishafi.” Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Muindi, A. (1990). “Usawiri wa Wahusika Makahaba katika vitabu vya Said Ahmed Mohammed.” Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Mulokozi, M. M. (1975). “Ushairi wa Kiswahili ni nini?” katika LUGHA YETU: Tuisome Tuijue.

Ndungo, C. (1985). “Wanawake na Mabadiliko ya Kihistoria”. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Rodney, W. (1972). How Europe Underdeveloped Africa. London: Rogle-L’Ouverture Publishers

Stigand, C. H. (1913) The Land of Zinj. London: Constial & Co Ltd.

Strobel, M. (1975). “Muslim Women in Mombasa: Kenya 1890-1973”. PhD thesis, Yale University

Wandera, S. P. (1996). “Usawiri wa Mwanamke katika Ushairi wa Kiswahili: 1800-1900: Uhalisi au Ugandamizwaji?”. Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Egerton.

Wandera-Simwa, S. P. (2015). “Taswira za Jinsia katika Hadithi za Wanyala (Mumbo)”. Tasnifu ya Uzamifu. Chuo Kikuu cha Laikipia.

Tarehe ya Uchapishaji
28 September, 2022
Jinsi ya Kunukuu
Wandera-Simwa, S. (2022). Mwanamke wa Kiswahili katika Utenzi wa Mwanakupona. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 4(1), 82-98. https://doi.org/10.37284/jammk.4.1.422