Kupambanua Mbinu za Uwakilishi wa Uhalisia-Ajabu Katika Mustakabali wa Uongozi Barani Afrika Katika Karne ya 21 Katika Riwaya ya Babu Alipofufuka.

  • Grace Adhiambo Onyango Chuo Kikuu cha Mount Kenya
  • Onesmus Gitonga Ntiba, PhD Chuo Kikuu cha Mount Kenya
  • Rocha Mzungu Chimerah, PhD Chuo Kikuu cha Pwani
Keywords: Kupambanua, Uwakilishi, Karne, Riwaya, Mustakabali na Afrika, Babu Alipofufuka, Uhalisia-Ajabu
Sambaza Makala:

Ikisiri

Sanaa za kihalisia-ajabu husheheni usimulizi wa matukio yasiyotafsirika wala kufikirika kuwa na uyakinifu katika maisha ya mwanadamu. Fasihi za aina hii hutilia nguvu umazingaombwe na kukiuka uhalisia. Riwaya ya Babu Alipofufuka ya Mohamed ni mfano mojawapo wa fasihi yenye uhalisia-mazingaombwe. Utafiti huu unapambanua mkabala huo kwa kusimikwa kwenye mada Mustakabali wa Uongozi katika bara la Afrika katika karne ya 21: Tathmini ya Uhalisia-ajabu katika Riwaya ya Babu Alipofufuka na Said Ahmed Mohamed. Malengo ya utafiti huu ni; Kupambanua uhalisia-ajabu na uozo wa uongozi na hatimaye kutambua suluhu kwa matatizo ya uongozi barani Afrika kwa mujibu wa riwaya ya Babu Alipofufuka. Uchunguzi katika kazi hii uliongozwa na nadharia ya uhalisia-ajabu kwa kujifunga kwa mihimili yake mitano: kinaya, uandishi ndani ya uandishi, umazingaombwe katika mukhtadha halisi, vurugu la kiwakati na muingilano wa matini. Utafiti wenyewe uliendeshwa kwa mtindo wa kimakusudi ambapo matini maalum zilichanganuliwa maktabani na vile vile mtandaoni. Mbinu ya uchanganuzi ilihusu yaliyomo katika riwaya ya Babu Alipofufuka. Mhakiki pia alilenga kuchanganua kazi nyingine za fasihi kwa misingi ya malengo ya utafiti huu. Matokeo ya uchunguzi huu yana umuhimu mkubwa kwani yatasaidia kuchunguza suala la uongozi katika kutatua matatizo ya ndani kwa ndani kwa mustakabali wa itikadi za Kiafrika. Uchunguzi huu unashikilia kuwa utandawazi ni nduli ambalo limechangia kuwepo kwa matatizo humu barani na kuzidi kuifanya Afrika kunyongeka katika minyororo ya utumwa mpya. Taswira hii ni dhahiri katika riwaya mpya za Kiswahili. Matokeo yake bila shaka yatapevua ufahamu kuwa Afrika ina itikadi za kijadi ambazo zilizingatiwa katika kutafuta suluhu kwa matatizo ya ndani kwa ndani hasa za kisiasa. Wanafunzi wa shule za upili na vyuo vikuu pia watanufaika na matokeo ya uchunguzi huu kwa kupata mwelekeo wa uhakiki wa kazi za fasihi mintarafu zenye uhalisia-ajabu.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Bergonzi, B. (1972). The Situation of The Novel. London, Nenguin Publishers.

Crafts, N. (2000). Globalisation and Growth in 20th Centuary. Washingtone DC, IMF, Working Paper WP/00/44.

Gromov, M. D. (1998). Nagona and Mzingile Novels, Tale or Parable. Swahili ForumVAAP No. 55.

Jauch, H. (ed.). (2001). Playing the Globalisation Game: The Implications of Economic Liberalisation for Namibia. Windhoek, Labour Resource and Study Institute.

Kezilahabi, E. (1985). African Philosophy and the Problem of Literary Interpretation. Madison, University of Winsconsin.

Kezilahabi, E. (1990). Nagona. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.

Khamis, S. A. M. (2005). “Vionjo Vya Riwaya Mpya ya Kiswahili.” Research in African Literatures 36/1: 92-108. Bayreuth: Bayreuth University.

Khamis, S. A. M. (2007). “Utandawazi au Utandawizi: Jinsi lugha ya Riwaya Mpya ya Kiswahili Inavyodai.” African Journalism Online Vol 70: SWAHILI FORUM 14: 165-180

Lindfors, B. (1981). Ngugi wa Thiong'o's early journalism. Journal of Postcolonial Writing, 20(1), 23-41. ¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬

Mbatiah, M. (1990). Dhana ya Kukua Kwa Mwandishi Kama Inavyodhihirika Katika Kazi za S. Robert na S.A Mohamed. Tasnifu ya Uzamili ambayo haijachapishwa. Nairobi: Chuo Kikuu Cha Nairobi.

Mohamed, S. A. (1981). ‘‘Kupatana na Riwaya zangu.’’ Mwamko 2. Jarida la Chama cha Kiswahili Chuo Kikuu cha Nairobi.

Mohamed, S. A. (2002). Babu Alipofufuka. Nairobi: J. K. Foundation.

Njogu, K. na Chimerah, R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Nyerere, J. (1962). Hotuba kuhusu utamaduni. Retrieved http://www.lukomwalange.blogspot.com on 13/3/2013, 1:30pm.

Pillai, P. (2011). Negative Effects of Globalisation. At http://www.buzzle.com/author. retrieved on 13/2/2013, 12:20pm.

TUKI (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Oxford University Press.

TUKI (2006). English –Swahili Dictionary. University of Dar es Salam, Institute of Kiswahili Study.

Walibora, K. (1996). Siku Njema. Nairobi: Longhorn Kenya.

Walibora, K. (2010). “Uhalisia na Uhalisiamazingaombwe: Mshabaha kati ya Dunia Yao na The Tin Drum.” SWAHILI FORUM 17. Uk 143-157. Mainz: Johannes Gutenberg University.

Wamitila, K. W. (2002). Bina-Adamu!. Nairobi, Phoenix Publishers.

Tarehe ya Uchapishaji
16 September, 2021
Jinsi ya Kunukuu
Onyango, G., Ntiba, O., & Chimerah, R. (2021). Kupambanua Mbinu za Uwakilishi wa Uhalisia-Ajabu Katika Mustakabali wa Uongozi Barani Afrika Katika Karne ya 21 Katika Riwaya ya Babu Alipofufuka. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 3(1), 124-131. https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.413