Urudiaji wa Kisarufi Katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari Bin Darimi

  • Aloo Ronald Odhiambo Chuo Kikuu cha Nairobi
  • Kineene wa Mutiso, PhD Chuo Kikuu cha Nairobi
Keywords: Urudiaji, Usambamba, Antistrofia, Epimoni, Haipozesia
Sambaza Makala:

Ikisiri

Katika makala haya, tumechunguza aina na mchango wa urudiaji wa kisarufi katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari bin Darimi. Ili kufanikisha hili, tumeongozwa na nadharia ya Umtindo ambayo inachunguza na kutoa fasiri kwa kazi za isimu na fasihi. Hii ni kwa sababu uchunguzi wa vipengele vya kifasihi hauwezi kujisimamia. Nadharia ya Umtindo inahusishwa na Geoffrey Leech katika mwaka wa 1969 kutokana na kazi yake ya kwanza ya ushairi alioandika huku akizingatia mawazo ya nadharia hii. Lengo la uhakiki wetu ni kuweka wazi aina mbalimbali za urudiaji wa kisarufi zilizotumiwa katika utenzi huu na michango yake katika kufanikisha fani na maudhui kwenye utungo huu. Baada ya uhakiki wetu, tumegundua kuwa urudiaji wa kisarufi unachangia maudhui, wahusika, vipengele vya kimtindo na vipengele vingine vya fani kwa ujumla katika utungo huu. Isitoshe, urudiaji huu wa kisarufi umekuwa na umuhimu katika kuleta mwangwi na usisitizaji. Tumetumia maelezo na ufafanuzi kutoka katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari bin Darimi kama njia ya kubainisha haya.

Upakuaji

Bado hatuna takwimu za upakuaji.

Marejeleo

Abrams. M. H. (2015). A Glossary of Literary Terms. New York: Cengage Learning, Inc.

de Beaugrande, R. A. & Dressler, W. U. (1981). Einfuhrung in die TexHinguistick (Konzepte Sprach-Und Literaturwissenschaft28). Tubingen: Niemeyer.

Croft, S. & Robert, M. (2000). Exploring Language of Literature. London: Oxford University Press.

Leech, G. N. (1969). A Linguistic Guide to English Poetry. London: Longman Group.

Msokile, M. (1992). Kunga za Fasihi na Lugha. Dar es Salaam: Educational Publishers and Distributors Limited.

Swann, R. & Side Wink, J. (1934). The Making of English Verses. London: Oxford University Press.

Wamitila, K. W. (2003). Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus publishers. (2008). Kanzi ya Fasihi l: Msingi wa Uchanganuzi wa Kiswahili wa Fasihi. Nairobi: Vide- Muwa Publishers Ltd.

Wamutiso, K. (2014). “Number Symbolism (nos. 1, 4, 7 and 1,000) in Swahili Poetry: The case of Utenzi wa Fatumah”, Kiswahili Vol. 77, pp. 132-148.

Tarehe ya Uchapishaji
9 Septemba, 2021
Jinsi ya Kunukuu
Odhiambo, A., & wa Mutiso, K. (2021). Urudiaji wa Kisarufi Katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari Bin Darimi. Jarida La Afrika Mashariki La Masomo Ya Kiswahili, 3(1), 100-107. https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.404